Freesoule
JF-Expert Member
- Jun 18, 2013
- 269
- 272
TANESCO, kuna malalamiko sehemu mbalimbali za nchi kuhusiana na mpango wa usambazaji umeme vijijini (REA) ila sauti za wananchi zimekosa uwakilishi. Nitazungumzia yale niliyoyaona huko Rungwe, katika vijiji vya kata ya Kalalo.
Sehemu nyingi umeme waliunganishiwa watu wachache tu, tena wale wa barabarani, ili viongozi wakipita wafikiri wananchi wa eneo husika wamepata huduma ya umeme. Sijui kama kuna ukaguzi wa aina yoyote hufanyika, na kama upo basi wahusika huwa hawafanyi kazi inayoridhisha hata kwa nusu asilimia. Zaidi ya asilimia 99 ya kaya bado zilikuwa gizani pale mpango wa REA kwa eneo hilo ulipotangazwa 'kumalizika'. Wengi wa waliopata umeme baadaye wametumia gharama zao wenyewe, tena mara nyingi kwa kutoa rushwa kwa wafanyakazi wa TANESCO.
Pia, kuna sehemu wananchi walichangishwa fedha ili kuunganishiwa umeme (wakati umeme wa REA ni bure), na wengine walichangishwa fedha hadi Tsh 150 000 ili kusukiwa umeme kwenye nyumba zao, kinyume kabisa na utaratibu. Wajibu wa TANESCO/REA ni kuwafikishia umeme wateja, usukaji wa umeme ndani ya nyumba si jukumu lao, ni jukumu la mteja husika. Lakini wafanyakazi wasio waadilifu wa TANESCO/REA walitumia mwanya wa uelewa mdogo wa wananchi kuwachangisha fedha za kuwasukia umeme, kinyume na utaratibu. Wakipokea pesa wanakufungia 'distribution box' (almaarufu 'main switch' kama ijulikanavyo kwa wengi wetu), soketi moja ya taa sebuleni na pengine soketi ya ukutani. Wale waliosuka umeme kwa gharama zao walitozwa faini na watu wa TANESCO/REA wakishirikiana na wenyeviti wa vijiji na mitaa. Fedha zote hizi hazikutolewa risiti, kwa hiyo hazikuingia kwenye mfuko wowote wa umma. Fedha za watu masikini, ambapo kwa umasikini wao wafadhili waliamua kuwafadhili kwa umeme wa bure kupitia mradi wa REA, zilitafunwa na wajanja bila huruma. Hata hivyo waliishia kutokupata umeme.
Haya yote yametokea katika vijiji vya kata ya Kalalo wilayani Rungwe. Wananchi wamepitia madhila yote hayo na bado hawajapata umeme huu mwaka wa pili. Wakidai kuwekewa umeme huambiwa 'phase ya REA' ilishapita. Kwa maana hiyo, wakitaka kupata umeme itabidi watumie gharama zao wenyewe.
Ni muhimu sana kwa TANESCO kufuatilia ufanisi wa mpango wa REA kwa nchi nzima, kufanya ukaguzi makini na siyo kuwatuma watu wanaochoma petroli kwenye 'malendi kruza ya mkonga' na kusema kila kitu kiko sawa. Wafanyakazi wengi wa TANESO na mawakala wa REA wasio waadilifu wamehusika kwa kiasi kikubwa kuuvuruga mradi wa REA kwa ubadhirifu na rushwa.