Ujumbe kwa Tanesco: Mpango wa usambazaji umeme vijijini (REA) umekumbwa na ubadhirifu na rushwa

Walichotufanyia hao Rea hapa chalinze kitongoji cha mbala ni maajabu, ramani ya mradi inaonyesha kitongoji cha mbala umeme utasambazwa km 5,akaja mkandarasi akaanza kuweka alama sehemu nguzo zitapita, baadae wakaja na kuanza kuchimba mashimo cha kushangaza nguzo zikawekwa sehemu chache na kusema mradi umefupishwa, hadi Leo tumebaki na mashimo ya nguzo na waziri nasikia ameshazindua kwa hizo nguzo chache, kama vp mje kufukia mashimo yenu arobaini na moja mliyoacha
 
Ndugu mpendwa mteja wetu tunaomba utusaidie taarifa za kijiji husika na namba yako ya rmtaarifa tuangalie kipo kwenye awamu ipi ya utekelezaji wa miradi yetu
Mkuu hili kiujumla mjitathmini ninyi kama TANESCO ama zile kampuni mzozipa hii miradi. Mimi pia ni mhanga kwenye hili. Kijijini kwetu umeme wa REA ulifika kwa awamu mbili; awamu ya kwanza umeme ulikuwa kama vita, watu walikuwa na kiu kubwa na hivyo baadhi ya wafanyakazi wenu wasio waadilifu wakaona fursa; walipiga watu pesa hadi laki sita kwa mtu mmoja. Kutokana na hili, maeneo ambayo hayakuwa kwenye mpango yakapewa umeme na yaliyokuwa kwa mpango yakakosa umeme. Kuna mfano mmoja wa ajabu sana; kitongoji kimoja wananchi walikataa kutoa pesa na kama kuwakomoa eneo lao likarukwa umeme ukaenda kuanzia kitongoji cha mbeleni. Hadi leo hii hiki kitongoji hakikupata umeme ilihali walio mbele yao wana umeme. Eneo na jina la kijiji nakutumia pm
 
Tunaomba jina la kijiji, wilaya, angalau wateja kadhaa na namba zao za simu tuwasikilize
 
Hello Mkuu TANESCO
Mie na wananchi Wenzangu tupo 70 Tunahitaji Umeme.
Tupo Geita Mjini , Mtaa wa Mwatulole Secondary.
Ila ,ili umeme uweze kutufikia kunahitajika nguzo .
Sasa Tumeanza Kukaa vikao ili tuweze kuufikisha umeme .
Nyie Kama Tanesco mnatusaidiaje ,Ukizingatia jukumu la Kusambaza Umeme lipo Juu Yenu. na Hamjafanya hilo.

Naomba Maelekezo yako kwa Hatua Zaidi.
 
Unawezaje kujua tatizo ndani ya kitengo kikubwa? Unapaswa kutambua kuna sheria za kufata na kanuni.haki ya kisikilizwq pia ipo
Mmojawapo wa jamaa ni Kelvin Martin Ulio, kuna kipindi alifanya Kibaha Pwani, wakamtema coz hakuwa na vigezo vya elimu, sasa msikaji wake akamfanyia mpango Tabora Mjini
 
Tanesco kwanini mteja kumwekea umeme eneo la kusimika nguzo 1 tu nalo mpaka miezi 2?
 
Hello Mkuu TANESCO
Mie na wananchi Wenzangu tupo 70 Tunahitaji Umeme.
Tupo Geita Mjini , Mtaa wa Mwatulole Secondary.
Ila ,ili umeme uweze kutufikia kunahitajika nguzo .
Sasa Tumeanza Kukaa vikao ili tuweze kuufikisha umeme .
Nyie Kama Tanesco mnatusaidiaje ,Ukizingatia jukumu la Kusambaza Umeme lipo Juu Yenu. na Hamjafanya hilo.

Naomba Maelekezo yako kwa Hatua Zaidi.
Tunaomba namba yako.ya simu kwa mrejesho dhidi.ya ombi hili
 
Ninaomba kujua vigezo vya kufikiwa na REA katika kitongoji. Kuna uhusiano wowote wa idadi ya kaya na kupatiwa huduma ya nishati?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom