UJUMBE KWA SIMBA SPORTS CLUB

fexcash

JF-Expert Member
Jul 30, 2017
352
604
Simba sports club ndio kikosi bora cha mpira kwa sasa kwa upande wa mashariki ya Africa. Lakini mnatuhuzunisha kwakuwa huo ubora unaoongelewa bado hamjauthibitisha.

Ubora wa mpira unaonekana uwanjani ndani na dakika 90 hapo nazungumzia team work (muunganiko wa timu), mipango na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

Na pia nje ya uwanja yani uwezo wa coach, hekima ya viongozi na benchi la ufundi.

Tukianza na uwanjani kiukweli Simba mnahuzunisha sana yani kuna wachezaji unaweza kujiuliza wanafanya nini kwenye kikosi cha Simba, hamna kujituma na hata uwezo wa mchezaji mmoja mmoja bado hauna effect kwenye timu. Simba kuna tatzo la goalkeeper Aishi Manura ni tatizo, HD sijui wamekufanya nn vijana wa dar ulivyokuwa Moro ulikuwa unauwasha kwelikweli, Mzamiru sijui anasubiri nn Msimbaz na wengine baadhi. Kiukweli mnatuuzunisha.

Sasa tukiamia nje wa pitch yani naanza na coach kiukweli sometimes unaishiwa mbinu kila cku unatest mitambo muda wa kutest umeisha la sivyo utaonyeshwa mlango wa kutokea.
Tuamie kwenye viongozi hapa nimzungumzie Haji Manara kiukweli huju jamaa ni unprofessional, yani unachokifanya ni kama ulopokaji sifa unazoipa Simba hzo sifa hazipo, Yani mtu akikusikiliz anaweza kuhisi unaongelea Madrid au Barcelona.

Hebu jifunge kuongea uhalisia wa timu itasaidia kujua mnaitaji kujipanga wapi.

Benchi la ufundi halimsaidii coach kila siku mnafungwa kwanamna hyohyo ila bado hamjirekebishi.

Simba punguzeni maneno tunataka vitendo kwamaana vitendo vinaongea kuliko maneno.

ALAMSIKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahahaha! naona umenuna hadi umepotea jukwaa! heri (sisi) mkate mkavu kwenye amani(yanga)! tunakimbiza mwizi kimya kimya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom