Ujumbe kwa Rais, Waziri wa Mawasiliano, Waziri wa Ajira na Maendeleo ya Vijana

Charles nghwaya

New Member
Jun 11, 2017
3
3
Habari Team

Mheshimiwa Rais,Waziri Mkuu& waziri wa Mawasiliano/Waziri wa ajira&Maendeleo ya Vijana.

1.Sisi ni sehemu ya wajasiliamali tuliopata ajila zetu ambazo sio rasmi kwenye mitandao ya simu (Freelancer)

Tulikuwa tunaomba msaada wako/Wenu kutusaidia kurekebisha sheria mpya ya TCRA.

Tumeambia kuwa kuanzia Trh 01/05 mwaka huu haitaruhusiwa mawakala wa usajili yaani (Freelancer's) kusajili line kwa kutembea mitaani kama Machinga!

Inatakiwa kila msajili line akodi Frem ya Biashara akate leseni pia awe na TIN no pamoja na Kitambulisho cha NIDA.

Mfumo huu kwa mazingira ya nchi yetu hautakuwa rafiki kwa vijana wa kitanzania ambao wamepata ajila zao kupitia hii kazi,kwa vile wengi watashindwa kukodi milango na kukidhi vigezo vya kuwa wasajili kwa mfumo mpya.

Kwa kushindwa kwao inamaana hawatakuwa na ajila tena.

Lkn pili kwa kufungua milango ya biashara itafanya malipo yao yashuke sana kwa vile hawatapata wateja wa kutosha,Ikumbukwe kuwa kazi yetu hatulipwi mshahara bali tunalipwa Commission kwa kadri ya ufanyaji wa kz,hivyo kwa mfumo wa kutembea inatulipa zaidi kuliko kuwa (fixed) sehemu moja.

Nini mawazo yetu!

Kama lengo ni kulipa kodi tunaunga mkono Serikali yetu kwa vile kweli hii kazi inatupa kipato cha kutosha na hasa wengi wetu,Hatuwezi kuajirika katika soko la ajira kwa vile Elimu zetu ni za chini! Lakini tunashukuru sana makampuni ya simu yametupa ajira Vijana wa Kitanzania zaidi ya Elfu 50 kwa vigezo vya kujua kusoma na kuandika pia uwezo wa kuelezea bidhaa za makapuni kwa wateja wetu! Kwa hiyo tunaunga mkono kulipa kodi kwa vile tunapata kipato,Hivyo kulipa kodi sio shida hata kidogo tunatambua Serikali lazima ijiendeshe kwa sisi Raia kulipa kodi sitahiki.

Pendekezo letu tunaomba kwa vile Commission zetu tunalipwa kila mwz serikali iweke sheria kwa sisi ambao tupo kwenye mitandao ya simu na tunalipwa kwa Commission tukatwe kodi moja kwa moja tunapolipwa Commission zetu,Mfn kama sheria ikisema tulipe asilimia kumi ya Commission zetu kila mwezi tunaweza kulipa kodi kubwa sana kuliko tukifungua frem ambazo ni fixed!

Kwa taarifa tulizonazo Kampuni zote za simu wanalipa Commission zaidi ya Bilioni 6 kila mwezi kwa vijana hawa wanaosajili line kulingana na makubaliano na Makampuni yao.

Kwa vile waziri anaweza kuomba hata tu file za malipo kwenye makampuni ya simu akapiga hesabu ya kukata 10% ataona jinsi atakavyopata kodi kubwa kwa mwaka,na kodi ambayo hatasumbuka kuipata kwa vile atapata kupitia moja kwa moja kwa makapuni kama serikali inavyopata kodi za wafanyakazi wengine kupitia waajili wao.

Pendekezo lingine kama tatizo ni kupunguza uharifu serikali na makapuni ya simu wana wataalamu wazuri wa IT wanaweza kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti vijana wasisajili line na kuwauzia watu ambao ni waharifu tunaimaini kuwadhibiti watu wachache ambao sio waaminifu inawezekana kuliko kuua ajira za Mamilioni ya Vijana kwa sababu ya watu wachache.

Mfano, inaweza kuweka System mteja akisajili line moja apate taarifa kwenye namba anazomiliki mteja huyo kuwa amesajili line ya mtandao X,hivyo mteja atajua kuna line amesajili na Msajili hajampa,au Mteja akatumiwa Password kwenye line aliyonayo kwa hiyo ili line ya pili isajiliwe lazima mteja atoe password hizo kwa Msajili,au ulisajili line moja uwekwe mda wa hata masaa 10 au siku 2 ndipo system iweze kukubali kupitisha line nyingine ya huyo mteja.

Hii ni mfn tu ya njia za kudhibiti uharifu wa kusema rudia kuweka kidole System inasumbua.

Lakini pia tukumbuke pia hizi pesa Bilioni 6 ambazo Makampuni ya simu wanazolipa vijana wa Kitanzania kama Commission zinaingia kwenye Mzunguko wa Uchumi wetu kila mwezi,japo hata sasa Serikali haipati kodi ya moja kwa moja ila inapata kodi kupitia bidhaa wanazonunua vijana baada ya kulipwa,Lkn pia Mzigo wote wa hawa Vijana tukiwatoa kuanzia trh 01/05 Mwaka huu ni Ipi plan B ya Serikali itawasaidia?

Tunaomba Waziri wa kazi kwa kushirikiana na Waziri wa Mawasiliano mliangalie hili.


20210408_130402.jpg
 
Back
Top Bottom