Ujumbe kwa Rais Magufuli: Wananchi wa Natta Serengeti tumeporwa eneo ndani ya WMA ya Ikona


Gibiba

Gibiba

Senior Member
Joined
Jun 22, 2016
Messages
111
Likes
27
Points
45
Age
38
Gibiba

Gibiba

Senior Member
Joined Jun 22, 2016
111 27 45
Mh. Rais, kwa maskitiko makubwa sana napenda kuwasilisha lalamiko la wananchi wa natta wilayani Serengeti.

Mh. Rais,wananchi wa natta tunayo kero kubwa ya kuporwa eneo ndani ya WMA ya Ikona na badala yake kuvamiwa eneo lingine lililopangiwa matumizi ya malisho tangu mwaka 2003 kwa vikao halali.

Mh. Rais, tangu mwaka 2003 kijiji cha natta kilitengeneza rasmi mpago wa matumizi bora ya ardhi ya kujiji.

Aidha ardhi hiyo iligawanywa kwa shughuli za aina tatu kama ifuatavyo;
Upande wa kaskazin mwa kijiji palitengwa kwa shughuli za kilimo pamoja na msitu wa asili.

Kusini mwa kijiji palitengwa kwa malisho,makazi na akiba.

Upande wa mashariki palitengwa kwa uhifadhi(WMA).

Aidha mpango huo uliendelea kutumika na kuheshimika tangu 2003 kwa kuzingatia kila kipande na matumizi kiliotengewa.Upande wa kilimo ziliendelea shughuli za kilimo kama kawaida mpaka sasa.

Upande wa mashariki,shughuli za uhifadhi zimeendelea kama kawaida na wanachi wameendelea kujipatia fedha ya utalii kwa maendeleo bila bughudha yoyote.

Pia kipande cha malisho,makazi na akiba kimeendelea kutumuka vyema kama matumizi yake yalivyopangwa.

Bila mashaka yoyote yale,ardhi hii imeendelea kutumika kama ilivyopangwa bila upande mmoja kuathiri mwingine.

Lakini kwa mshangao na masikitiko makubwa,mnamo february 2016,imeletwa ramani ya wma tofauti na ya awali inayooneaha kutokuwemo kwetu kupitia eneo la awali na badala yake kuingizwa kwenye ramani eneo lililopangiwa malisho na akiba.

Mh.rais baada ya wananchi wako kupokea taarifa hiyo ilizua hali ya taharuki kwa kila mwananchi na mara moja utaratibu wa vikao na mikutano ya wanchi vilianza nia ikiwa ni kidai haki yao inayoelekea kuporwa na wachumiatumbo wachache.

Aidha kupitia mkutano wa wananchi kiliundwa kikosi kazi cha watu 7 nikiwamo mm kwa ajili ya ufuatiliaji wa nyaraka za wma zilizotutambua kwa eneo la awali.Licha ya ukweli uliyoendelea kuonekana tokana na majibu ya kikosi kazi hicho,bado tumeendelea kukwamishia haki yetu ambayo tunaona kama kuna vivuli vya viongozi wa wilaya na mkoa vinavyotukinga kwa kukwamisha ufanisi wa jambo hili kwa maslahi yao.

Ofisi ya mkuu wa wilaya tumeenda mara kadha lakini hakuna majawabu ya maana tumepata mpaka sasahivi.

Suala hili pia limefikishwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa tangu mwezi wa 3 mwaka huu na akaahidi kutupatia haki yetu ndani ya wiki moja mbele,lakini mpaka naandika ujumbe huu hakuna majawabu yoyote yamerejeshwa toka ofisini hapo.

Ukimyaa huu umeendelea kututia mashaka makubwa kulingana na unyeti wa suala na namna linafanyiwa urasimu na wasaidizi wako.

Samba na hilo mh.rais,katika ufuatiliaji uliofanywa na kikosi kazi hicho cha wananchi,yako mambo yalibainika ikiwa ni pamoja na kubaini sehemu ya watu waliopelekea kuporwa kwa ardhi hiyo.Ziko hatua walipaswa kuchukuliwa na wananchi lakini kwa kukumbatiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya,kwa maslahi yake alilikwamisha suala hili kuwezekana.

Mh.rais kwa hatua zote hizo tulizopitia bila mafanikio yoyote,wananchi sasa wanaandaa safari ya kufika kwako wakijua kwamba ndipo utakapopatikana msaada wa pekee.

Lakini kabla haijafikiwa hatua hiyo,
nimeshauriwa kama mjumbe wa kikosi kazi kukuandikia waraka huu kama utangulizi na taarifa kwamba kuna watu nyuma ya ujumbe huu watafika hapo ofisini kwako.

Mh.rais tunaomba msaada wako kama utafanikiwa kuusoma ujumbe huu tafadhali.Wananchi wako wanateseka,na ww ndio kimbilio lao.

Ahsante kwa kupokea!

HAPA KAZI TU!

Mawasiliano;0789014728.
 
Gibiba

Gibiba

Senior Member
Joined
Jun 22, 2016
Messages
111
Likes
27
Points
45
Age
38
Gibiba

Gibiba

Senior Member
Joined Jun 22, 2016
111 27 45
Moderator naomba tafadhali utumie kila namna ujumbe huu umfikie rais wa nchi.

Ni muhim sana.
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
22,868
Likes
26,895
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
22,868 26,895 280
Mbunge wenu ana hizi taarifa?
 

Forum statistics

Threads 1,236,111
Members 474,999
Posts 29,247,012