Ujumbe kwa Rais Kikwete:Waachieni wazee wa Pemba

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa inayoitwa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.

Muheshimiwa, wakati unafungua bunge kule Dodoma ,tarehe 30/12/2005,ulisema kwamba Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa katia ya Pemba na Unguja,na ukaahidi kuushughulikia. Japo kauli yako hii haikukidhi ukweli halisi wako waliokupa imani na kuwa na subra.Wakisubiri kile ulichokianzisha na kukiiita mazungumzo ya kutafuta suluhu la kudumu la huo ufa. Lakini kama kawaida ya CCM ilikua ni ule ule usanii wenu wa kupoteza muda kusubiri uchaguzi mwengine.

Katika kikao cha Halimashauri kuu ya CCM huko Butiama, wajumbe kutoka ZNZ walisamama na kutoa maneno ya kashafa dhidi ya Wapemba na kila alie CUF na kusema wazi hawako tayari kushirikiana nao, na wakafika hata kudai ASP yao ili wakawacharange mapanga, Wapemba, Waarabu na maCUF.

Muheshimiwa baada ya kikao hicho tulikusikia pale Diamond Jublee ukisema walichokifanya CCM wenzako hao ni kutumia haki yao ya KIDEMOKRASIA KUJIELEZA.

Wewe mwenyewe ,ulikua miongoni ya wabunge 55 (G55) kutoka Tanganyika mliopeleka hoja bungeni kudai serikali ya Tanganyika. Wachaga walishawahi kudai Ndani ya UN, kupitia aliekua chifu wao Marehemu chifu Mareale, kwamba wapewe serikali yao. Hata hivi karibuni, Kigoma wameshawahi kudai kujitenga kama hawatapewa haki zao za kiraia.

Hakuna hata mmoja katika hao hapo juu alidaswa au kuulizwa na kuambiwa kwamba ni haini. Tunavyojua vyama vilivyokuwepo Tanganyika na ZNZ kabla ya 1964 au mpaka 1977 vimepigwa marufuku katika sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992. Sasa hawa wanaodai ASP mbona wao hawaitwi mahaini?

Wapemba wananyimwa haki zao za msingi kama Wazanzibari, hayo yanafanywa na serikali zote mbili za CCM, chama ambacho wewe ni mwenyekiti, na wewe ndie rais waserikali kuu yaani hiyo ya Muungano. Kwa lugha fupi maovu wanayofanyiwa Wapemba wewe unayasimamia.

Sasa , katika hali kama hiyo, Wapemba kwa sababu kama destri ya wazanzibari ni watu waungwana na wastaarabu, wametumia njia ya kistaarabu kupeleka malalamiko na mawazo yao katika UN, ambayo Tanzania ni mwanachama na imesaini maazimio yote muhimu, au matangazo yote muhimu ya UN. Tena wamekwenda wazi wazi bila kujificha.

Muheshimiwa , hao wazee 12 ni wawakilishi tuu ya Wananchi wa Pemba, na katika waraka wao kuna sahihi za Wapemba 10,000, hawa pia ni kama wawakilishi ya wananchi wote wa Pemba.

Cha ajabu, kwa sababu tuu wao ni Wapemba , na kwasababu wameikataa CCM, ulikua kama walivyomumiani wa KiCCM kila anaekaaa lazima anyonye damu ya Wapemba, umeamua kuonyesha makucha yako, umetuma makomandoo, majeshi ya kitanganyika , usiku wa manane na masilaha makubwa, kwenda kuwakamata na kuwadhalilisha wazee wetu, wazee wasio kuwa na hata na kisu cha ukindu, iweje watekwe nyara usiku wa manane na makomandoo 40.

Sasa mmewachukua, mmewapeleka kusikojulikana, hakuna anaejua wapi wapo, lengo ni kuwadhalilisha kwa sababu tuu ni Wapemba.

Kama ni mahaini kama mnavyosema, kwanini wasiwe mikononi mwa polisi, kwa nini sasa ni wiki, hamjawafikisha mahakamani ,na kuwapa haki zao zote za msingi kama binaadam mwengine. Kwanini wawe katika mikono ya majeshi katika makambi yao, kwa sheria gani mnayoitumia?

Muheshimiwa jaaliwa ingekua ni wazee wako wewe wanaofanyiwa haya ungejisikia vipi, au kwasababu wao ni Wapemba walioikataa CCM? Juzijuzi tuliona mama Kikwete na baadae Serikali ilivyoingilia kati harakaharaka sakata la mahujaji, baada ya ndege yao kuchelewa kuondoka Dar. Kwa nini? Kwa sababu ya uchungu wa wazee.

Tunachokueleza muheshimiwa Kikwete ni kwamba mnachokifanya ni kuwadhalilisha na kuwatesa wazee wetu pasi na kosa lolote, mnawatesa kiakili wao na familia zao na Wapemba wenzao na wapenda haki na amani wote, kwa sababu wao hawajui wako wapi na familia zao ziko vipi, na familia zao hazijui wako wapi na wako vipi.

Kwa sababu sasa matunda ya uovu mlioupanda kwa miaka 40 unaaza kutoa matunda, mnajaribu kupoteza malengo kwa kuwakama na kuwadhalilisha wazee wetu.

Nadhani huzijui hasira na ghadhabu zetu, muheshimiwa hii sio 1964 kama mliwakama wazee na ndugu za watu na jamaa zao wakakaa kimya na watu hao kupotea. Hii ni 2008. Ujue kwamba dhamana ya wazee wetu hao iko mikononi mwako, na wewe ndie tunaekujua, madhara yoyote yatakayo wapata kwa kitendo mnachokifanya sisi tunakujua wewe. Maradhi yoyote yatakayowapata sasa au baadae kwasabau ya udhalilisho mnaowafanyia jukumu liko juu yako wewe.

Tafadhali waachie wazee wetu warudi wakakae na familia zao,na kujishughulikia na maradhi tofauti yanayowasumbua.

Msimamo ni ule ule kama mmeshindwa kuwatendea haki Wapemba katika nchi yao, basi muwe ni wenye kukubali mawazo yao kama nyinyi mlivyo na haki ya kutoa mawazo yenu.

Madai hayo ni ya Wapemba wote, wala kuwakamata na kuwadhalilisha wazee wetu hao haitobadilisha msimamo wetu, tunachodai ni haki yetu. Mapambano yanaendela. Kama nyinyi hamko tayari kutupa haki zetu iweje kukerwe na sisi kutaka chetu.

Tafadhali warudisheni wazee wetu katika familia zao, msikitie kidonda msumari wa moto, chumvi iliyotiwa inatosha. Tafadhalini Tafadhalini.
 
Last edited by a moderator:
Hivi wanao mshauri ndugu Rais JK ni akina nani ? JK huwa anapata muda wa kukaa mwenyewe na kuangalia hali halisi na hasa mambo ya Zanzibar ? Je wale wanao shitakiwa kwa uhaini walikamatwa kabla hajaambiwa ama baada ya kuambiwa ? Je andhani kwa kuwakamata ndiyo CCM inaweza kupata ushindi ama kukubalika Pemba ?Utawala bora ndiyo huu ?je uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa Katiba ni upi ?Kwa mujibu wa mwandishi wakati JK naG55 wanayafanya haya mbona hawakutiwa nguvuni na kuambiwa wahaini ?
 
Wewe mwenyewe ,ulikua miongoni ya wabunge 55 (G55) kutoka Tanganyika mliopeleka hoja bungeni kudai serikali ya Tanganyika. Wachaga walishawahi kudai Ndani ya UN, kupitia aliekua chifu wao Marehemu chifu Mareale, kwamba wapewe serikali yao. Hata hivi karibuni, Kigoma wameshawahi kudai kujitenga kama hawatapewa haki zao za kiraia.
Mzee wa Shughuli, the message delivered successful!!

Narudia kukazia "HAYA NI MAWAZO YA WAPEMBA", haijalishi idadi yao lakini ujumbe lazima ufike panapohusika!! Siku zote dhurma uchangia watu kuenenda tofauti na matakwa ya wadhurumaji. Tatizo kubwa ni hicho kisiki kinachokariri kuwa Babake alikuwa mwanamapinduzi ilhali alikuwa mwoga ka' MBWA KOKO!!
 
Basi JK watu wanakuacha upambane na historia .Kumbe una chuki dhidi ya watu wa Pemba tangia zamani ? Mbona leo umekuwa Rais unawalazimisha wabakie katika Muungano wakati ulidai Tanganyika ?
 
Wahaini wapo wengi sana na hata huyo kisura mwenyewe ni muhani
wakati alipo jiingiza katika lile kundi la tanganyika alikuwa anataka nini?au sifa tu
 
Kikwete was a bogus personality then, and even now. He made a heap of bogus promises to get the presidency, and thanks to our ignorant population, he made it. I would not blame Col Kikwete for being our president but rather our own population for making him our president. I guess he will not get away with it next time.
 
Siamini kama kweli Serikal inaweza kuendesha kesi hii kama ya uhaini.Nadhani wanapaswa kuwa more smarter than that .Wakae wawasikilize na si kufanya haya mambo ya ajabu .CUF bado wako kimya nadhani wanatafuta namna .Wacha tuone , lakini siamini kama JK anaweza kudhani majeshi yanaweza kuzima mawazo ya watu .
 
JK ni mtu mwenye mawazo yaliyo hai, na siyo hivyo tu bado anatafuta njia iliyobora kuyatatua haya ya zenji, mtakumbuka jamaa amakumbwa na mabaraa mengi wakuu, naona tumuuombee atufikishe salama.
 
Mimi nafikiri hawatakuwa na kesi wanawatisha tu kwa maana wana haki ya kueleza mawazo yao, isitoshe UN haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania kwaiyo sio authority ya kibabaikia bali wamefikisha message kuwa pemba kuna mgogoro mkubwa hata CCM wakikaa kimya.
 
JK aliingia kwa NGUVU.KASI NA ARI kaishiwa vyote?sasa anakuja na kipi?maana ukiwa na la kwako ukashindwa basi waweza kuwa mbabe kama Mkapa aliingia akiwa mr.clean alipofisadi akawa mbabe........
 
Kikwete was a bogus personality then, and even now. He made a heap of bogus promises to get the presidency, and thanks to our ignorant population, he made it. I would not blame Col Kikwete for being our president but rather our own population for making him our president. I guess he will not get away with it next time.

Kichuguu I like it. Mimi wala sioni sababu ya kuendelea kumlaumu Muungwana. acha yatokee yanayotokea hadi hapo akili zetu zitakapoamka. acha tuendelee kuteseka na kuumia kwa ajili ya ujinga wetu.. who cares!!!! Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari kuna shule ya msingi kule kigoma wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tano wanakaa chini na kuandikia chini.. What the hell is that.. Still tuna viongozi wanatembelea magari ya milioni 120 mtu mmoja.. UUUUwiiiii nina uchungu lakini sioni kama wale waliopewa madaraka ya kuiongoza nchi hii wana uchungu.. Why , Kwa nini? Pesa tulizowalipa Majambazi wetu wa Richmond zingejenga shule ngapi za kisasa? Pesa za EPA zingejenga sekondari ngapi?

Mimi nimesema hivi, acha tuendelee kunyongwa kwa ujinga wetu.. Siku itafika (Miaka 50 ijayo, I will not be alive) wadanganyika watakuwa wameamka. watakuwa hawapo tayari kudanganywa na kilo moja ya sukari na kanga wapige kura.. hawatakuwa tayari kuwatandikia zulia jekundi mafisadi.. hawatakuwa tayari kula nyama za ng'ombe wanazopewa na mafisadi.

Acha waendelee kuiba.. na mimi nikipata pa kuiba ntaiba kwani watanifanya nini?
 
Hivi jamani kama nchi tunaelekea wapi mbona mimi sielewi? Kwa mawazo yangu naona kuna nafasi moja ambayo katiba ya nchi imemfanya mungu inapwaya kweli kweli. What do we do so tunaacha tuendelee kuaibika hivi hivi tu? Lakini hili liwe somo kwa watz wote kwamba si kila mtu anaweza kuwa rais simply kwa sababu ana sura nzuri. Urais ni kitu kingine jamani ukikosa mtu makini hata vining'ina vyetu vitalipa hii gharama ndugu zangu.
 
JK ni mtu mwenye mawazo yaliyo hai, na siyo hivyo tu bado anatafuta njia iliyobora kuyatatua haya ya zenji, mtakumbuka jamaa amakumbwa na mabaraa mengi wakuu, naona tumuuombee atufikishe salama.

tatizo ni kuwa atachukua muda gani 'kutafuta' njia ya kumaliza matatizo. Mimi nilidhani wakati alipokuwa anagombea, tayari alikuwa na vision ya nini anataka kukifanya kwa ajili ya nchi yake. Kumbe inavyoonekana aliutafuta urais na baada ya kuupata akaanza kazi upya ya kutafuta suluhisho kwa ajili ya matatizo. kama ndivyo hivyo, kazi tunayo
 
JK aliingia kwa NGUVU.KASI NA ARI kaishiwa vyote?sasa anakuja na kipi?maana ukiwa na la kwako ukashindwa basi waweza kuwa mbabe kama Mkapa aliingia akiwa mr.clean alipofisadi akawa mbabe........

Kuna kila dalili na ni > 100% kwa JK kuwa mbabe ndani ya awamu ya pili na atakapostaafu, BWM atakuwa cha mtoto!!! Hebu tujiulize kwanini kadiri siku zinavyokwenda anazidi kujiimarisha upande wa mafisadi tena kwa kiburi cha waziwazi? si chama chake wala serikali yake imeweza kuongelea wazi kwa wananchi ufisadi uliotokea tanzania, Why? Why? there must be very offensive motive malicious behind this silence,huyu sasa hivi anatengeneza kwanza strong capsule atakayoitumia baadaye kama vile yeye sasa anavyotumiwa na BWM, Angalieni uteuzi wake wa mabosi juu jinsi ulivyo,then kila kwenye chaguzi za chama ana upande/chaguo zake
Rais yuko busy na safari za nje kila siku hata muda wa kuugua hana wakati hatuoni maisha bora na tunazidi kuporomoka, huku taratibu za tenda serikalini zinapindishwa bila aibu, hapo baadaye tutegemee nini zaidi ya ubabe baada ya ushindi wa kishindo kwa pesa yetu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom