Ujumbe kwa Rais Kikwete:Waachieni wazee wa Pemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe kwa Rais Kikwete:Waachieni wazee wa Pemba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, May 16, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa inayoitwa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Muheshimiwa, wakati unafungua bunge kule Dodoma ,tarehe 30/12/2005,ulisema kwamba Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa katia ya Pemba na Unguja,na ukaahidi kuushughulikia. Japo kauli yako hii haikukidhi ukweli halisi wako waliokupa imani na kuwa na subra.Wakisubiri kile ulichokianzisha na kukiiita mazungumzo ya kutafuta suluhu la kudumu la huo ufa. Lakini kama kawaida ya CCM ilikua ni ule ule usanii wenu wa kupoteza muda kusubiri uchaguzi mwengine.

  Katika kikao cha Halimashauri kuu ya CCM huko Butiama, wajumbe kutoka ZNZ walisamama na kutoa maneno ya kashafa dhidi ya Wapemba na kila alie CUF na kusema wazi hawako tayari kushirikiana nao, na wakafika hata kudai ASP yao ili wakawacharange mapanga, Wapemba, Waarabu na maCUF.

  Muheshimiwa baada ya kikao hicho tulikusikia pale Diamond Jublee ukisema walichokifanya CCM wenzako hao ni kutumia haki yao ya KIDEMOKRASIA KUJIELEZA.

  Wewe mwenyewe ,ulikua miongoni ya wabunge 55 (G55) kutoka Tanganyika mliopeleka hoja bungeni kudai serikali ya Tanganyika. Wachaga walishawahi kudai Ndani ya UN, kupitia aliekua chifu wao Marehemu chifu Mareale, kwamba wapewe serikali yao. Hata hivi karibuni, Kigoma wameshawahi kudai kujitenga kama hawatapewa haki zao za kiraia.

  Hakuna hata mmoja katika hao hapo juu alidaswa au kuulizwa na kuambiwa kwamba ni haini. Tunavyojua vyama vilivyokuwepo Tanganyika na ZNZ kabla ya 1964 au mpaka 1977 vimepigwa marufuku katika sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992. Sasa hawa wanaodai ASP mbona wao hawaitwi mahaini?

  Wapemba wananyimwa haki zao za msingi kama Wazanzibari, hayo yanafanywa na serikali zote mbili za CCM, chama ambacho wewe ni mwenyekiti, na wewe ndie rais waserikali kuu yaani hiyo ya Muungano. Kwa lugha fupi maovu wanayofanyiwa Wapemba wewe unayasimamia.

  Sasa , katika hali kama hiyo, Wapemba kwa sababu kama destri ya wazanzibari ni watu waungwana na wastaarabu, wametumia njia ya kistaarabu kupeleka malalamiko na mawazo yao katika UN, ambayo Tanzania ni mwanachama na imesaini maazimio yote muhimu, au matangazo yote muhimu ya UN. Tena wamekwenda wazi wazi bila kujificha.

  Muheshimiwa , hao wazee 12 ni wawakilishi tuu ya Wananchi wa Pemba, na katika waraka wao kuna sahihi za Wapemba 10,000, hawa pia ni kama wawakilishi ya wananchi wote wa Pemba.

  Cha ajabu, kwa sababu tuu wao ni Wapemba , na kwasababu wameikataa CCM, ulikua kama walivyomumiani wa KiCCM kila anaekaaa lazima anyonye damu ya Wapemba, umeamua kuonyesha makucha yako, umetuma makomandoo, majeshi ya kitanganyika , usiku wa manane na masilaha makubwa, kwenda kuwakamata na kuwadhalilisha wazee wetu, wazee wasio kuwa na hata na kisu cha ukindu, iweje watekwe nyara usiku wa manane na makomandoo 40.

  Sasa mmewachukua, mmewapeleka kusikojulikana, hakuna anaejua wapi wapo, lengo ni kuwadhalilisha kwa sababu tuu ni Wapemba.

  Kama ni mahaini kama mnavyosema, kwanini wasiwe mikononi mwa polisi, kwa nini sasa ni wiki, hamjawafikisha mahakamani ,na kuwapa haki zao zote za msingi kama binaadam mwengine. Kwanini wawe katika mikono ya majeshi katika makambi yao, kwa sheria gani mnayoitumia?

  Muheshimiwa jaaliwa ingekua ni wazee wako wewe wanaofanyiwa haya ungejisikia vipi, au kwasababu wao ni Wapemba walioikataa CCM? Juzijuzi tuliona mama Kikwete na baadae Serikali ilivyoingilia kati harakaharaka sakata la mahujaji, baada ya ndege yao kuchelewa kuondoka Dar. Kwa nini? Kwa sababu ya uchungu wa wazee.

  Tunachokueleza muheshimiwa Kikwete ni kwamba mnachokifanya ni kuwadhalilisha na kuwatesa wazee wetu pasi na kosa lolote, mnawatesa kiakili wao na familia zao na Wapemba wenzao na wapenda haki na amani wote, kwa sababu wao hawajui wako wapi na familia zao ziko vipi, na familia zao hazijui wako wapi na wako vipi.

  Kwa sababu sasa matunda ya uovu mlioupanda kwa miaka 40 unaaza kutoa matunda, mnajaribu kupoteza malengo kwa kuwakama na kuwadhalilisha wazee wetu.

  Nadhani huzijui hasira na ghadhabu zetu, muheshimiwa hii sio 1964 kama mliwakama wazee na ndugu za watu na jamaa zao wakakaa kimya na watu hao kupotea. Hii ni 2008. Ujue kwamba dhamana ya wazee wetu hao iko mikononi mwako, na wewe ndie tunaekujua, madhara yoyote yatakayo wapata kwa kitendo mnachokifanya sisi tunakujua wewe. Maradhi yoyote yatakayowapata sasa au baadae kwasabau ya udhalilisho mnaowafanyia jukumu liko juu yako wewe.

  Tafadhali waachie wazee wetu warudi wakakae na familia zao,na kujishughulikia na maradhi tofauti yanayowasumbua.

  Msimamo ni ule ule kama mmeshindwa kuwatendea haki Wapemba katika nchi yao, basi muwe ni wenye kukubali mawazo yao kama nyinyi mlivyo na haki ya kutoa mawazo yenu.

  Madai hayo ni ya Wapemba wote, wala kuwakamata na kuwadhalilisha wazee wetu hao haitobadilisha msimamo wetu, tunachodai ni haki yetu. Mapambano yanaendela. Kama nyinyi hamko tayari kutupa haki zetu iweje kukerwe na sisi kutaka chetu.

  Tafadhali warudisheni wazee wetu katika familia zao, msikitie kidonda msumari wa moto, chumvi iliyotiwa inatosha. Tafadhalini Tafadhalini.
   
  Last edited by a moderator: Mar 31, 2009
 2. N

  Nakandamiza Kibara Senior Member

  #2
  May 16, 2008
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi wanao mshauri ndugu Rais JK ni akina nani ? JK huwa anapata muda wa kukaa mwenyewe na kuangalia hali halisi na hasa mambo ya Zanzibar ? Je wale wanao shitakiwa kwa uhaini walikamatwa kabla hajaambiwa ama baada ya kuambiwa ? Je andhani kwa kuwakamata ndiyo CCM inaweza kupata ushindi ama kukubalika Pemba ?Utawala bora ndiyo huu ?je uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa Katiba ni upi ?Kwa mujibu wa mwandishi wakati JK naG55 wanayafanya haya mbona hawakutiwa nguvuni na kuambiwa wahaini ?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  This ze massage to you ..............Bob Marley.
   
 4. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2008
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mzee wa Shughuli, the message delivered successful!!

  Narudia kukazia "HAYA NI MAWAZO YA WAPEMBA", haijalishi idadi yao lakini ujumbe lazima ufike panapohusika!! Siku zote dhurma uchangia watu kuenenda tofauti na matakwa ya wadhurumaji. Tatizo kubwa ni hicho kisiki kinachokariri kuwa Babake alikuwa mwanamapinduzi ilhali alikuwa mwoga ka' MBWA KOKO!!
   
 5. N

  Nakandamiza Kibara Senior Member

  #5
  May 16, 2008
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Basi JK watu wanakuacha upambane na historia .Kumbe una chuki dhidi ya watu wa Pemba tangia zamani ? Mbona leo umekuwa Rais unawalazimisha wabakie katika Muungano wakati ulidai Tanganyika ?
   
 6. t

  think BIG JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Makamba, Pius Msekwa, Kingunge, ...

  Wahaini si hao 12 tu, ni wale wote 10,000 waliosaini ile barua. sasa hapo tuone hiyo kesi itakuwaje!
   
 7. M

  Mkuu Senior Member

  #7
  May 17, 2008
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wahaini wapo wengi sana na hata huyo kisura mwenyewe ni muhani
  wakati alipo jiingiza katika lile kundi la tanganyika alikuwa anataka nini?au sifa tu
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  May 17, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kikwete was a bogus personality then, and even now. He made a heap of bogus promises to get the presidency, and thanks to our ignorant population, he made it. I would not blame Col Kikwete for being our president but rather our own population for making him our president. I guess he will not get away with it next time.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  JK siku hizi anaitwa ZE COMEDY
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Siamini kama kweli Serikal inaweza kuendesha kesi hii kama ya uhaini.Nadhani wanapaswa kuwa more smarter than that .Wakae wawasikilize na si kufanya haya mambo ya ajabu .CUF bado wako kimya nadhani wanatafuta namna .Wacha tuone , lakini siamini kama JK anaweza kudhani majeshi yanaweza kuzima mawazo ya watu .
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  we game theory taratibu mkuu, rais wa nchi huyo
   
 12. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  JK ni mtu mwenye mawazo yaliyo hai, na siyo hivyo tu bado anatafuta njia iliyobora kuyatatua haya ya zenji, mtakumbuka jamaa amakumbwa na mabaraa mengi wakuu, naona tumuuombee atufikishe salama.
   
 13. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwani rais wa nchi ndo nini bwana yeye ni raia kama wengine bwana, kama anastaili kupewa Sifa hiyo kama wengine kwa mambo yake ni sawa tu!

  Wewe kwa upeo wako unaona hiyo a.ka haimfai JK? Chukua maigizo wanayofanya akina Mpoki na Joti, then chukua ahadi na mambo anayoyafanya JK angalia kama haviko sawa??

  Mimi nadhani hii ni matunda ya mambo na matendo yake juu ya nchi yetu ya Tanzania, kama watu wameamua kumuita hivyo poa tu, jina na likue liwe laivu, mbona mwinyi alikuwa anaitwa mzee wa Ruksa, mkapa akaitwa Mr clean wakati Fisadi mkubwa, basi wacha nae ajiunge na akina Joti
   
 14. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mawazo gani hayo unayoyazungumzia wewe, na kama alikumbwa na mabalaa kibao kayatatua kweli au ndio anatuongezea matatizo juu ya shida zetu

  Kumbuka Ukame, umeleta matatizo chungu nzima sasa hivi nchini kwetu jee hapa alitatua au kaongeza matatizo?

  Haya mambo kibao yanayoendelea sasa hivi, tunaibuiwa kila kukicha then anakaa kimya ndio anasubiri kutatua au?

  Leo ni mwezi wa tano mana yake tumebakiza miaka miwili na nusu kabla ya uchaguzi, je Kuna mtu anaweza kueleza hapa bayana kuwa JK mpaka sasa kafanya kitu gani kwa Watanzania ndani ya huu muda wake?
   
 15. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri hawatakuwa na kesi wanawatisha tu kwa maana wana haki ya kueleza mawazo yao, isitoshe UN haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania kwaiyo sio authority ya kibabaikia bali wamefikisha message kuwa pemba kuna mgogoro mkubwa hata CCM wakikaa kimya.
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  JK aliingia kwa NGUVU.KASI NA ARI kaishiwa vyote?sasa anakuja na kipi?maana ukiwa na la kwako ukashindwa basi waweza kuwa mbabe kama Mkapa aliingia akiwa mr.clean alipofisadi akawa mbabe........
   
 17. M

  Msesewe Senior Member

  #17
  May 17, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichuguu I like it. Mimi wala sioni sababu ya kuendelea kumlaumu Muungwana. acha yatokee yanayotokea hadi hapo akili zetu zitakapoamka. acha tuendelee kuteseka na kuumia kwa ajili ya ujinga wetu.. who cares!!!! Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari kuna shule ya msingi kule kigoma wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tano wanakaa chini na kuandikia chini.. What the hell is that.. Still tuna viongozi wanatembelea magari ya milioni 120 mtu mmoja.. UUUUwiiiii nina uchungu lakini sioni kama wale waliopewa madaraka ya kuiongoza nchi hii wana uchungu.. Why , Kwa nini? Pesa tulizowalipa Majambazi wetu wa Richmond zingejenga shule ngapi za kisasa? Pesa za EPA zingejenga sekondari ngapi?

  Mimi nimesema hivi, acha tuendelee kunyongwa kwa ujinga wetu.. Siku itafika (Miaka 50 ijayo, I will not be alive) wadanganyika watakuwa wameamka. watakuwa hawapo tayari kudanganywa na kilo moja ya sukari na kanga wapige kura.. hawatakuwa tayari kuwatandikia zulia jekundi mafisadi.. hawatakuwa tayari kula nyama za ng'ombe wanazopewa na mafisadi.

  Acha waendelee kuiba.. na mimi nikipata pa kuiba ntaiba kwani watanifanya nini?
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Very interesting !
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Kali hii
  meseji delivered
   
 20. B

  Bobby JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hivi jamani kama nchi tunaelekea wapi mbona mimi sielewi? Kwa mawazo yangu naona kuna nafasi moja ambayo katiba ya nchi imemfanya mungu inapwaya kweli kweli. What do we do so tunaacha tuendelee kuaibika hivi hivi tu? Lakini hili liwe somo kwa watz wote kwamba si kila mtu anaweza kuwa rais simply kwa sababu ana sura nzuri. Urais ni kitu kingine jamani ukikosa mtu makini hata vining'ina vyetu vitalipa hii gharama ndugu zangu.
   
Loading...