maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,144
Kwanza nichukue fursa hii kuipongeza serikali yetu chini ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli ambae anapambana usiku na mchana kuhakikisha nchi inasonga kwa kasi usiku na mchana. Pili niwapongeze baadhi ya watendaji wake akiwemo waziri wa Elimu Prof Ndalichako kwa kuendana na kasi ya Rais wetu.
Ila pamoja na juhudi zao hizi bado kuna baadhi ya watendaji hawafanyi inavyotakikana kitu kinachoweza kutafsiriwa kama hujuma kwa juhudi za Rais wetu.
Mfano mdogo ni hiki kinachoendelea sasahivi cha walimu wa part time kusumbuliwa malipo yao kwa miezi 6 na hata mwaka mzima kuhangaikia malipo huku wakitakiwa kuwa wanaendelea kufundisha kishingo upande wakiwa na njaa na hata kukosa nauli wakati mwingine.
Hivi usawa huu nani anaweza kukaa miezi 6 au mwaka bila kulipwa na aka-survive? Maana hata hapa ninapoandika leo mwezi June walimu wa part time wanadai malipo yao ya January na kila siku hawatulii ni kufuatilia tu badala ya kufundisha.
Naamini hata Prof Ndomba mwenyewe hana ubavu huo wa kufanya kazi bila kulipwa huku akitakiwa aingie darasani kufundisha kwa miez 6.
Na hata akiingia kufundisha hatofundisha kwa moyo wala kwa kujituma..na hiki ndicho kinachotokea kwa walimu wa part time badala ya kufundisha muda mwingi wanalazimika kufuatilia malipo na hata wakati mwingine kukosa nauli ya kufika chuo kufundisha.
Wanaoathirika ni wanafunzi na huku ni kurudisha nyuma juhudi za serikali ya awamu ya 5 na mbaya zaidi hiki ni chuo cha serikali ambako uzembe huu hautakiwa kuwa unajirudiarudia.
Kwa ujumbe huu naomba mkuu wa chuo kwa usikivu wake afanye hima kuhakikisha tatizo hili linalozorotesha elimu yetu halifumbiwi macho maana wanafunzi wanalipa ada na wanastahili elimu bora sio bora elimu kama kinachotokea sasahivi walimu kukosa hata nauli za kwenda chuo.
Na mwisho nimuombe waziri wetu mchapakazi kuangalia kwa ukaribu na kusaidia utendaji wa taasisi hii muhimu ya elimu kwakuwa inajikita kutoa zaidi elimu ya sayansi na teknolojia hakutakiwi kuwe na ubabaishaji wa aina yoyote ambao utazorotesha utoaji wa elimu bora, maana inaonesha watendaji wake hawatambui umuhimu wa kuweka mbele maslahi ya wadau hivyo kufanya matatizo kuwa yanajirudiarudia.
Nawasilisha