Ujumbe kwa mabinti ambao hawajaolewa kuhusu wanaume wakatili kwenye ndoa

NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
917
1,198
1. Usiogope kuolewa kwa hofu kwamba utauwawa au kupewa ulemavu na mumeo kwenye ndoa!

Tangu mwaka umeanza umeanza au ndani ya miaka 10 iliyopita ni ndoa ngapi unazifahamu au za watu maarufu ambazo umesikia mke kauwawa na mumewe?

Shetani anakuza ubaya wa mmoja ili kuwakatisha tamaa muone ndoa na waume wazuri waliochongwa na mungu na maadili mazuri wameisha!

Binti yangu, usinunue huo uongo!

Shetani anakuandaa kisaikolojia kuwa na talaka kesho kwa kisingizio cha domestic violence!

Bado tupo wanaume ambao wake zetu wanaweza kututolea ushahidi ya kwamba hata kutupiana maneno makali haijawahi kujitokeza, tunaheshimu, tunajali, tunashuka na kuyamaliza kwa upendo na unyenyekevu yale yanayojitokeza kati yetu na wao kwa msaada wa Mungu.

Muhimu: Wanaume wasiopiga, wasioua wako wengi mno kuliko wanaotishia uhai wako, kaa na mungu vizuri, usiwe na haraka ya ndoa, wala usipuuzie dalili mbaya kwenye uchumba na mahusiano zinazoonesha kwamba huyo mtu ni mtata au hana hofu ya kweli ya mungu!

Wewe kaa vizuri na Mungu.

Jiheshimu na kujitunza

Ukifika muda wa kuamua kuolewa angalia vyote kiroho chake, adabu yake, utu wake na uwezo wake kutatua changamoto na migogoro kwa upendo na utu!

2. Hakuna mwanaume ambaye ataficha makucha ukijipa muda, ukiomba mungu na usipopumbazwa na mnachokiita penzi ni upofu!

Ukifuatwa na kijana au mwanaume kwa ajili ya kutaka mahusiano na wewe ya kuelekea ndoa, cha kwanza kabisa, usimuoneshe kwamba una kiu, njaa ya kuolewa!

Mpe muda mrefu wa kukaa na kumjua kama rafiki! Usiogope ukisema bahati haiji mara mbili! Ndoa ni ya milele, kwa duniani ni mpaka kifo kiwatenganishe hasa kama ni ya kikristo! Hivyo huwezi kufanya uamuzi wa kukurupuka kwa kitu ambacho maisha yako yaliyobaki duniani utaishi nacho, usiwe mjinga, fungua macho! Alikataa muda wa kutosha, kama ana haraka muache aende! Wanaume wa kweli wako kama simba, hulipa gharama kupata wanachokipenda/ kukitaka!

Mbili, hakikisha mahusiano yake na Mungu, wazazi, jamii, na kila eneo hayatii shaka! Yote haya kuyaona, kuyajua haiwezi kuwa ndani ya miezi mitatu ya uchumba, jipe muda acha kiherehere.

Pata muda kumuomba mungu, na kusikiliza moyo wako vizuri kabla ya kusema "i do" maana itakugharimu maisha yako yote yaliyobaki chini ya jua!

Usifungue moyo "kipuuzi" na kudai "you are in love" na mtu ambaye bado unahitaji kumjua!

Unaruhusiwa "kufurahishwa" au "kuvutiwa" au "kupenda ukarimu wake" lakini "kupenda kule kwa kumuingiza moyoni" ni hatua ya mwisho baada ya kujiridhisha kila kitu ni salama na heri!

Ukipuuza haya, nitakuja msibani kwako na wewe, au mahakamani kwenye kesi yako ya kubondwa na mmeo!

3. Kijana asiye na ibada ya kweli kama tabia, asiyemuogopa mungu kama hakimu wake sasa na siku ile ya hukumu, asiyesikiliza au kutii sauti ya mtumishi mwaminifu wa mungu, huyu kesho atakupiga na hata kukuua, hana kitu cha mungu ndani yake!

Mara nyingi mabinti mnaangalia ni mkristo mwenzangu? Halafu mnasema haya ya madhehebu si tatizo, wote tuna yesu yuleyule... Kama mna yesu yuleyule kwanini haupo anakoabudu au wewe kuwa anakoabudu? Mbona unavutia kwako na yeye anavutia kwao? Usidanganyike, imani isipokuwa moja, huko ndani kutawaka moto mwingi mno, na hamna namna ya kuuzima maana kila mmoja anaamini la kwake!

Kama ni kijana kakufuata, lakini hana mahusiano binafsi na mungu yanayolenga kumjenga, kutunza moto wa mungu, na kumpa hatua kila siku na kila wiki, hapo umeshapigwa na kitu kizito tayari!

Hakikisha ana ratiba inayoeleweka ya usomaji neno, ratiba ya kueleweka ya kuomba, ratiba ya kueleweka ya kufunga kila wiki mara kadhaa walau masaa 12 kutwa, ratiba ya usomaji vitabu na kutazama video za watumishi wa kweli wa mungu na kubwa kuliko yote uaminifu wake kwenye mahudhurio ya ibada chini ya mtumishi mwaminifu wa mungu, tena hapa akuoneshe notebook yake ya kuandikia masomo na ikiwezekana muulize maswali kwenye kila alichoandika na kujifunza kuona anazingatia?

Zile simu mnazopigiana masaa mengi wakati wa mahusiano zinapaswa kugusia haya sana na sio umenipendea nini?

Hakikisha ana rekodi nzuri kwenye nyumba ya mungu, anatumika kwa uaminifu, analeta watu kwa yesu kwa kuhubiri/ kushuhudia au kutoa sadaka za injili kwa uaminifu, mwaminifu kwenye zaka na mambo ya kujenga ufalme wa mungu, hii ni kwa sababu hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo utakapokuwa, asiyewekeza muda, pesa na nguvu zake kwa mungu, moyo wake haupo mikononi mwa mungu, hata kukuua anaweza!

Haya yaangalie sana binti kuliko u-handsome wake, pesa yake, kazi nzuri au mafanikio kwenye vitu vinavyoweza kuisha! Hakikisha ni tajiri wa roho yake sana, moyo wake umeuzwa kwa mungu, mengine yatajipa tu!

Mwisho lakini si kwa umuhimu

Hakikisha ana baba wa kiroho

Mtu mwenye mamlaka juu yake anayeliheshimu neno na kuheshimu ndoa!

Baba wa kiroho asiyeheshimu neno, asiyeheshimu ndoa, atakuwa na watoto wa kiume washenzi kama yeye, hata kama itachukua muda watapatwa na kile alichonacho baba yao anayewawekea mikono!

Ukiamua kuzingatia hongera.

Ukipuuza tutakutana miaka michache ijayo ukiwa na majuto!


Pastor Dickson Cornel Kabigumila,

ABC Global,

0655466675
 
KWANINI UOE/LEWE

Kijana usioe
Ndoa ni Utapeli
Ndoa ni ubinafs
Kataa ndoa
 
Jf bhana,
Yaani Pastor anatumia I'd feki,
Kisha mwisho wa Uzi anataja jina lake halisi pamoja na Namba yake ya Simu
 
Back
Top Bottom