Ujumbe huu unawahusu CHADEMA: Wekeni akiba ya Maneno, msiwahukumu Wazanzibar wala ACT-Wazalendo

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,141
2,000
Mada inahusika,

Ujumbe huu unawahusu wana mageuzi wa Kweli wa CHADEMA na GT pekee na sio wafia chama na wapiga debe.

Kuifahamu historia ya mapambano ya Zanzibar walau kuanzia 1995 hadi sasa
Vyovyote iwavyo huwezi kuacha mchango wa Maalim Seif na wanamageuzi wenzake. Tafakarini nguvu ya Upinzani Zanzibar licha ya uchache wa watu wa huko lakini wamejitofautisha kwa mbali na watu wa huku Bara. Kikubwa ni uaminifu, umadhubuti na kujielewa. Hiyo inachagizwa na AJENDA ya Zanzibar.

Chama chochote kile kikikubalika Zanzibar na Yumkini wafuasi wa Maalim Seif hicho chama kinakuwa na nguvu kwa siasa za Zanzibar. Ilikuwa CUF na sasa ni ACT. Kwanza kubalini kuwa ACT kwa sasa Zanzibar ndio inakubalika na imebebeshwa Ajenda ya Zanzibar kupitia Maalim Seif.

Kumbukeni kuwa Wazanzibari wamepitia mateso mengi, maudhi, kebehi, mauaji na kila aina ya uovu wa kisiasa kuliko jamii nyengine yoyote hapa Tanzania baada ya kuja vyama vingi. Kumbukeni hawa wanajuwa wanachokifanya na kamwe hawahitaji mwalimu wa kudadavuwa kutoka kwengine.

Kitendo cha Kupendwa ACT-Wazalendo ni baada ya wasaliti ndani ya CUF kutaka kuipoteza Ajenda ya Zanzibar. Wazanzibari wanahitaji viongozi wakweli na wanaotambua shida zao ndani ya Muungano. Kiongozi yoyote wa chama chochote kile hawezi kuuungwa mkono Zanzibar bila kukubaliana na usalama wa ajenda zao.

Kama mnakumbuka migomo ya 1995 hadi wanafunzi kufukuzwa mashule, wafanyakazi wapinzani kufukuzwa makazini, watu kuuwawa yalitokea Zanzibar pekee hadi ikafanyika miafaka ya awali zaidi ya miwili na bado hakukuwa na mafanikio. Wakati Wazanzibari wanafanya haya na hadi kuilazimisha CCM kuuwa na kuzalisha wakimbizi mwaka 2001 Wazanzibari walikuwa Peke yao wakati ule na CUF yao.

Wakati wanagoma, kunyanyaswa na kudhulumiwa hivyo vyama vyengine vilikuwa havionekani kukerwa na kilichowapata Wazanzibari. Hatukuona wengine wakiandamana na kupaza sauti za wazi. Watu walifikiri yale yaliwahusu wazanzibari sasa jitihada hizo za kujitolea hadi kufanikiwa Zanzibar kuwa na GNU kulihitaji Sacrifice na Risk za roho za watu. Hatua hiyo hata kama haijafanikisha malengo kwa asilimia mia lakini walau kuna kauchochoro fulani ambacho kwa Upande wa Bara hata robo ya siasa za Zanzibar hazijafikia.

Maana yangu wasitokee wana Mageuzi hasa CHADEMA tunayoiamini, ikawa wepesi wa kusahau historia na kushindwa kuitazama Zanzibar kwa jicho la pekee. Hii inaitwa Zanzibar Chapter, siasa za kule zisichukuliwe kirahisi kihivyo.

Hebu jiulizeni kwa nini mara baada ya Maalim Seif kufanikiwa yeye na Mh Mstaafu Karume kupata GNU wahafidhina wa CCM walichukia kweli kweli?

Jiulizeni Miaka 5 ya GNU ya 2010 - 2015, wahafidhina walivyopata tabu ndani ya serikali na sasa kutamani kuivunja GNU?

Tukubali tu chama chochote kitakachokubali kubeba ajenda ya Zanzibar bila watu wengine na wafuasi wa vyama vyengine kuielewa siasa ya Zanzibar wanaweza kuwahukumu tofauti viongozi wa vyama kama inavyoonekana leo ACT. Hiki ni chama ambacho kama vilivyo vyama vyengine lazima vitangulize maslahi ya wanachama wao na hapa muhimu ni ile dhana ya Zanzibar Chapter. Huwezi kuendesha siasa za Zanzibar kwa mtazamo wa Tanzania nzima. Kama kuna Viongozi ndani ya CHADEMA au kwengineko wanashindwa kuliona hili ndio huibuka zile dhana za Ukoloni wenyewe.

Hivi unadhani mtu kama Maalim Seif aweze kuwasaliti Wazanzibari kweli kama inavyotaka kuaminishwa leo eti kufuata vyeo ? wamesahau kwamba hakuna sacrifice ambayo hajaifanya ikiwemo hiyo ya kukubali kupoteza vyeo kwa maslahi ya wazanzibari?

Mtu ambaye ni mastermind anayejua wapi pa kugoma, wapi pa kususa, wapi pa kuridhiana wapi pa kusamehe, wapi pa kukemea, wapi pa kushupaa na wapi pa kulainika ili kufikia malengo eti watokee watu waanze kutumia scenario moja tu ya 2020 kuhukumu haya bila kujua kituo kiko wapi cha Maslahi ya Wazanzibari?

Hivi mnadhani ACT walikuwa wajinga kwenda kuchukuwa maoni ya wanachama wao Zanzibar yote? Hivi mnadhani siasa za Zanzibar zinahitaji direct method tu ? huko ni kutozijua siasa za Zanzibar.

Lau mngejua kwamba Dr Mwinyi anapata tabu ya Wahafidhina wa CCM leo na vile wahafidhina wanavyolaani ACT kukubali kuingia GNU basi baadhi ya wafuasi wenzetu wa Chadema wasingethubutu kupaza maneno ya kuudhi hadharani. Ni kukosa kujua kinachoendela Zanzibar.

Unaopaswa kuwa Mwelekeo Sahihi
Chukueni mwelekeo wa baadhi ya viongozi weledi ndani ya CHADEMA ambao hadi sasa wameamua kunyamaza kimya. Wekeni hakiba ya maneno kuhusu ACT na waachiieni ili mprove wrong ili mje muwasute baadae.

Tambuweni strategies za siasa na mikakati inatofautiana na wakati, mahitaji na maeneo. Eneo la Zanzibar ni very Perculiar, linahitaji lipewe nafasi yake na sio kuanza kuparamia Viongozi wa chama kinachokubalika huko bila kuzingatia hayo.

Tambueni kuwa Siasa za Zanzibar zinajitosheleza kwa sababu ya uwepo wa Muungano, ukishalijua hilo utajuwa Mbinu za mapambano ya Zanzibar sio lazima ziwe za Tanzania nzima.

Hakuna haja ya kutoa kebehi na matusi naamini iko siku kupitia haya maamuzi ya ACT wanamageuzi wanaweza kuja kuwapongeza hawa hawa ACT.

Chukueni dhana ya Maridhiano japo feki ikibidi iwasaidie kusogeza mbele dhana ya mageuzi na mapambano na jitahidini kusoma njiambali mbali za mapambano duniani.

MWISHO
Nachukuwa nafasi hii kuawapongeza ACT kwa kujali hisia za wengi za wanachama wao hasa wa Zanzibar na kuwatilia maanani kama supporters wao kindaki ndaki kwa sasa lakini na kwa pekee kuibeba ajenda ya Zanzibar kwa vitendo kwa kutambua siasa za Zanzibar zina kona nyingi. Natambua mchango wa manahodha Hodari waliopo ACT. Kudos.

Nashauri vyama vyengine viwape muda ACT na mambo ya ndani ya Upinzani yasianikwe hadharani kwa maslahi mapana ya Upinzani. Bora kuweka hakiba ya maneno. Kubwa zaidi watu watambuwe Zanzibar inahitaji kutazamwa kama Ajenda Maalumu kwenye siasa za Upinzani za Tanzania. Hawa walishatangulia katika mapambano ya siasa. Tukubali hilo na tuwe nao ili dhana ya mabadilo isonge mbele.

Nadhani nimeeleweka na wahuisika tu.

Kishada.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,962
2,000
Nachukuwa nafasi hii kuawapongeza ACT kwa kujali hisia za wengi za wanachama wao hasa wa Zanzibar na kuwatilia maanani kama supportes wao kindaki ndaki kwa sasa lakini na kwa pekee kuibeba ajenda ya Zanzibar kwa vitendo kwa kutambua siasa za Zanzibar zina kona nyingi. Natambua mchango wa manahodha Hodari waliopo ACT. Kudos.

Nashauri vyama Bora kuweka hakiba ya maneno. Kubwa zaidi watu watambuwe Zanzibar inahitaji kutazamwa kama Ajenda Maalumu kwenye siasa za Upinzani za Tanzania. Hawa walishatangulia katika mapambano ya siasa.

Kishada.
Naunga mkono hoja.
P
 

Real Patriotist

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
229
1,000
Jambo la ajabu ni hili; anayesema wanachadema "wasilaumu" au kuwabeza ACT na Maalim juu ya uamuzi wao kujiunga na GNU nae pia "anawalaumu" CHADEMA.

Anayesema wanamageuzi bora wangekaa kimya na kuwa na akiba ya maneno yeye mwenye hajakaa kimya kanyanyua kinywa chake kuwasema hao wengine,
Sasa mie nashindwa hata kuelewa kwa kweli mnatuchanganya.

Hebu mtuache sisi ni watu wazima tunaelewa mbivu na mbichi aisee msihamishe reli kabisa waliokosea tunawajua na kama uamuzi ni sahihi tunaelewa. Maanake humu kila mtu anavutia kwake na kumnanga aliyekinyume nae.

Lakini jambo ka kuelewa ni hili ya ACT waachiwe wenyewe na ya CHADEMA vile vile ila ipo siku kila mmoja atajipambania nafsi yake na watakapoungana wenye kufanana matatizo katika mapambano hapo ndipo itakapokuwa mbaya zaidi. Msione wananchi wamekaa kimya na wengine wameamua kufunika kombe mkadhani wanafurahishwa na huu uhanithi wenu endeleeni tu ila mkumbuke ipo siku hata yawezekana ikawa si kizazi chetu watakaoliona hili.
 

RugeWashington

New Member
Dec 7, 2020
1
20
Acha kutuaminisha oja zisizokuwa na mshiko ili kuondoa mjadala mezani.
Swali la Dw kwa katibu mkuu lilikuwa" Kwa kauli yenu sasa na kukubali kuunda serikali ya pamoja, ni kweli sasa mnaitambua na kuridhia uchaguzi mkuu 2020 na hivyo mnaitambua serikali serikali iliyopo madarakani. Hapa jibu lilipaswa kuwa ndio au hapana. Kisha swali la pili lingetegemea jibu la swali la kwanza. Kiufupi mimi nawapongeza wana Act. Ila msiendelee na hoja za nataka sitaki hii Tz ya sasa sio ya 1995,
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,141
2,000
Acha kutuaminisha oja zisizokuwa na mshiko ili kuondoa mjadala mezani.
Swali la Dw kwa katibu mkuu lilikuwa" Kwa kauli yenu sasa na kukubali kuunda serikali ya pamoja, ni kweli sasa mnaitambua na kuridhia uchaguzi mkuu 2020 na hivyo mnaitambua serikali serikali iliyopo madarakani. Hapa jibu lilipaswa kuwa ndio au hapana. Kisha swali la pili lingetegemea jibu la swali la kwanza. Kiufupi mimi nawapongeza wana Act. Ila msiendelee na hoja za nataka sitaki hii Tz ya sasa sio ya 1995,
Taja mfano wa hoja zisizokuwa na mashiko hapa. tuanzie hapo. Mimi nazungumzia CHADEMA kuweka Hakiba ya Maneno, wewe unazungumzia Suali la DW.
 

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,874
2,000
ACT imechagua njia ya diplomasia ili kuimarisha siasa nchini badala ya CCM kutuweka kwenye kona ya Uhasama.
CCM ukiwaendea wa utemi utamaliza nguvu zako,maana wanatumia Vyombo vya dola.
Siku Upinzani ukiungwa mkono na vyombo vya dola ,hapo ndio tunawez kusema tukaze msuli
 

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,180
2,000
Siasa za Zanzibar ni za kisultani. Kwa CCM ni kurithishana madaraka kati ya familia za Karume na Mwinyi, kwa upinzani ni usultani wa Maalim Seif.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
80,456
2,000
Napinga Maalim Seif kuingia SUK , alichokikataa 2015 ni kipi na anachokikubali leo ni kipi ? na hata Chadema wakileta ubwege kama huu hatutanyamaza , ukitaka kuona umakini wetu mwangalie Mdee leo , hana tofauti na Ebitoke kwa jinsi mitaa inavyomuona.

Ni kweli tumekuwa pamoja kwenye mapambano kwa miaka mingi , lakini kwa hili tusameheane , haiwezekani watu wauawe kwa namna ile halafu tushirikiane na wauaji , tumuogope Mungu , Maridhiano kwenye Uhai wa watu hayawezekani
 

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
272
500
SEMA BAADHI YA WAZANZIBARI SIO WOTE.
KAMA NI WOTE JE HAO WALIOKO MADARAAKANI NI KINA NANI?

WA OMAN AU WABARA?

TUNAJUA WAPEMBA NI WAFIA SULTANI NA WANA VINASABA NAE!

MANENO MEEENGI BADALA YA KUNYOOKA KWENYE POINT WEWE MLETA MADA UNAZUNGUKA MBUYU UKIBWABWAJA TU.

SEIF KISHA KATA MZIZI WA FITNA NENDENI MKAIJENGE NCHI SULTAN NAE KISHARUDI OMAN TOKA UINGEREZA NA AMEKUBALI YAISHE.
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,141
2,000
Kweli maalim ni game changer. Yaani Leo nimeamini watu walivyo wepesi wa kusahau.

Unaambiwa wahafidhina was CCM wanalia na kumlaani Mwinyi kwa nini asingewapuuza ACT hofu yao ni Maalim.

Huko upinzani nako watu wanafoka balaa.

Maalim huyu huyu akianza mambo take ndani ya SUK kwa maslahi ya upinzani watu watasahau haya.

Mimi nimeshauri watu waweke hakiba ya maneno tu. Wasimalize yote

Huyu mzee huwa anajuwa hesabu vizuri. Anajuwa wapi as use na kwa nini. Anajuwa wapi aridhie, wapi ashupae, wapi akemee, wapi adinde.

Naamini alijipa muda kuangaza note ndani na nje ya nchi. Hesabu zimeangukia ajiunge SUK. Mimi naamini si bure.

Muda utasema
,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom