Ujumbe huu kwa viongozi wa Bunge

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
Viongozi wa bunge walikuwa na nafasi/wana nafasi ya kubadilisha mtazamo wa wabunge wa upinzani ie CHADEMA kwa kufanya yafuatayo Kiongozi wa bunge (Spika/naibu spika/mwenyekiti wa kamati) kama mwamuzi wa mechi kati ya serikali na bunge inabidi asiwe na upande anaotetea bali wajibu wake uwe ni kuhakikisha sheria kanuni na taratibu za bunge zinafuatwa na pande zote mbili ie kwa huu wakati ambapo wabunge wengi wa CCM wamekuwa wakisimama kama serikali upande wa pili ni CHADEMA na baadhi ya wabunge wa NCCR MAGEUZI huku wengine wakishindwa waingie kambi gani na kubaki kana kwamba ni watazamaji nusu wapo CCM na nusu wapo kama wabunge nafasi ambayo kwa muda mwingi inachezwa na CHADEMA. Kisaikolojia wabunge wa CHADEMA wananyanyaswa kwa hiyo kutotendeka kwa haki sawa kokote kwa makusudi au bahati mbaya kutakakofanywa na kiongozi wa shughuli za bunge katika siku husika CHADEMA wanakuwa wepesi sana kuliona na kuchukua hatua wanazohisi wao zinafaa na endapo kiti kinapuuzia ndio tunayaona yanayotokea na yataendelea kutokea kama haki haitatendeka. Nilifuatilia jana jioni tarehe 18 june 2012 michango ya Tundu Lissu,Mwigulu Nchemba, na Kapteni Mstaafu John Komba. Nikianzia na Tundu Lissu alipotumia maneno yanayodaiwa ni ya maudhi mara moja Willium Lukuvi aliomba mwongozo akakubaliwa na Lissu akakaa chini Lukuvi akasikilizwa Lakini wakati Mwigulu Nchemba akichangia alitumia maneno ya maudhi kama "pepo" nk uliombwa mwongozo lakini haukushughulikiwa mara moja sio hivyo tu aliichia kwa kutupa kwa kupeperusha Bajeti mbadala hakuna hatua yoyote(onyo,mwongozo) uliotolewa kwa kitendo alichokifanya ambacho binafsi nilitafsiri sio cha kiungwana na ni cha kuudhi. Nimetolea mfano huu mmoja wa kuonesha jinsi viongozi wa Bunge wanavyoweza kusababisha kuchafuka kwa hali ya hewa ya bungeni kwa wafuatiliaji waliona jinsi wakati Mwigulu Nchemba akichangia jinsi kulivyokuwa na fujo za kutaka mwongozo baada ya mwendeshaji wa kikao kuendelea kupuuza maombi ya mwongozo. Viongozi wa Bunge watumie busara ya kiwango cha juu sana katika maamuzi yao hasa wanapoendesha vikao vya bunge wakumbuke wao ni kama marefa ambao wana nafasi kubwa ya kuharibu mechi. Kupuuzia na kuendelea na ushabiki wa kisiasa bungeni utapelekea maafa katika bunge letu. Mimi sio mtabiri lakini wasipojirekebisha na kuendeleza maslahi ya vyama vyetu tutegemee zaidi ya haya tuliyoona na kusikia siku hizi mbili Tanzania kwanza,vyama badae Stewart Frenk Njelekela. Mkulima-Ludewa Source:Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima
 
Kama wakulima huko Ludewa wanaelewa nini maana ya HAKI basi viongozi wa bunge tendeni haki sio kiminya haki bungeni wakati wa kuchangia.
 
CCM. Chama tawala kimeshika nchi na huu ni wakati wao wa kulinda/kujilinda wasiangukie pabaya. Lazima wengine wasubiri zamu zao kama watanzania wakiwapatia nchi. Nawaonea hurumu wabunge wetu kutoka Vyama vya upinzani. Wasikate tamaa Mola atawasaidia kama wanafanya kwa manufaa ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom