Ujumbe hatari wanaswa na serikali...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797



[h=1][/h]UJUMBE wa hatari unaotumwa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) umenaswa na Serikali.
Tayari baadhi ya Watanzania wametumiwa ujumbe huo ambao unaeleza namna ambayo umefika wakati wa mikoa ya Kusini kuwa Taifa huru ambalo linaweza kujitegemea na kuhimizwa kutumwa kwa watu wengi zaidi ili kufanikisha mkakati huo.

Akizungumza kuhusu ujumbe huo jana, mkoani hapa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema Serikali haitakubali kuona kuna watu ambao hawaitakii mema Tanzania wanaotaka kuigawa na kwamba tayari wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuwadhibiti wanaotuma ujumbe huo wenye lengo baya kwa Taifa.

“Kuna ujumbe mfupi unaotumwa katika simu za mkononi, ambapo unazungumzia kuigawa Tanzania. Naamini kuna baadhi ya wananchi watakuwa wameupata, lakini ni vema nikaurudia ili waufahamu unavyoeleza,” alisema Dk. Nchimbi.

Alinukuu ujumbe huo ambao unasema hivi: Mtwara kuanzia jiwe la mzungu Kilwa hadi Msimbati unapoishia Mto Ruvuma na Bahari ya Hindi Nanyumbu, Liwale hadi Kinjumbi inatosha kuwa nchi kubwa kuliko Burundi, Rwanda, Malawi Cape Verde, Botswana na zingine. Taifa letu litaiwa Tanzania ya Kusini.

“Tumepeleke maombi ya kujitenga Umoja wa Mataifa tuwe nchi huru Kusini kutoka zamani tuko nyuma ya pazia, kunja pazia liwalo na liwe. Wao wao sisi kwa sisi, mbona Sudan wameweza kugawana nchi, tuma ujumbe huu kwa watu wengi uwezavyo kwa watu wa Kusini,” ilisema sehemu ya ujumbe ambao Dk. Nchimbi alikuwa akiinukuu.

Hata hivyo, aliwahakikishia Watanzania kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha watu wenye nia ya kuigawa nchi hii hawafanikiwi na ipo tayari kutumia nguvu zake zote ili kukomesha watu wenye nia mbaya na taifa hili.

Aliongeza kuwa kwa wale ambao watatumiwa ujumbe huo wanatakiwa kujibu kwa kuandika ‘wrong number’ na kuongeza kuwa iwapo itatumwa meseji inayozungumzia namna ya kuwagawa Watanzania kwa aina yoyote unatakiwa kujibu hapo si mahala pale.

Dk. Nchimbi alisema pia iwapo watatokea watu ambao watafanya mikutano ya hadhara, lakini inaonesha nia ya kuwagawa Watanzania, wasikubali kusikiliza na badala yake waondoke eneo hilo kwani hiyo itamfanya huyo anayehubiri kuigawa nchi kukosa watu wa kumsikiliza lakini kama haitoshi bado wananchi wanatakiwa kumwambia kuwa hapo si mahala pake atatufute mahali pa kusemea hayo mambo yake.

Kuhusu ujumbe ambao unaashiria kuigawa nchi, alisema Serikali imejipanga na kutoa onyo ole wao ambao wanatumia simu za mkononi kuhatarisha amani ya nchi kwani watasakwa kokote walipo kwa maslahi ya taifa na kusisitiza wasijidanganye kwani hawataachwa.



ChANZO:JAMBOLEO.
 
Kweli Hiyo NCHI iakuwaje? GAS kwanza IKO BAHARINI sio sawasawa na BIAFRA, NIGERIA - Maneno ya Baadhi y Wanasiasa wetu Wanataka Umati Uwafuate kwa UDI na UVUMBA... a Hawajali ni kwa nja GANI; Hawajui When you feed someone too MUCH PROPAGANDA they become too HOT TO HANDLE...

Yaani kujitenga Kweli wanaENGINEER kwenye SECTOR hizi hapo CHINI?????


 
Hawa watu waccm wanaota sana, wanadhani wataendesha nchi kwa vitisho na ugangwe, kweli karne hii unaletea wananchi ugangwe, unawaletea walipakodi ..watu wanaovuja jasho lao kukushibisha wewe Nchimbi na serikali yako, na yule raisi wako kama kipepe, hivi kweli mtaweza na vitisho hivi katika karne hiiii?

Kweli aliye zoe vya kunyonga vya kuchinja hawezi.

Watoto wetu tutawaambia haya, wasikubali kuonewa hata kidogo na serikali ya ccm, na wawaambiae watoto wawatoto hayo.
 
Wakati mwingine viongozi wetu ni vichekesho kwelikweli. Hivi kweli anaamini wataondoka mkutanoni wamuache mhutubiaji kwa hali ilivyo?

Kwa hiyo hata huko misikitini na makanisani wanakohamasishana nako waondoke wawaache mashehe na mapdre peke yao?

Hili jambo dogo kiasi hiki tunashindwa kulimaliza kweli? Nchimbi tafuta njia nyingine za kumaliza huu mgogoro, vinginevyo utaonekana kituko.
 
Hawa jamaa huwa wanadhani wananchi ni wajinga wa kutupwa, wanawadanganya wana Mtwara eti wajue kuna watu wapo behind mzozo. Hakuna watu siku hizi wameelimika. kama serikali inaweza kamata ujumbe mfupi mbona magaidi , mafisadi hamuwakamati? MMMmmmmm Tanzania hii mtu waweza kufa CCM ikiendelea madarakani
 
Wakati mwingine viongozi wetu ni vichekesho kwelikweli. Hivi kweli anaamini wataondoka mkutanoni wamuache mhutubiaji kwa hali ilivyo?

Kwa hiyo hata huko misikitini na makanisani wanakohamasishana nako waondoke wawaache mashehe na mapdre peke yao?

Hili jambo dogo kiasi hiki tunashindwa kulimaliza kweli? Nchimbi tafuta njia nyingine za kumaliza huu mgogoro, vinginevyo utaonekana kituko.

akili ndo imeishia hapo, mshauri mkuu Mwigulu nchemba unategemea nini?
 
Huyu huwa ana tabia ya kuleta mambo ya utoto kwenye mambo serious. Tangu aliposema eti hawezi kupatikana waziri mwingne kama yeye huwa namwona he is not serious in anything. Coupled with alivyokuwa anajibu hoja wakati anawasilisha hotuba yake huwa namwacha kama alivyo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
the government must think twice and not judging through false own plans that they created to makes people to afraid of government.
 
Hii spinning ya kitoto kwa vyovyote ni serekali yenyewe inatafuta sababu na huruma.

Yani wanajijambisha halafu wanajipiga finga wenyewe!
 
Huyu huwa ana tabia ya kuleta mambo ya utoto kwenye mambo serious. Tangu aliposema eti hawezi kupatikana waziri mwingne kama yeye huwa namwona he is not serious in anything. Coupled with alivyokuwa anajibu hoja wakati anawasilisha hotuba yake huwa namwacha kama alivyo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Hata mm alini-bore sana wakati anajibu maswali pale bungeni wkt wa budjet yake, alikuwa anajibu kwa dharau sana.
 
Nchi hii ina matatizo mengi sana! Siamini huyu Nchimbi ni Dr wa nini? Kama Doctor of Philosophy, alifundishwa nini? Anashindwa kufikiri? Why? Anashindwa kufanya upembuzi wa kina, nini sababu ya matatizo hayo? Watanzania tumechoka siasa za katuni. Tunataka siasa inayoleta tija kwa watanzania. Vitisho haisaidii na ni dalili ya Serikali kuporomoka!

Nashangaa Polisi tunawapa mishahara wenyewe kupitia kodi zetu! Tunawanaunulia nguo na vifaa vya kazi halafu wanatuua sisi waajiri wao, mwananchi. This is totally shit!
 
''Nchimbi hana uwezo sawa na nafasi aliopewa, hapo hakuna mjadala. jamaa ana dharau wakati hana shule (contents za kichwani na sio vyeti) au labda anatumia dharau kama ''Deffence mechanism''. Kwa wakati huu tanzania ilivyo kisiasa hatuitaji watu kama Nchimbi. wahusika wa mlipuko wa Arusha wamekamatwa? au Inelijensia porojo ipo kazini kung'oa watu kucha? Watanzania wamechoka sana na hakuna kitakachozuia machafuko hata ya nchi nzima endapo mbinu za kiintelijemsia makini za mataifa mumiani zikianza kutumika kwa lengo la kutugawa ili wacume koulaini. Serikali dhaifu ya JK ina kazi moja tu ya kutuepusha na janga hili. "KUJIUZULU''
 
Yale yale ya hoja dhaifu.... eti andika 'wrong number.. '
naona wanataka kucheza na vichwa vya watu.. hakuna lolote kama hilo... hivi kwanini daima serikali ikiona hatari inajibu kwa weak arguments badala ya kutafuta arguments za kuridhisha?
Of course kusini kama sehemu nyingine ya Tzania watakuwa huru ikikita ile sera yetu ya majimbo.. kwa maandeleo ya nchi...na hili hakuna wa kulizuia iwe kwa vitisho kiasi gani...
Kusini, kaskazini, mashariki, magharibi vyote vitakuwa huru, na hakutakuwa na vitisho vyovyote kwa mtu au chombo chochote... kutakuwa tu na ushindani wa kimaendeleo kwa ajili ya kuiendeleza Tanzania yetu... Natamani kuiona hiyo siku.... na itakuja hiyo siku....
 
Back
Top Bottom