Ujumbe alioutuma Mh. Selasini muda mfupi kabla hajapata ajali Bomang'ombe

Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

Hata neno linatuambia kuwa ombeni nanyi mtapewa.......Pengine beyond madrasa hakuna mradi mwingine je??
 
Mwenye macho haambiwi TAZAMA.

Hiyo ndio michango ya Mh. Selasini Mbunge wa CHADEMA.

Tunamshukuru mungu anapokea maombi yetu.
Huyo sio Mungu bali ni pepo...Hakuna Mungu wa hivyo....wengine mkiitwa AL shaabab na mkiambiwa mna tabia za ki Alqaeda na Boko Haram mnalalamika....Hata Osama September 11 alinukuliwa kusema "mungu mkubwa"... Hakika huyo sio Mungu wa mbinguni.........Tumewazowea.
 
Hii dunia ni tambara bovu,hata ufanye mema mangapi hukosi lawama hao,angewapelekea msaada wangesema ametoa wapi hela fisadi,kwani kikwete ni mara ngapi mmesikia ametoa msaada makanisani?kwanini muwe wepesi kuhukumu,huwezi jipendekeza pesa inatafutwa, na Nakila aombaye hupewa.i know you guys are Great Thinkers hebu fikirini sana sio kupotosha chadema,kama wewe ukifagilii potezea tu sio upandikize mabaya alaah!
 
Hivi mbunge anapimwa utendaji wake ni kwa kutoa hela au kusimamia na kuibana serikali kutekeleza miradi yake kwa wananchi. Napata shida sana kwenye hili.
 
Pole kamanda na nakuombea kwa Mungu upone haraka na pole kwa waliofariki,Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi.Amina
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

Na hao wajasiriamali kwani hampo pia. au hizo shule nako hampo.
 
Nendeni kwa wananchi waheshimiwa mbona mwagawa tu hela watembelee uongee nao ache kuwasiliana na matu wako kwa mitandao.
 
Hayo kweli ndiyo majukumu ya mbunge? This way, tunaipatia serikali free ride.
 
Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...

Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...

Nyie kama wananchi wa Rombo, mnamsaidiaje mbunge wenu kutatua hizo kero zenu? Au mnakuja kupiga vuvuzela humu JF! Tafakari, chukua hatua!
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

We ndo mdini.
Kama wenye misikiti,na maimam awakujitokeza kumweleza shida zao angejuaje?
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki
Ndugu yangu ni ukweli usiopingika kuwa sehemu kubwa ya nchi yetu hasa bara wakaaji ni wakristo. Mimi kwenye jimbo ninalotoka hakuna msikiti. Sikuwahi kusikia adhana mpaka pale nilipoenda mjini. Wala dini uislamu sikuwahi kuisikia Katika utoto wangu. Nnachopenda kusisitiza ni kuwa si kila sehemu kuna msikiti. Au hata yakiwepo ni machache hasa bara hivo kutokuwepo kwa rekodi ya msikiti ambao umepata msaada kutoka kwa Mbunge inabidi uchunguze kabla ya kufikia hayo unayoyawazia.
Mfano ukienda kwenye rekodi za wabunge wa pemba utakuwa kuna msaada umetolewa kwa Kanisa? Kama ipo nadhani itakuwa michache.
 
Hana Mahusiano kabisa na Wananchi huku Jimboni, huwa anamtuma Katibu wake kuleta hiyo michango akidai yuko bize sana, PIA hajawahi kutoa pesa toka mfukoni mwake ila anatumia zamfuko wa Jimbo tu, hilo kila mtu huku Rombo analijua,(kama mfuko usingekuwepo, tusingemuona hata kwa uwakilishi unaofanywa sasa),posho za mleta michango toka Mfuko wa Jimbo ni kubwa kuliko pesa alizogawa mwaka jana.
Kwa ufupi hana chake, kama mnabisha njooni Rombo!
NASIKIA KUNA BAADHI YA VIJANA WANAZUSHA KUWA SINA USHIRIKIANO NA WANANCHI WANGU NA NIKICHEZA 2015 JIMBO LITARUDI CCM!

Kwa ufupi sana naomba niandike hapa baadhi ya michango yangu kama Mbunge kwa Wananchi wangu.
1. Ndueni Sec. 2Million (Ununuzi wa computer na Printer)
2. Mbomai Sec. 2Million (Ununuzi wa Computer na Printer)
3. Tarakea Sec. 2Million (Ukarabati wa mabweni ya Wasichana)
4. Msangai S/Msingi 1Million (Ukarabati wa vyoo)
5. Kikundi cha Wajasiriamali 2.Million
6. Kijiji cha Mashima 1.5 Million (Ujenzi wa ofisi ya Kijiji)
7. Ngaleku Sec. 2Million (Uingizaji umeme)
8. Kirongo Samanga 2Million (Ujenzi wa Kituo cha Polisi)
9. Kijiji cha Samanga 1.Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji)
10. Kirachi Sec. 2Million (Ujenzi wa Jiko)
11. Kitirima Kingachi 1Million (Ujenzi wa Kituo cha Polisi)
12. Katangara Mrere 500,000/= (Kikundi cha Kinamama-MAZINGIRA)
13. Ofisi ya Kijiji Mrere 2Million (Kuezeka Ofisi)
14. Kiraeni Sec. 2Million (Ujenzi wa mabweni)
15. Bustani Sec. 2Million (Kuunganisha Maji)
16. Ugwasi Sec. 2Million (Kuunganisha Maji)
17. S/Msingi Kwangao 2Million (Ukarabati)
18. Kwaya ya KKT Mkuu 600,000
19. Huruma Convent 2Million (Ukarabati wa mabwawa ya kufugia Samaki)
20. Tumaini Center 2Million (Msaada kwa Watoto Yatima)
21. Kikundi cha Vijana na Maendeleo 1Million (Mradi wa Kufuga Kuku)
22. Kilamacho Sec. 1Million (Kuingiza Umeme)
23. Maharo S/Msingi 1Million (Umeme)
24. Makiidi Sec. 2 Million (Ujenzi wa Madarasa)
25. Parokia ya Mkuu 1Million (Mchango wa Ujenzi nyumba za mapadre)
26. Shimbili Saccos 1Million (Ujenzi wa ofisi)
27. Kwaikuru S/msingi 1Million (Ukarabati wa mitaro ya maji ya mvua)
28. Kikundi cha Wajasiriamali cha MWANGARI 2Million (Ukarabati wa mashine ya kusaga)
29. Booni Sec. (Ukarabati wa Madarasa)
30. Mamsera Sec. 1Million (Ujenzi wa madarasa)
31. mamsera Sec. 300,000 (Ujenzi wa jiko)
32. Tanya Sec. 1Million (Ujenzi wa Madarasa)
33. Parokia ya Mahida 1Million (Ujenzi wa nyumba ya mapadri)
34. Ngoyoni 2Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kata)
35. Holili S/msingi 2Million (Ukarabati)
36. Holili 2Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kata)
37. Olele 2Million(Ujenziwa ofisi ya kata).

Hayo ni baadhi tu ya mambo madogo madogo ambayo nimeweza kuisaidia Jamii ya WanaRombo... Mikakati yangu na Mipango ya Maendeleo nitaitoa Siku chache zijazo....

Joseph Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA

SALA ZENU NI MUHIMU ILI AWEZE KUPONA NA KUENDELEZA GURUDUMU NA UKOMBOZI KWA WATU WA ROMBO NA WATANZANIA KWA UJUMLA.

Ujumbe huo aliuweka kwenye facebook wall yake
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

Waliomba wakanyimwa? au ni kulalama tu kama issue you MOU za huduma za jamii za kikiristo? Nitajie sehemu yenye msikiti huko rombo. Usiwe na mawazo ya udini kwenye kila jambo.
 
Adolf siku zote kama hujui kitu ni bora kukaa kimya. Fanya utafiti kwanza sasa kule Rombo ulitaka ajenge msikiti ama? maana Rombo imejaa Wakatoliki hata hao Lutheran aliwachangia kwaya wako wachache sana, mie sijawahi kuona msikiti kule. Halafu unapodai kuwa Chadema ni wadini ina maana hata kina Zitto Kabwe ambao ni Waislamu unawatusi na kuwadhalilisha. pima hoja yako usikurupuke ndugu

Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki
 
Ndugu yangu mbona umekaa kidini sana..utakufa siku c zako kwa kushabikia udini...unajuaje kama hizo parokia ziliombaa msaada kutoka kwake? Au unajua idadi ya makanisa na misikiti iliyo rombo?fanya tathmini kabla hujashutumu..

Na wewe umejuaje kama hizo Parokia zimeomba? Selasini mdini hafai kuwa mbunge
 
Mkuu Eddie kuupataa msikiti Rombo ni sawa na kulipata kanisa Iraq, sioni shida kabisa hapo!Rombo nzima ina misikiti haifiki mi 5!labda uende ukawasaidie kuanzisha.


Acha uongo wewe, Iraq makanisa ya kumwaga na Rombo misikiti ipo tena mengi sana!
 
Kuna maeneo ambayo hakuna misikiti. Muulize mtu aliyetoka jimbo la Moshi vijijini, vunjo. Vilevile kuna maeneo ambayo hakuna makanisa. Rombo ni mojawapo ya maeneo ambayo kuona msikiti ni kama kumwona kakakuona!

Granted! lakini Rombo misikiti ipo Mbunge wa Chadema na Chadema wadini nukta!
 
mkuu
Hata kama ni tofauti ya itikadi bado Tanzania hatujafika hapa ndugu kumlaani/kumwombea mabaya mtu mwenye matatizo si uungwana

Hakuna iliemuombea mabaya, soma between the lines if anything muombi ni muweze apitishie hukumu ya haki kwa Mh
 
Back
Top Bottom