Ujuha, unafiki, ushabiki na uzandiki ndio uliotufikisha hapa tukilalama kila kukicha, kisa Kiwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujuha, unafiki, ushabiki na uzandiki ndio uliotufikisha hapa tukilalama kila kukicha, kisa Kiwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Qamara, Nov 22, 2011.

 1. Q

  Qamara New Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni suala la kusikitisha raisi kuongea na wazee na kuwaeleza mambo ambayo hata mwanafunzi wa darasa la pili huwezi kumdanganya. Mtoto wa miaka nne hutumwa dukani kuchukua sbuni, majni ya chai, sukari, mafuta ya kupikia chakula. Ukimuuliza kuwa sukari robo inauzwa shilingi ngapi? bila shaka atakwambia ni tshs: 560. Sasa kiongozi mzima anawadanganya wazee tena hajui kama vyombo vya habarivinamfuatilia? hajui watu wanaomsikiliza si wazee wake wa CCM tu, kuna Watanzania wasomi, wchambuzi w kauli, wanazuoni n.k, ambao hutafsiri neno kwa neno.

  Inafahamika kuwa ndani ya CCM wamesha zoea kuwa uki jumlisha 2+5=8, badla y 7, hivyo sio ajabu kikwete kuwadanganya kama mazuzu wale wazee wake wa chma chake ambao baada ya kikao che kuisha hupewa 5000 za nauli. Tujikumbushe kweli Mwali Nyerere kila alipofika na kuhutubia wazee au wananchi wa sehemu yeyote nchini aliwapa nauli? . Sasa tukisema Kiwete ni muongo ni makosa, siku zote anpoongea na wazee wa DSM husema uongo, hutoa takwimu za bei za uongo kisa anataka kuwaridhisha wananchi kwa kuwahutubia wazee wanafiki wa CCM ambao ndio waliosababisha CCM kulifikisha nchi kuelekea porini na kuteketea kwa kasi, na kwa ari kubwa. Hakuna asiyejua kuwa bei ya sukari ni kubwa sana na hutofautiana kila sehemu ndani ya nchi hii. hapa DSM ukiwa Posta sukari ni Tshs: 2500, ukiwa Kariakoo ni Tshs: 2400/2600/2300, ukiwa Kigoma ni zaidi ya 3000.

  Nchi moja kila kata/wilaya/mkoa sukari bei tofauti. Hakuna asiyejua kuwa wafanya biashara wengi Tanzania ni makada wa CCM kila wilaya, kata, mkoa, na Taifa, wengine ndio walio mpatia uraisi kwa fedha zao, wengine walijitolea kwa hali na mali ili wapate wanachotaka baadaye.Sasa yamedhihirika kuwa aliyepiganiwa hana uwezo wa hata kufikiri bei ya sukari mitaani. Hatujui kazi ya usalama wa taifa ni nini? je nikukaa baa usiku, eti wanatafuta taarifa za iintelijinsia? hawana habari na hali ya uchumi wa nchi, mafisai wanakula nchi wanavyo taka kila sehemu nchi hii?. Hii ni aibu kwa kiongozi mkubwa kama raisi kutokujua hat bei ya sukari mitaani, ndio sababu Kikwete amepelekwa kufungua miradi mengi ya watu binafsi na kuambiw hii ni miradi ya serikali ya kilimo kwanza.

  Kwa hali hii, hii ni msiba mkubwa kwa taifa ambalo inaidadi kubwa ya watu wake ambao ni vijana wa kati ya miaka 0-35 wnakadiriwa kufikia 71% of the whole population. Tunatakiwa kufikiria upya kufahamu maana ya raisi na uraisi. tukijua hili hatutapata shida katika kumchagua kiongozi/raisi ambaye atatuelekeza kuelekea katika ukombozi wa matatizo yanayo tukabili.

  Tujadili hili kwani huu ni msiba mkubwa kwa taifa na kikwete hana maana yeyote ya kuendelea kutupotezea muda wetu, watu wenye haiba na karama ya uongozi ni wengi na anatutia kiwingu tu.
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tulitegemea katiba nzuri ili ikifika 2015 tuwaondoe lakini kwa mara nyingine wamejikinga which way to go???
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  ...eti wazee, kweli mimi nafanana na Dikteta??
  ...naweza kuamua kuwa dikteta, gazeti liwe la Daily News tu na la chama changu, UHURU!

  Hayo ni maneno ya RAIS wa nchi, jamani!
   
Loading...