Ujue waraka wa elimu kuhusu adhabu ya viboko shuleni Tanzania Bara

Sema Tanzania

Verified Member
May 18, 2016
245
500
Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, washika dau pamoja na wananchi wote kuwa mnamo mwaka 2002, Serikali ya JMT kupitia Wizara ya Elimu ilitoa Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko na kuweka utaratibu mahususi wa utolewaji wa adhabu ya viboko. Adhabu hiyo inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa ya jinai yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima. Waraka huu pia unaongeza kuwa adhabu ya viboko itakayotolewa sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Nani mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwanafunzi kwa viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko umeweka bayana kuwa ni Mwalimu Mkuu wa shule husika ama mwalimu mwingine atakayeteuliwa na mwalimu mkuu kwa maandishi, kila mara kosa linalostahili adhabu hii linapotendeka. Aidha, waraka huu unaonya kuwa mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike.

Waraka umeweka wazi kuwa kila mara adhabu ya viboko inapotolewa sharti iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, la kujaza taarifa zihusuzo adhabu husika, hii ikiwa ni pamoja na jina la mwanafunzi aliyepewa adhabu, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo. Kwa kuwa waraka unamtambua Mwalimu Mkuu kama mtu mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi husika basi unamtaka pia atie saini yake katika kitabu hicho maalum kila adhabu ya viboko inapotolewa.

Waraka unasemaje pale mwanafunzi / mzazi anapokataa adhabu ya viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko unasema mwanafunzi anapokataa adhabu ya viboko sharti asimamishwe shule ili kupisha hatua zingine za kinidhamu juu ya kosa lake.

Mwisho kabisa waraka huu unawaonya waalimu kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atakiuka utaratibu ulioidhinisha na waraka huu. Kwamba kupitia Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko ni marufuku kwa mwalimu yeyote kuonekana na fimbo mkononi kwa lengo la kumuadhibu mwanafunzi.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
 
  • Thanks
Reactions: cmp

Mgugu

JF-Expert Member
Jul 1, 2015
2,154
2,000
Nyie ndio mnatuharibia watoto wetu kenge nyie, watoto wanakosa heshima na adabu kwa kuendekeza uzungu wenu.
Hata vitabu vya dini vinahimiza tusiwanyime mboko watoto wetu.

Maendeleo hayana chama
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,371

Safi kabisa mkuu ila hawa walimu wa kibongo hawana muda wa kusoma hili kwakuwa sifa mojawapo ya kuwa mwalimu ni kufeli/kupata alama za chini kwenye mitihani ya form four na form six.Sasa hapo tunapata walimu wasio na weledi wala uelewa wa sheria,kanuni,taratibu na miongozo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
3,694
2,000
Huna mtoto wewe ndo maana unajiropokea tu.Ungejua watoto wanavyochapwa mashuleni ni kama wanyama hakuna utaratibu wa kuwaadhibu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio ivyo mkuu naelewa kadhia wanazo kutana nazo watoto wetu lakini suala la kuwaadhibu watoto haliwezi kuzuilika kabisa kama marekebisho ya sheria hizi yawepo lakini si kwa kuondoa viboko mashuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: cmp

cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,371
2,000
Nyie ndio mnatuharibia watoto wetu kenge nyie, watoto wanakosa heshima na adabu kwa kuendekeza uzungu wenu.
Hata vitabu vya dini vinahimiza tusiwanyime mboko watoto wetu.

Maendeleo hayana chama
Unaonekana bado hujabahatika kupata mtoto ndo maana waongea haya.Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.Watoto wanapewa adhabu kubwa mno zaidi ya jeshini bila kuzingatia umri,jinsi nakadhalika.Shida nyie walimu sifa mojawapo ya kuwa mwalimu sharti upate matokeo mabaya ndo unakimbilia kwenye ualimu kama last option.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,371
2,000
Sio ivyo mkuu naelewa kadhia wanazo kutana nazo watoto wetu lakini suala la kuwaadhibu watoto haliwezi kuzuilika kabisa kama marekebisho ya sheria hizi yawepo lakini si kwa kuondoa viboko mashuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria na muongozo uliopo ni mzuri mno tatizo walimu hawafuati muongozo wao vichwa vyao vinavyowatuma ndivyo wanavyofanya.Shame on them.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgugu

JF-Expert Member
Jul 1, 2015
2,154
2,000
Unaonekana bado hujabahatika kupata mtoto ndo maana waongea haya.Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.Watoto wanapewa adhabu kubwa mno zaidi ya jeshini bila kuzingatia umri,jinsi nakadhalika.Shida nyie walimu sifa mojawapo ya kuwa mwalimu sharti upate matokeo mabaya ndo unakimbilia kwenye ualimu kama last option.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa baba junior, ila nakuambia tu sheria za namna hii hazimjengi zaidi ya kumharibu mwanao. Mazingira ya shule zetu nadhani wewe mwenyewe unayajua hebu fikiria tunatengeneza vijana wa namna gani kwa mazingira haya tuliyonayo endapo sheria za kipumbavu namna hii zikiwa kweli zinatekelezwa.

Maendeleo hayana chama
 
Arista

Member
Feb 25, 2018
80
125
Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, washika dau pamoja na wananchi wote kuwa mnamo mwaka 2002, Serikali ya JMT kupitia Wizara ya Elimu ilitoa Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko na kuweka utaratibu mahususi wa utolewaji wa adhabu ya viboko. Adhabu hiyo inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa ya jinai yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima. Waraka huu pia unaongeza kuwa adhabu ya viboko itakayotolewa sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Nani mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwanafunzi kwa viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko umeweka bayana kuwa ni Mwalimu Mkuu wa shule husika ama mwalimu mwingine atakayeteuliwa na mwalimu mkuu kwa maandishi, kila mara kosa linalostahili adhabu hii linapotendeka. Aidha, waraka huu unaonya kuwa mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike.

Waraka umeweka wazi kuwa kila mara adhabu ya viboko inapotolewa sharti iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, la kujaza taarifa zihusuzo adhabu husika, hii ikiwa ni pamoja na jina la mwanafunzi aliyepewa adhabu, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo. Kwa kuwa waraka unamtambua Mwalimu Mkuu kama mtu mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi husika basi unamtaka pia atie saini yake katika kitabu hicho maalum kila adhabu ya viboko inapotolewa.

Waraka unasemaje pale mwanafunzi / mzazi anapokataa adhabu ya viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko unasema mwanafunzi anapokataa adhabu ya viboko sharti asimamishwe shule ili kupisha hatua zingine za kinidhamu juu ya kosa lake.

Mwisho kabisa waraka huu unawaonya waalimu kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atakiuka utaratibu ulioidhinisha na waraka huu. Kwamba kupitia Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko ni marufuku kwa mwalimu yeyote kuonekana na fimbo mkononi kwa lengo la kumuadhibu mwanafunzi.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
Tusipo wapiga viboko akina lissssuuuu watakuwa wengi humu nchini,lazima mtoto afunzwe adabu na heshima .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom