2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 2,982
- 4,457
Bila kupoteza muda kwenye mada.
Najua wengi mshasikia sana mambo ya kutafuta sarafu flani ya zamani na kuahidiwa kupewa donge nono la pesa.
Kwa sasa kuna page hapo Insta inajitangaza kutafuta hazina za Kijermani za kale ni vitu vingi wanasema zikiwemo hizo coins.
Jambo la kujiuliza bank zote duniani hazina hii sarafu kwa dau hilo kweli? Na ina kazi gani? Labda wataiweka kwenye majumba ya makumbusho kwa ajili ya utalii, je ni kweli? Si kweli kwani kuna watu wanazo na wamecoment lakini hakuna Mrejesho au jinsi ya kukabidhiana.
UTAPELI UKO HIVI
Wanajipanga watu kadha atokezaa mtu mwenye sarafu na mwingine anatangaza kuitafuta hii kwa dau kumbwa labda mil 10, akitangaza vijana wataingia mtaani kuisaka, mwingine anajifanya anajua mwenye nayo akitaka ahadi ya pesa pindi akionyesha. Wanakubaliana kwenda kwa mwenye nayo inaonyeshwa wanapatana labda mimi nakupa mil 2
Anapigiwa bosi simu kuhakiki je unaitaka kweli? Anajibu ndio naitaka. Hapo vijana washapata uhakika hata kama hawana pesa lazima wakakope sababu wana uhakika na pesa tena ndefu. Unaingia mkopo unakwenda kulipia ile sarafu baada ya kulipa sasa uko na mtangaza tenda kwenda kwa boss kukabidhi sarafu ili upewe mil 10.
Unafika kwa boss anakwambia kashapata na haitaji tena nyingine, unapunguza dau hadi mil 2 ili kurudisha pesa yako anakataa katu kata.
Wanakwenda kwa mwenye sarafu kujaribu kurudisha anakwambia yeye mwenyewe alinunua kwa sababu ilikua inatafutwa na pesa kashatumia. Mpaka hapo hujatapeliwa? Umenunua sarafu ya sh 100 kwa mil 10 hujaishia jela?
Jambo la kutafakari huwezi kupata pesa nyingi kwa muda mfupi lazma uumie tu.
Wenye sarafu za Kijermani dili hilo hapo. Mimi ninayo tayari.

Kwanini pesa hiyo inunuliwe kwa pesa nyingi hivyo? Utaambiwa ni dawa, madini au ina kazi maalumu.Mf. kisa cha @LwandaMagere aliambiwa atafute tsh 100 ya mwaka 1993 atapewa milioni 100