GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,546
- 108,876
Kabla ya AFCON 2019 Kauli zao zilikuwa…..
“ Tuna Timu nzuri, bora kabisa na Taifa Stars hii ya Rais Magufuli na jinsi anavyoijali na ilivyofanya Maandalizi makubwa huku tukiwa na Mchezaji wetu Gumzo kwa sasa Ulaya nzima Mbwana Samatta itaweza Kufanya vyema kabisa huko na Dunia itajua kuwa Tanzania ipo juu katika Soka kwa sasa Barani Afrika na tunauhakika wa Kupata Alama Nne ili ziweze Kutuvusha 16 bora “
Baada ya Kufurumushwa kwa Aibu AFCON 2019 Kauli zao zimekuwa….
“ Ugeni umetusumbua, hatukuwa na Timu imara, Wachezaji hawakupewa Posho zao, Majeruhi yaliongezeka, Joto huko nchini Misri lilikuwa Kali kuliko hata la nchini Kwetu Tanzania, hatukuwa na Wachezaji wengi wanaocheza Soka nje ya Tanzania, hatukubeba Mashabiki wetu ambao wangeenda Kuishangilia Timu yetu ambapo kwa Mzuka wao hao Senegal, Kenya na Algeria wangetukoma na isitoshe lengo Kuu la Tanzania wala halikuwa Kushiriki kivile katika Mashindano haya bali tumeenda tu kupata Uzoefu na pia kuwapa Exposure Wachezaji wetu “
Hakuna Watu wa Ajabu duniani kama Watanzania. Tukiamua Kuacha Unafiki wetu nina uhakika tutafanikiwa kwa mambo mengi sana tu ila kama kuna Dhambi ambayo kila mara ndiyo imekuwa ikitugharimu Watanzani katika mambo yetu mbalimbali iwe katika ngazi ya Mtu Mmoja Mmoja au Kijamii basi ni Undumilakuwili Wetu.
Tujitafakari bado hatujachelewa.