Ujue Undumilakuwili na Unafiki wa Watanzania walio wengi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
37,632
2,000
Kabla ya AFCON 2019 Kauli zao zilikuwa…..

“ Tuna Timu nzuri, bora kabisa na Taifa Stars hii ya Rais Magufuli na jinsi anavyoijali na ilivyofanya Maandalizi makubwa huku tukiwa na Mchezaji wetu Gumzo kwa sasa Ulaya nzima Mbwana Samatta itaweza Kufanya vyema kabisa huko na Dunia itajua kuwa Tanzania ipo juu katika Soka kwa sasa Barani Afrika na tunauhakika wa Kupata Alama Nne ili ziweze Kutuvusha 16 bora “

Baada ya Kufurumushwa kwa Aibu AFCON 2019 Kauli zao zimekuwa….

“ Ugeni umetusumbua, hatukuwa na Timu imara, Wachezaji hawakupewa Posho zao, Majeruhi yaliongezeka, Joto huko nchini Misri lilikuwa Kali kuliko hata la nchini Kwetu Tanzania, hatukuwa na Wachezaji wengi wanaocheza Soka nje ya Tanzania, hatukubeba Mashabiki wetu ambao wangeenda Kuishangilia Timu yetu ambapo kwa Mzuka wao hao Senegal, Kenya na Algeria wangetukoma na isitoshe lengo Kuu la Tanzania wala halikuwa Kushiriki kivile katika Mashindano haya bali tumeenda tu kupata Uzoefu na pia kuwapa Exposure Wachezaji wetu “

Hakuna Watu wa Ajabu duniani kama Watanzania. Tukiamua Kuacha Unafiki wetu nina uhakika tutafanikiwa kwa mambo mengi sana tu ila kama kuna Dhambi ambayo kila mara ndiyo imekuwa ikitugharimu Watanzani katika mambo yetu mbalimbali iwe katika ngazi ya Mtu Mmoja Mmoja au Kijamii basi ni Undumilakuwili Wetu.

Tujitafakari bado hatujachelewa.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
39,172
2,000
Tuweni wa kweli na wawazi ili tuweze kusonga mbele, kwenye kile kikundi kinachoitwa Timu ya Taifa, ni kiasi gani Taifa limefanya investment pale? Utakuta ni Zero, hatuna Academy, hatuna UMISETA, UMITASHUTA, MICHEZO YA MASHIRIKA/MAKAMPUNI then ngenge fulani la watu wenye matarajio yao wenyewe wanaamua kujiunga na kuanzisha kikundi chao cha mpira wewe unakuja na siasa zako na kukiita Timu ya Taifa.....tuache unafiki, matokeo mazuri ni baada ya maamuzi mazuri, investment ya longtime na kuweka siasa kando.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
39,172
2,000
mfano mzuri, kabla ya 2017 pengine, ni nani alikua akimfahamu Mwakinyo (bondia), ni kiasi gani kilikua invested kwake in terms of cash, technical and moral support? Hakuna! Leo hii amefanilkiwa kw ajuhudi zake binafsi basi kuna wapuuzi wa CCM wanasema ni juhudi zao
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,313
2,000
wamejitahidi,nasikia ni kwa muda mrefu hatujawahi kuingia kwenye hayo mashindano...I mean ku qualify..
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
37,632
2,000
Tuweni wa kweli na wawazi ili tuweze kusonga mbele, kwenye kile kikundi kinachoitwa Timu ya Taifa, ni kiasi gani Taifa limefanya investment pale? Utakuta ni Zero, hatuna Academy, hatuna UMISETA, UMITASHUTA, MICHEZO YA MASHIRIKA/MAKAMPUNI then ngenge fulani la watu wenye matarajio yao wenyewe wanaamua kujiunga na kuanzisha kikundi chao cha mpira wewe unakuja na siasa zako na kukiita Timu ya Taifa.....tuache unafiki, matokeo mazuri ni baada ya maamuzi mazuri, investment ya longtime na kuweka siasa kando.
Kiongozi sikujui ila kwa haya Maelezo yako tu yenye Umakini na Ukweli mtupu sihitaji Kukuchambua sana ili niweze kujua kuwa una Akili na ukweli ni kwamba upo vizuri mno Kichwani na nimevutiwa hasa na Ujengaji wako wa Hoja na mpangilio mzima wa Facts zako. Uko vizuri Kiongozi na Heko pia.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
39,172
2,000
Kiongozi sikujui ila kwa haya Maelezo yako tu yenye Umakini na Ukweli mtupu sihitaji Kukuchambua sana ili niweze kujua kuwa una Akili na ukweli ni kwamba upo vizuri mno Kichwani na nimevutiwa hasa na Ujengaji wako wa Hoja na mpangilio mzima wa Facts zako. Uko vizuri Kiongozi na Heko pia.
Barikiwa sana sana, tuweni wa kweli
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,208
2,000
Hawa, yaani mtu anakaa ikulu anapokea mgeni mzungu anamuita MUHESHIMIWA, muwekezaji, rafiki yetu, mtu makini...akipanda jukwaani kuhutubia mzungu yule yule anamuita BEBERU, Mwizi...yaani sie acha tuendelee kuwa maskini ni ma pro..wa undumila kuwili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom