kaijage mkiza
New Member
- Oct 19, 2016
- 4
- 1
Asante mkubwaNiliwahi kupata tatizo kama lako hilo mkuu na nikatumia dawa hizo hizo na sindano juu (gentamycine) lakini wapii. Nikaenda hospitali kubwa nikafanyiwa kipimo kikubwa zaidi cha mkojo kinaitwa urine culture ndio akaonekana bacteria anayesumbua na kutibiwa. Kwenye majibu ya kipimo pia niliorodheshewa list ya dawa ambazo haziwezi kummudu bacteria huyu (ambazo kimsingi zote nilikuwa nimeshatumia). So mkuu achana na hayo madawa kwanza yatakuua figo ni makali mno. La msingi ingia mfukoni tafuta hospitali makini yenye wataalamu makini ukafanye kipimo cha uhakika uone tatizo ni nini. Hizi hospitali zetu za nchi ya viwanda hazitibu mkuu ni vituo vya kukomaza maradhi na kusindikizana akhera tu. Kule wanafanya kazi kwa mazoea tu, mf. ukimtajia dalili hizo ye anaconclude tu ni STD anakutwanga dozi moja amazing. Unapokwenda kutibiwa kwingine usiache kumwambia Dr. historia ya matibabu yako na dawa ulizotumia. Binafsi Dr. alishangaa sana nilipomueleza historia ya matibabu yangu na akanipa kauli moja kuwa kwny tatizo langu ilitumika bunduki kuua mbu.