Ujue ugonjwa wa Kichocho (Bilharzia); Chanzo, dalili na tiba

mwakyoma2011

Member
Mar 10, 2011
17
0
Nina kichocho dalili nimeanza kuziona leo. Je, dawa gani ya kutibu ugonjwa huu?

----- Maoni kutoka kwa wadau-----

MziziMkavu anasema,
Ndugu pole sana kwa kutokwa na damu wakati unakojoa ni Dalili ya Ugonjwa wa kichocho nenda Hospitali kamuone Daktari haraka iwezekanavyo upate kutibiwa.

KICHOCHO (Biliharzia) NI UGONJWA HATARI

unnamed+(33).jpg

Aina za Konokono wanaoambukiza Kichocho na wale wasio ambukiza. Sehemu wanaopenda kukaa Konokono

Namna ya uambukizwaji

Kichocho ni ugonjwa usababishwao na vijidudu ambavyo mtu hupata anapotumia maji yaliyo na vijidudu vya ugonjwa huu hashwa katika nchi za kitropiki. Bilirhazia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Viini vilivyokomaa huishi katika mishipa katika kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa.

Mayai yanapokuta maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi, ambao hupenya konokono hawa wa majini. Katika konokono hawa wa majini viluwiluwi huwa hukua na kuongezeka na kutoka. Viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya kwenye ngozi na wakisha penya huingia hadi kwenye mishipa ya Ini ambapo hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu na haja kubwa.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka mitatu na nusu lakini huweza kuwa zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpaka na kibofu husababisha athari kubwa. Maambukizi yasiyotibiwa husababisha matatizo ya Ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Wakati mwingine mayai huingia katika uti wa mgongo au mara nyingine katika ubongo.

Jinsi ya kujizuia

Inasemekana hakuna chanjo iliyopatikana. Katika nchi ambazo ugonjwa huu upo, inadidi kujitahidi kuepuka maji ambayo si Safi na salama. Usidhani ya kuwa maji yoyote ni safi na salama katika sehemu zenye ugonjwa huu. Kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea, hizi ndizo sehemu za hatari.

Fukwe za bahari na fukwe zilizo na mawimbi si rahisi kuwa na konokono wa majini, hivyo hizi sehemu zinaweza kuwa salama. Viluwiluwi huweza kuishi kwa masaa 48 baada ya kutoka kwa konokono na huweza kusafiri mwendo mrefu, kwa sababu hii maeneo yenye maji katika sehemu zenye ugonjwa huu hayawezi kuwa salama kabisa.

Maziwa katika nchi ya Tanzania na Malawi yana vimelea vya kichocho, lakini fukwe nyingi karibu na mahoteli ya kitalii yana uoto mdogo wa mimea hivyo huwa ni sehemu ambazo si rahisi kupata ugonjwa huu.
Mabwawa ya kuogele ni salama kama yana dawa ya klorini (chlorine) na hakuna konokono wa majini.
Bahari ni salama
Maji ambayo yamatuama kwa siku tatu ni salama endapo hakuna konokono wa majini.Maji ya kuoga yanayochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mito na maziwa yanaweza kusabaisha maambukizi.

Namna ya kujikinga na kichocho

Kama unapopalilia, vaa mabuti marefu ya mpira. Viluwiluwi hawa hufa haraka mara tu wanapokuwa nje ya maji na hawawezi kuepuka kifo. Nguo na ngozi zenye maji zikikaushwa kwa haraka husaidia kujikinga na maambukizo.

Dalili za maambukizi
Wasafiri wengi walioambukizwa huwa hawaonyeshi dalili yeyote ya ugonjwa huu
Kunakuwa na mwasho katika sehemu alipoingilia kimelea kama "mwasho wa muogeleaji".Unapata homa baada ya wiki nne baada ya kutumia maji yaliyoambukizwa. Unapatwa na kikohozi kikavu ndiyo dalili ya hatua hii ya maambukizo. Kupungua kwa uzito na kujihisi kuchoka. Damu katika mkojo na haja kubwa kama ugonjwa umekomaa. Na pia kuvimba kwa miguu. Na muda wa kuambukizwa huchukua wiki nne (4) kwa mayai kuonekana katika choo na kuonekana kwenye mkojo. Lakini hata hivyo ikishajua tu umetumia maji yenye vimelea basi inabidi uchunguzi ufanyike miezi mitatu baada ya kutumia.

Tiba ya kichocho
Kichocho hutibiwa na madawa maalumu dhidi ya vimelea hivi ambazo hupatikana katika kliniki na hospitali yoyote ile iliyo karibu na makazi yako. Ni vizuri kupima mara kwa mara unapopatwa na mashaka ya kuambukizwa na kichocho hasa baada ya kutumia maji yenye vimelea vya kichoccho
 
Dawa ni praziquanter. Bado kuna umuhim mkubwa mno wa kwenda hosp. Labda utwambie kwnn hutaki kwenda hosp.
 
Dalili gani? Kichocho sio ugonjwa wa mchezo, unatibika kirahisi lakini ukichelewa tiba unaweza kupata madhara makubwa baadae ikiwapo saratani ya kibofu cha mkojo.Nenda hospitali ukachunguzwe wahakikishe kama kweli ni kichocho yaweza kuwa ni tatizo jingine.

Kichocho kinarespond vizuri sana kwa praziquantel 40mg/kg body weight as a single dose. Hospitali ni muhimu anyway.
 
Kweli naamini watanzania wameichoka sekta ya afya na hawaimini hata kidogo!
Nenda kwa babu ukapate kikombe.
 
Hebu achana na kujitibisha nyumbani, fasta nenda hospital kapate vipimo uanze dawa. Baada ya hapo uwe unaoga maji safi na salama. Kichocho kikikomaa ni hatari.
 
Kichocho kinarespond vizuri sana kwa praziquantel 40mg/kg body weight as a single dose. Hospitali ni muhimu anyway.

Madakatari mtindo huu utatuponza..I dont support prescribing in a forum like this, huyu mtu ni wa kushauriwa aende hospitali akapate uchunguzi na tiba, sioni sababu ya kuogopa kwenda hospitali na kichocho. ncahlelea mtu mwingine naye asije akapata kichocho au ndugu/rafiki mwenye kichocho naye akaprescribe!
 
We riwa mbona umeangalia kwenye prescription tu wakati post yote imesisitiza huyu mtu aende hospitali? sijui unacholalamika ni nini, hata hivyo hakuna mtu asiyejua umuhimu wa hospitali, mtu akiuliza hapa kwenye forum anataka aelimishwe zaidi, na wengine wanataka kulinganisha matibabu alopewa kama yanaendana na ushauri alopata hapa. Sioni tatizo la hicho unachokilalamikia wewe. Mfano mtu akiuliza namna ya kutengeneza nywele utamwambia aende Saloon, unafikiri saloon hakujui, anataka apate opinion ya wataalam ambao anadhani watamsaidia.

Riwa prescription ninazotoa mimi hazina matatizo ni standard kama wasiwasi wako ni huo, kungekuwa na uwezekano wa kufanya investigations online, na kupata uhakika wa diagnosis ningetibu hapa hapa na najua hata wewe ungenishukuru siku moja, sema wabongo hamuaminiani ndio maana hamtakuja muendelee.
 
ma dr please mnadhalisha fani,hyo praziquantel what if iki fanya reaction?piahuyu mtu aja sema ameona dalili gani ?huenda dalili hzo zikawa siyo za schistosomiasis.best choice nenda hospital
 
watanzania tu wavivu sana wa kusoma, wengi wanasoma introduction wanadhani wameelewa somo, sijaona hata post moja humu ambayo haijamwambia huyu bwana aende hospitali, sasa inapotokea watu wanaanza kulaumu na eti watu wanadhalilisha fani nashindwa kuelewa, I thought mtu akiomba msaada humu jamvini anasaidiwa as much as one can, lakini naona ukitoa msaada unadhalilisha fani. Nawashauri madaktari kwenye hili Jukwaa tafadhali msiwape watu ushauri mnadhalilisha fani, my keyboard is not working in this forum from today, I have got some people P.Messaging me for help and I have been helping kumbe nadhalilisha fani, sorry, I wont do it again people, endeleeni kushauriwa na google browsers.
 
Ugonjwa wa Kichocho ni ugonjwa hatari unaenezwa na konokono wanaoishi katika maji baridi (yasiyo na chumvi) katika nchi za kitropiki. Ugonjwa huu unasababishwa na minyoo bapa wanaoshambulia zaidi maini, utumbo mpana, kibofu cha mkojo, mapafu na hata ubongo. Huu ni ugonjwa unashika nafasi ya pili duniani kwa magonjwa ya vimelea (wa kwanza ni Malaria).

Inakadiriwa (WHO, 2010) kuwa takribani watu milioni 200 duniani wanaambukizwa ugonjwa kichocho, 85% ya watu hao wanaishi Afrika na watu milioni 100 wanaishi ni minyoo hii bila kuonyesha dalili yeyote. Inakadiriwa pia kuwa takribani watu milioni 700 duniani wapo katika hatari ya kuupata ugonjwa huu kwa sababu ya kazi za uvuvi, kilimo, ufugaji, nyumbani au za burudani (kuogelea, kutalii kando ya mito,mzaiwa na bahari) zinazowapeleka katika katika maeneo yenye maji yenye minyoo hii bapa. Watu laki 5 wanakadiriwa kufa duniani kote kutokana na ugonjwa wa Kichocho.

Ripoti ya mwaka 2000 ya Chitsulo na wenzake ilikadiria kuwa watu waliokuwa na ugonjwa wa kichocho walikuwa milioni 15, ambayo ilikuwa ni 57% ya Watanzania wote na ilikuwa ni ya pili duniani kwa kuwa na watu wengi wenye minyoo bapa. Kwa upande wa mifugo imeripotiwa kuwa takribani ngombe milioni 165 hupata ugonjwa huu duniani kote kila mwaka.

Kwa maelezo zaidi, dalili na jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Hi. jana nilienda hospital niliona dalili ambazo hazikunipendeza na nizakuogopesha maana sikuwahi ziona. nikiwa napata haja ndogo mwishoni inamalizika na damu. je hiyo ni moja ya dalili zakichocho?

Asante
 
leo nmeamka asubuh naenda kukoajoa nkaona dam mwishon na mpka sasa nkikojoa maumivu makal ..tatizo n nn na nfanyaje
 
leo nmeamka asubuh naenda kukoajoa nkaona dam mwishon na mpka sasa nkikojoa maumivu makal ..tatizo n nn na nfanyaje
Ndugu pole sana kwa kutokwa na damu wakati unakojoa ni Dalili ya Ugonjwa wa kichocho nenda Hospitali kamuone Daktari haraka iwezekanavyo upate kutibiwa.

KICHOCHO (Biliharzia) NI UGONJWA HATARI

unnamed+(33).jpg

Aina za Konokono wanaoambukiza Kichocho na wale wasio ambukiza.
Sehemu wanaopenda kukaa Konokono

Namna ya uambukizwaji

Kichocho ni ugonjwa usababishwao na vijidudu ambavyo mtu hupata anapotumia maji yaliyo na vijidudu vya ugonjwa huu hashwa katika nchi za kitropiki. Bilirhazia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Viini vilivyokomaa huishi katika mishipa katika kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa.

Mayai yanapokuta maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi, ambao hupenya konokono hawa wa majini. Katika konokono hawa wa majini viluwiluwi huwa hukua na kuongezeka na kutoka. Viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya kwenye ngozi na wakisha penya huingia hadi kwenye mishipa ya Ini ambapo hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu na haja kubwa.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka mitatu na nusu lakini huweza kuwa zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpaka na kibofu husababisha athari kubwa. Maambukizi yasiyotibiwa husababisha matatizo ya Ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Wakati mwingine mayai huingia katika uti wa mgongo au mara nyingine katika ubongo.

Jinsi ya kujizuia

Inasemekana hakuna chanjo iliyopatikana. Katika nchi ambazo ugonjwa huu upo, inadidi kujitahidi kuepuka maji ambayo si Safi na salama. Usidhani ya kuwa maji yoyote ni safi na salama katika sehemu zenye ugonjwa huu. Kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea, hizi ndizo sehemu za hatari.

Fukwe za bahari na fukwe zilizo na mawimbi si rahisi kuwa na konokono wa majini, hivyo hizi sehemu zinaweza kuwa salama. Viluwiluwi huweza kuishi kwa masaa 48 baada ya kutoka kwa konokono na huweza kusafiri mwendo mrefu, kwa sababu hii maeneo yenye maji katika sehemu zenye ugonjwa huu hayawezi kuwa salama kabisa.

Maziwa katika nchi ya Tanzania na Malawi yana vimelea vya kichocho, lakini fukwe nyingi karibu na mahoteli ya kitalii yana uoto mdogo wa mimea hivyo huwa ni sehemu ambazo si rahisi kupata ugonjwa huu.
Mabwawa ya kuogele ni salama kama yana dawa ya klorini (chlorine) na hakuna konokono wa majini.
Bahari ni salama
Maji ambayo yamatuama kwa siku tatu ni salama endapo hakuna konokono wa majini.Maji ya kuoga yanayochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mito na maziwa yanaweza kusabaisha maambukizi.

Namna ya kujikinga na kichocho

Kama unapopalilia, vaa mabuti marefu ya mpira. Viluwiluwi hawa hufa haraka mara tu wanapokuwa nje ya maji na hawawezi kuepuka kifo. Nguo na ngozi zenye maji zikikaushwa kwa haraka husaidia kujikinga na maambukizo.

Dalili za maambukizi
Wasafiri wengi walioambukizwa huwa hawaonyeshi dalili yeyote ya ugonjwa huu
Kunakuwa na mwasho katika sehemu alipoingilia kimelea kama "mwasho wa muogeleaji".Unapata homa baada ya wiki nne baada ya kutumia maji yaliyoambukizwa. Unapatwa na kikohozi kikavu ndiyo dalili ya hatua hii ya maambukizo. Kupungua kwa uzito na kujihisi kuchoka. Damu katika mkojo na haja kubwa kama ugonjwa umekomaa. Na pia kuvimba kwa miguu. Na muda wa kuambukizwa huchukua wiki nne (4) kwa mayai kuonekana katika choo na kuonekana kwenye mkojo. Lakini hata hivyo ikishajua tu umetumia maji yenye vimelea basi inabidi uchunguzi ufanyike miezi mitatu baada ya kutumia.

Tiba ya kichocho
Kichocho hutibiwa na madawa maalumu dhidi ya vimelea hivi ambazo hupatikana katika kliniki na hospitali yoyote ile iliyo karibu na makazi yako. Ni vizuri kupima mara kwa mara unapopatwa na mashaka ya kuambukizwa na kichocho hasa baada ya kutumia maji yenye vimelea vya kichoccho
 
kwani kasema anatokwa na damu wakati wa kukojoa au just maumivu wakati wa kukojoa?@mzizimkavu
 
Kama alivyo shauri MziziMkavu, nenda hospital kwani pia yaweza kuwa ni maambukizi(infections) kwenye njia ya mkojo au hata kwenye tezi dume (prostate gland) hivyo kuifanya njia ya mkojo kuwa nyembamba sana au tezi dume kuvimba na kusababisha mlango wa kibofu cha mkojo kuwa mwembamba, yote hayo husababisha mkojo kutoka Kwa shida na hata kuchana kuta za njia ya mkojo and thus matone ya damu kuonekana
 
Back
Top Bottom