Ujue ubakaji na adhabu zake kulingana na Sheria ya Tanzania

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
May 26, 2018
1,114
958
Nimeshawishika kuandika bandiko hili baada ya kuona umuhimu wa kuwaepusha watu na vitendo ambavyo vinaonekana ni vya kawaida tu lakini kusema kweli vinaweza kukuingiza katika hatia ya UBAKAJI.

Nilisikia mtu mmoja anasema anaingiza kichwa tu! Hata kichwa tu kinatosha kuwa ubakaji.

Ujue ubakaji (rape) na adhabu yake


The penal code cap 16 of the laws in Tanzania r. E 2002. Section 130 (2);


"Mtu mwanamume atafanya uhalifu wa ubakaji kama ataingiliana kingono na msichana au mwanamke katika mazingira yafuatayo;


(a) Kama sio mke wake, au kama ni mkewe na wameachana, na hakuridhia kufanya mapenzi kwa wakati huo.


(b) Kwa ridhaa ya mwanamke ambapo ridhaa hiyo imetokana na matumizi ya nguvu, vitisho vya kifo au kuumizwa, au wakati mwanamke huyo amewekwa chini ya ulinzi.


(c) Kwa ridhaa ya mwanamke ambapo ridhaa hiyo ilitolewa wakati mwanamke huyo alipokuwa na matatizo ya akili, au alipewa vilevi vya aina yoyote na mwanamume husika au mtu mwingine, isipokuwa tu kama itathibitishwa kulikuwa na makubaliano ya awali ya kufanya ngono kabla ya kupewa vilevi hivyo.


(d) Kwa ridhaa ya mwanamke ambapo mwanamke alidanganywa kuwa mwanaume huyo ni mume wake kumbe sivyo.


(e) Kwa ridhaa ya mwanamke ambapo msichana au mwanamke huyo ana umri chini ya miaka kumi na nane, isipokuwa tu kama msichana huyo ana umri wa miaka kumi na tano kwenda juu, na wameoana kihalali, na hawajaachana.


(3) Mtu yeyote;


(a) Mwenye mamlaka, na akayatumia mamlaka yake kumbaka, au kumkamata na kumbaka mwanamke au msichana,


(b) Ambaye ni msimamizi, au mfanyakazi katika rumande au jela iliyoanzishwa kisheria, au katika kambi ya wanawake au wasichana, akatumia mamlaka yake kumbaka mwanamke au msichana katika jela, kambi, au rumande hiyo,


(c) Ambaye ni msimamizi au mfanyakazi katika hospitali, akatumia nafasi hiyo kumbaka msichana au mwanamke;


(d) Kama ni mganga wa kienyeji na akatumia nafasi hiyo kumbaka mwanamke au msichana ambaye ni mteja wake kwa malengo ya kumtibu."


(e) Ambaye ni kiongozi wa dini, akatumia nafasi hiyo kumbaka msichana au mwanamke,


4) Kwa malengo ya kuthibitisha ubakaji;


(a) Muingiliano hata uwe mdogo kiasi gani, unatosha kuwa ubakaji.


(b) Sio lazima pawepo na ushahidi wa mikwaruzo, michubuko ya mwili ili kuthibitisha ubakaji.


131(2) Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini;


(a) Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu.


(b) Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya pili, atapewa adhabu ya kifungo cha miezi kumi na mbili pamoja na adhabu ya viboko.


(c) Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya tatu na amekuwa mbakaji sugu, atapewa adhabu ya kifungo cha maisha.


131 a (1) Ubakaji unapofanywa na kundi la watu (mtungo), kila mshiriki aliyefanya au kusaidia kufanyika kwa ubakaji atahesabika amefanya ubakaji.


(2) Kila aliyeshiriki ubakaji wa kundi (mtungo) atapewa adhabu ya kifungo cha maisha bila kujali uhusika wake wa ushiriki katika ubakaji.


132 (2) Mtu atahesabika amefanya jaribio la kutaka kubaka, kama atafanya yafuatayo ;


(a) Atamtisha mwanamke au msichana kwa malengo ya kutaka kumuingilia.


(b) Kama atatumia mamlaka yake kumtisha mwanamke ili amuingilie.


(c) Kama atamlaghai kwa namna yoyote.


(d) Kama atajifanya ni mume wa mwanamke huyo.


Mtu yeyote anayefanya jaribio la kutaka kubaka atapewa adhabu ya kifungo cha maisha au katika hali yoyote kifungo kisichopungua miaka kumi.
 
Hiyo ya 3(b), itabidi Lulu amshtaki mtu kwamba alibakwa, mana ckumbuki kuambiwa alienda jela mjamzito, ila nkaambiwa katolewa sababu ni mjamzito! (kuna mamlaka zilijua kuwa dogo kabakwa mpaka kapata mimba!)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya 3(b), itabidi Lulu amshtaki mtu kwamba alibakwa, mana ckumbuki kuambiwa alienda jela mjamzito, ila nkaambiwa katolewa sababu ni mjamzito! (kuna mamlaka zilijua kuwa dogo kabakwa mpaka kapata mimba!)

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana, lakini sio lazima awe amebakwa. Huenda palikuwepo na maridhiano yasiyo na undue influence au pressure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ikutokea mwanamke kaniwekea bastora kichwani lazima nimtafune huo si ubakaji? nilifikiri linapo fanyika bila ridhaa ndio ubakaji kwa maelezo ya hapo juu
Mkuu ridhaa inayozungumzwa hapa sio kusema NDIO AU HAPANA.

Ukisema hapana halafu UKASIMAMISHA basi concept nzima ya ridhaa inakufa.

Mwanaume kubakwa ni jambo lisilowezekana kimantiki, kibaiyolojia, na kisaikolojia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Regnatus Cletus ,
1. Hivi kwanini sasa ushahidi wa mtoto mdogo aliyebakwa hata kama uko uncorraborated unachukuliwa kama ulivyo tu, endapo mahakama inaamini kwamba huyo mtoto anasema ukweli ???


2. Hivi unadhani kwamba siyo muda muafaka wa kubadilisha sheria za nchi na kukubali ukweli kwamba mwanaume anaweza kubakwa na mwanamke ???
 
Back
Top Bottom