Uchaguzi 2020 Ujue Muundo na Mamlaka ya Kamati na kamati ya Rufaa ya Maadili ya Uchaguzi

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
Kwa mujibu wa GAZETI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA la Tarehe 5 Juni, 2020 SEHEMU YA TANO Ukururasa wa 14. Angalia Kiambatisho.



5.2.2 Kamati ya Kitaifa
Itakuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamiko ya ukiukwaji wa maadili kwenye uchaguzi wa Rais na Rufaa
kutoka Kamati ya Jimbo. Kamati hii itaundwa na-
(a) mjumbe mmoja wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;
(b) mwakilishi mmoja kutoka kila chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi wa Rais. Aidha, mwakilishi
huyo atapaswa kuwasilisha kwa Mwenyekiti wa Kamati barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu
wa chama husika; na
(c) mjumbe mmoja atakayewakilisha Serikali atakayeteuliwa kwa maandishi kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu; na
(d) Katibu na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kutoka miongoni mwa Maafisa
waandamizi wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wakati wa kikao cha kamati, Katibu au Katibu Msaidizi atachukua muhtasari wa kikao na atawajibika
kutunza kumbukumbu za vikao.





5.2.1 Kamati ya Rufaa
Itakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa kutoka Kamati ya Kitaifa na itaundwa na-
(a) Mwenyekiti ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
(c) mjumbe mmoja kutoka kila chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi wa Rais ambaye ni Mwenyekiti
au Katibu Mkuu au mwakilishi wa chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi wa Rais;
(d) mjumbe mmoja atakayeiwakilisha Serikali ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu au
mwakilishi wake; na
(e) Katibu wa Kamati ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi au mwakilishi wake na Katibu Msaidizi wa
Kamati ambaye ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wakati wa kikao cha kamati, Katibu au Katibu Msaidizi atachukua muhtasari wa kikao na atawajibika
kutunza kumbukumbu za vikao.
 

Attachments

  • GAZETI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.pdf
    4.4 MB · Views: 12
Mkurugenzi wa tume hastahili kuwa mjumbe maana tayari ameshatoa hukumu kwa mtuhumiwa.
Kwa kuwa inaonekana, (kwa suala la Lisu) tume ndiye mlalamikaji, basi mjumbe yeyote kutoka tume hastahili kuwemo kwenye kamati maana huwezi kuleta tuhuma halafu ukawa mshiriki wa kutoa maamuzi - its obvious utapendelea upande wako

Mkuu ukisoma kanuni inaonekana anaruhusiwa kutoa tuhuma, ila tuhuma anapaswa kuzipeleka kamati ya maadili, then kamati ikijiridhisha ndipo inaweza sasa kumuita mtuhumiwa.
 
Sasa nimeanza kuamini aliyekurupuka aitwe ni Polepole bila wao wenyewe tume kuona uzito wa kuita mtu kwa issu zinazoweza kuwa solved hata kwa barua tu.
 
Kwanza haikuwa sahihi mkurugenzi wa tume kumwambia Lissu anatakiwa kwenye kamati badala yake mkurugenzi alitakiwa kuandika malamiko yake na kuyapeleka kwa Tume na tume ikijiridhisha na uvunjifu wa kanuni ndipo imwandikie mlalamikiwa
 
Mkurugenzi wa tume hastahili kuwa mjumbe maana tayari ameshatoa hukumu kwa mtuhumiwa.
Kwa kuwa inaonekana, (kwa suala la Lisu) tume ndiye mlalamikaji, basi mjumbe yeyote kutoka tume hastahili kuwemo kwenye kamati maana huwezi kuleta tuhuma halafu ukawa mshiriki wa kutoa maamuzi - its obvious utapendelea upande wako

Ondoa shaka na wasiwasi, mchakato wake ni mrefu na mgumu sana....

Kuna maeneo (watoa tuhuma - NEC) wanajifunga mwenyewe na bahati mbaya sana hawafuati taratibu za kikanuni katika kuandaa na kuwasilisha tuhuma zao kwa muhusika....

Dr Wilson Charles Mahera, Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hana lolote, anaonekana wazi ni kilema wa sheria. Haijui sheria lakini anasimamia taasisi inayohitaji awe na weledi kiasi wa sheria. Huyu hawezi kufanya lolote nje ya utaratibu wa kikanuni mpaka sasa....

Huyo ni msaidizi wa Humphrey Polepole katibu mwenezi na itikadi wa CCM. Anafanya kazi ya CCM kwa mwavuli wa NEC....

Kwa hiyo bwana Mahera absolutely 100% anapiga siasa tu....

Anajaribu kumtisha tu mgombea wa CHADEMA nje ya sheria na kanuni...

Ni afadhali angemtishia kwa risasi au bunduki lakini kwa sheria na kanuni amefeli spectacularly....!!

Anamsaidia mgombea wa CCM kupiga kampeni tu huyo. Nothing less, nothing more....
 
Naomba kujuzwa kati ya mwenyekit wa tume na mkurugenz wa tume ya uchaguzi nani ni mkubwa sio kiumri kwa madaraka na pia majukumu yao nj yap???
.
Natanguliza shukarani

Muundo wa Taasisi
UUNDO WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


Tume inaundwa na Wajumbe saba (7), miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na

Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au

Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni

mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu

anayetoka sehemu ya pili ya Muungano. Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2)

ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Kifungu cha

4(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.



Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka miongoni mwa Wanachama wa Chama cha

Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) na Wajumbe wengine

wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia na

kuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri

ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume.

Tume ina jumla ya Wajumbe saba (7), hata hivyo kwa sasa mjumbe mmoja

amemaliza muda wake na hivyo kubakiwa na wajumbe sita (6) kama inavyoonesha

hapa chini:-



Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Na. Jina Wadhifa


1. Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage, Mwenyekiti

2. Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk, Makamu Mweyekiti

3. Mhe. Jaji (Mst.) Mary H.C.S Longway, Mjumbe

4. Mhe. Asina A. Omari, Mjumbe

5. Mhe. Jaji (Mst) Thomas Mihayo, Mjumbe

6. Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri, Mjumbe



Wajumbe wa Tume hukaa Madarakani kwa kipindi cha miaka mitano tangu

kuteuliwa kwao, lakini Rais anaweza kuwateua tena kwa kipindi kingine kadri

atakavyoona inafaa.

Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume husaidiwa na Sekretarieti

inayoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na Katibu

wa Tume. Kwa sasa Mkurugenzi wa Uchaguzi ni Dkt. Wilson Mahera Charles.

Aidha, Tume ina Idara 5 na Vitengo 4 vinayoongozwa na Naibu Katibu na

Wakurugenzi kama ifuatavyo:-

(i) Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu;

(ii) Idara ya Mipango;

(iii) Idara ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura;

(iv) Idara ya Uendeshaji Uchaguzi;

(v) Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura;

(vi) Kitengo cha Fedha na Uhasibu;

(vii) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;

(viii) Kitengo cha Huduma za Sheria; na

(ix) Kitengo cha Ununuzi, Ugavi na Lojistiki.
 
Back
Top Bottom