Zijue faida za Mmea wa Mlonge, Jitibu magonjwa 300 kwa kutumia mlonge

Si lazima utafune yale majani. Chuma yatupie kwenye mboga inapoungwa taste haibadiliki. Ila isichemke sana.
Hii ni thread educative, hongera sana.These are the kind of threads one would like to read,sio thread za kijinga jinga tu.Okay,ninayo Milongelonge shambani kwangu.Lakini taste ya mbegu zake au unga wake mm,inahitaji moyo.Sijawahi kula majani yake kama mboga,lakini nasikia nayo ni extremely nutritious.Kwa wale wanaoweza kula unga wake while mixed with warm water,nasikia ni dawa nzuri ya kisukari pia.
 
Jamani mimi hata sijui huu mti unafananaje, naweza kuuita ni mti wa maajabu
 
Naweza kupata huo mti kwa hawa wauza miti na maua? Naomba picha ya huo mti plz ili na mimi nikapande kwa nyumba yangu

Hii ni thread educative, hongera sana.These are the kind of threads one would like to read,sio thread za kijinga jinga tu.Okay,ninayo Milongelonge shambani kwangu.

Lakini taste ya mbegu zake au unga wake mm, inahitaji moyo.Sijawahi kula majani yake kama mboga,lakini nasikia nayo ni extremely nutritious.Kwa wale wanaoweza kula unga wake while mixed with warm water,nasikia ni dawa nzuri ya kisukari pia.
 
Duh! Yaani pamoja na sifa zote hizo lakini bado wala sifahamu huo mti unafananaje!! Kwa wakazi wa dar, je kuna mtu anaweza kunijuza unapatikana sehemu zipi ili angalau nikauone ulivyo?!

Nenda pale makumbusho ndani ya zile nyumba za makabila ya Tanzania kuna watu watakuonesha Mlonge ulivyo!!
 
Duh! Yaani pamoja na sifa zote hizo lakini bado wala sifahamu huo mti unafananaje!! Kwa wakazi wa dar, je kuna mtu anaweza kunijuza unapatikana sehemu zipi ili angalau nikauone ulivyo?!

Kama unakaa Dar Es Salaam, pale Ocean Road karibu na ofisi za MKURABITA upo mti wake ni mkubwa tu, pitia siku moja utauona. Ukikata tawi na kupanda hasa wakati huu wa mvua hapa Dar Es Salaam utaota tu

Nyati
 
MLONGE
Unga wa majani ya Mlonge ambao ni lishe, tiba na kinga hutibu magonjwa kama shinikizo la damu, kupooza viungo au kufa ganzi, homa ya matumbo(typhoid), kuwashwa mwili,vidonda vya tumbo, malaria sugu, enia, upele n.k.
Mbegu za Mlonge hutibu Malaria, Saratani ya tumbo, hupungusa sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji,huongeza kinga ya mwili CD4s. (Tumia mbegu 3x3 muhimu kila ukitafuna mbegu tatu kumbuka kutumia maji glass 3 au zaidi).

Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment).

Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku.

Dozi ya Ukimwi. Dozi ya ukimwi ni kutumia unga wa majani kijiko cha chai mara tatu kutwa kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita. Pia mgonjwa anatakiwa kutafuna mbegu tatu mara tatu kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita.

Unahamasishwa na kushauriwa angalao nyumbani kwako uwe na mashina kadhaa ya mmea huu kwa matumizi yako.


Tuwe makini na hapo kwenye RED. Kwani siamini, na ingekuwa vizuri tusiwadanganye wenzetu
 
Tuwe makini na hapo kwenye RED. Kwani siamini, na ingekuwa vizuri tusiwadanganye wenzetu
Ni kweli , Mlonge hautibu UKIMWI...unachofanya mlonge ni kuimarisha afya ikiwamo kuongeza nguvu ya kujikinga na maradhi(cd4 n.k)...Hii ningependa kuona hata kwenye vikopo vya unga wanavyouza ikisisitizwa kuwa Mlonge siyo tiba ya Ukimwi ila inaweza ikampa unafuu mgonjwa wa ukimwi kutokana na virutubisho vyake.
 
Swali wakuu je?? Mti huu unaweza kuota sehemu ya baridi mfano nikipanda mkoa wa iringa huko njombe unaweza kuota??

Niliwahi msikia mtaalam 1 wa tiba asili dr ndode akidai kuwa huu mti ndio ule mti ulioandikwa kwenye bible kua ulitumika kutibu maji je ni kweli?
 
Swali wakuu je?? Mti huu unaweza kuota sehemu ya baridi mfano nikipanda mkoa wa iringa huko njombe unaweza kuota??

Niliwahi msikia mtaalam 1 wa tiba asili dr ndode akidai kuwa huu mti ndio ule mti ulioandikwa kwenye bible kua ulitumika kutibu maji je ni kweli?
Mkuu hapo inabidi utafute mbegu zake na ujaribu kuzipanda huko Njombe...nijuavyo mimi ni mti unaohimili sana kukua vizuri kwenye mazingira ya joto(tropics).
Kuhusu kutibu maji sijakuelewa....nijuavyo mimi ni kwamba mbegu za mti huu zilizokomaa zikisagwa , zinaweza kuwekwa kwenye maji yaliyochanganyika na uchafu na baada ya muda uchafu huo hujitenga na maji.
*************
In addition to their usefulness as a source of oil, moringa seeds can be used for water treatment (Fig. 11). Dr. Samia Jahn, a German woman who for many years worked for the Deutsche Gesellschaft für
Technische Zusammenarbeit (GTZ), told ECHO how to use moringa seeds to clarify water. Suspensions of ground seed of the moringa tree are used as primary coagulants. They can "clarify Nile water of any degree of visible turbidity." At high turbidities their action was almost as fast as that of alum, but at medium and low turbidities it was slower. The doses required did not exceed 250 mg/l. Coagulating the solid matter in water so that it can be easily removed will also remove a good portion of the suspended bacteria. Jahn wrote that river water is always polluted with human waste. At GTZ's sampling site, the total coliform bacteria count during the flood season was 1,600-18,000 per 100 ml. After one hour of treatment with moringa seed powder, the coliform count was 1-200 per 100 ml. According to Jahn, "Good clarification is obtained if a small cloth bag filled with the powdered seeds of the moringa is swirled round in the turbid water."
Fig 11. A comparison of non-treated (jar on left) vs. moringa-seed-treated (jar on right) pond water. Photo by Beth Doerr.
To prepare the seed for use as a coagulant, remove the seed coats including the "wings." The white kernel is then crushed to a powder using a mortar or by placing in a cloth on top of a stone and crushing. Two heaping teaspoons or two grams of the powder should be mixed with a cup of clean water in a bottle (e.g. a soda bottle). The water and moringa kernel powder should be shaken for five minutes to form a paste. This paste is then poured through a cloth strainer into 20 liters of the water to be purified. The water is stirred rapidly for two minutes, and then slowly for 10-15 minutes. Leave the bucket of water undisturbed for at least an hour. Impurities will then sink to the bottom. The water should be strained again into a storage container for use. This process removes 90-99% of impurities. If there is a possibility of disease in the water, it can be purified by chlorine, boiling or solarizing (placing in the direct sun in a clear bottle for two hours).
clip_image002.jpg
 
Mimi nimeupanda nyumbani. Huwa natumia kama ifuatavyo: kutibu malaria natafuna mbegu 8x8x5 na kunywa maji lita 1.5, vijiko viwili vya chai vya unga wa mlonge kwenye uji wa ulezi kwa matumizi ya mwanangu, natafuna majani mateke kuondoa stress, uchovu na kupata virutubisho
 
Ukitafuna mbegu zake na ukanywa maji huna haja ya juice maana muda wote kinywa kina sukari ya ajabu. Watu wasiogope kutafuna ni tamu unapokunywa na maji unaweza kukata lita 5 kwa sababu muda wote utajisikia kunywa maji kutokana na utamu ulio kinywani. Tiba inawafaa watu wasiopenda kunywa maji kwa kuwa itamlazimu kunywa.
 
Duh! Yaani pamoja na sifa zote hizo lakini bado wala sifahamu huo mti unafananaje!! Kwa wakazi wa dar, je kuna mtu anaweza kunijuza unapatikana sehemu zipi ili angalau nikauone ulivyo?!

That's marvellous, kwa waliopo Dar, tembelea eneo lenye bar nyingi sana Dar pale Banana, karibu kabisa na kwa Mamaseles na Chacha. Utauona mlonge majani na mbegu zake, hata mimi niliudharau, kumbe ni mali sana, sasa nitaupanda kwangu, tena kijitawi tu kinatosha. Tunakushukuru Mkuu.
 
Duh! Yaani pamoja na sifa zote hizo lakini bado wala sifahamu huo mti unafananaje!! Kwa wakazi wa dar, je kuna mtu anaweza kunijuza unapatikana sehemu zipi ili angalau nikauone ulivyo?!

Utaipata kwenye bustani za jiji, Magomeni nyuma ya kituo cha daladala zinazokwenda Kariakoo, au bustani ya city karibu na hospitali ya Ocean Road mbegu zipo chini zimeanguka, wakazi wengi wa Bunju hutumia mti wa mlonge kama fensi ya kuzunguka nyumba zao.

Kama upo upanga nenda karibu na Muhimbili primary school hapo kuna makaburi ndani yake miti ya milonge ipo mingi sana chuma mbegu zilizokauka ukapande.
 
Nawasalimu wana JF. Mimi nilipanda miti ya mlonge kutokana na ushauri juu ya mmea huu. Bahati nzuri miti imestawi vizuri na kutoa mbegu nyingi. Sasa najiuliza mbegu na majani nivitumie vipi kwa afya? Je, naweza kutafuna mbegu zikiwa kavu? Je nitafuna mbegu za mlonge kuna faida/hasara gani? Je, naweza kutafuna majani mabichi ya mlonge? Kufanya hivyo kuna faida na hasara gani? Je naweza kuchemsha majani au mbegu za mlonge na kunywa? kuna faida au hasara gani? Nawaombe mnisaidie. Asante sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom