Ujue mbuyu wenye miaka zaidi ya 500, unaoweza kubadili jinsia

Imani ya hovyo, haiwezekani kubadilika jinsia

Hilo la umri wa 500 inawezekana.
 
Watu walikua na Imani kwamba ukienda kuhiji Kama umeua watu wengi hurudi.
Idd Amin alikua ALHAJ
 
Hiyo ya umri inatajwatajwa sana... hii ya kubadili jinsia ni fresh new kutoka kwako
 
Wakati wazungu wanatumia karibu Sh Mil 50 kubadili jinsia zao, huko bagamoyo gharama yake ni kuzungumka tu mbuyu.

Kweli imani ni kifungo kibaya zaidi ya gereza.
 
Mimi na Crew yangu tulifika hilo eneo tukapata habari zake, tukauzunguka mti huo mara 7, ilikua for fun hakuna mtu aliweka imani ya kinachoelezwa,

Pia kuna kisima hapo hapo Kaole wanasema kipo tangu karne ya mbali huko hakikauki maji pia hakina chumvi licha ya kua karibu na bahari, watu wana nawa na wengine wanakunywa maji yake kwa ajili ya kupata baraka.
Kile kisima kilichimbwa Kama choo Cha kukaa ndio maana hakiwezi kukauka kamwe. Ni Kama unavyoflash maji halafu yanaendelea kuwepo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom