Ujuaji wa CHADEMA wawafanya wawe vipofu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujuaji wa CHADEMA wawafanya wawe vipofu !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, Feb 10, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baada ya Bunge la JMT kutoa tafsiri ya maana ya ‘Kambi ya upinzani bungeni’ ambapo lengo lake kuu lilikuwa ni kujali maslahi ya kitaifa zaidi na si ubinafsi wa watu wachache wenye uchu na uroho wa madaraka. Kamati mbali mbali za bunge jana zilifanya chaguzi zao za viongozi wa kamati hizo, ambapo CDM walipata kamati moja , UDP kamati moja na TLP kamati moja. Hili kwa kweli laonyesha ni mwanzo mzuri kwa wapinzani kuimarisha kambi yao, na si chama kimoja kuhodhi/kupora madaraka ya kambi nzima.
  Kwa maana hiyo basi, CDM sasa wanauwezo wa kuchagua kutoka kambi yao tu mawaziri vivuli au kuchagua kutoka vyama vingine pia, kwa mie naona mawaziri vivuli ni kama wabunge wa viti maalum tu. Yale macho (kuongoza oversight committees zote 3) ambayo CDM walitegemea kuyapata hawana tena, hivyo basi watakuwa watazamaji zaidi kuliko watekelezaji zaidi.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  CUF wanaongoza kamati ipi .....?
   
 3. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Fikiria tena mara ya pili kama jina lako lilivyo
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Si lazima CUF waongoze, kwani kamati zenyewe ni chache, mgawanyo huo hapo juu ndio upo sawa, kuliko chama kimoja tu kung'ang'ania na kutoka nje ya bunge ili wapate madaraka hayo. Tunalipongeza bunge kwa kuona mbali na kujali maslahi , umoja na mshikamano wa kitaifa zaidi
   
 5. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ....mfinyu wa mawazo!
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CHADEMA wekeni mbele maslahi ya kitaifa kuliko utashi wa nafsi zenu wa uchu na uroho wa madaraka, huo ndio ukweli
   
 7. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ThinkTwice Bro............. soma historia ya maana ya Kambi Rasmi halafu fikiria mara mbili kwa kilichotokea na what CHADEMA anachosimamia na kulilia on the same line.... sio kuropoka tu...............
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni mtazamo wako ila ukweli ndio huo, CHADEMA yageuka kuwa wabunge wa viti maalum , yote hayo ni ubishi na kiburi chenu, na watanzania wameisha wajua kuwa nyie nia yenu si kuwakomboa wananchi kama mnavyo jinasibu bali ni kuwakandamiza watanzania kwa kujinufaisha binafsi
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa nini CHADEMA hawataki ushirikiano ? hapo ndipo watanzania hawawaelewi CHADEMA
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  CUF wameshirikiana na chama gani zanzibar...?
   
 11. P

  Pokola JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Unamaanisha WEWE na nani? Au ni Watanzania wanaoishi Ufarisayoni? Umefanya utafiti gani hadi kubaini hisia za hao watanzania unaowataja hapa? Mfarisayo!!!
   
 12. i

  ibange JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  usiwe kama dodoki unameza kila kitu kinachosemwa na ccm. chadema walikuwa na haki ila ccm wanasema ni wabinafsi. kama ccm si wabinafsi kwanini wasiwape uwaziri watu wa vyama vingine?
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Naomba kuuliza CUF katika hizo kamati hawajapata mwenyekiti? kama itakuwa vita yote ile ni kwa ajili ya vyama vidogo vya upinzania basi nawapongeza sana CUF kwa hilo. Ifike wakati kwa CDM kujenga vyama vidogo vya upinzani kama walivyojengwa wao ndani ya bunge. Labda tuwe wachoyo wa fadhila au wepesi wa kusahau hawa CUF wanaoonekana wabaya ndio waliofanikisha kina Slaa kuwika ndani ya bunge kupitia hizi kamati. Mtakumbuka kuwa CUF haikuongoza hata kamati moja kati ya zile tatu ambazo mbili walipewa CDM na Slaa na Zitto kuziongoza na moja walipewa UDP ikaongozwa na Cheyo. Ingekuwa CUF wanataka uongozi au ni waroho wa posho wasingeziachia hizi kamati! na kwa ninavyosoma comments za wengi watu hapa inaonesha kuwa CUF wanaelewana sana na CCM kama CUF wangekuwa hawaangalii maslahi ya taifa nina imani wangetumia fursa hii kuzichukua na kuzihodhi kamati zote tatu kwa maana CCM wasingewatosa! Ila ninachokiona ni kinyume chake.

  Huu ni mtazamo wangu tu..................
   
 14. O

  Omumura JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hamad Rashid a.k.a. mfarisayo!kamati ya maendeleo ya jamii!
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Wewe ulitaka CHADEMA tufanye nini? Tukenue meno au?
   
 16. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa zanzibar kwenye baraza la wawakilishi kuna vyama viwili tu CCM na CUF , sasa waungane na nani ?
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wekeni maslahi ya kitaifa mbele na acheni ubinafsi , hilo ndilo la kufanya
   
 18. Don Alaba

  Don Alaba Senior Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Cuf imefunga ndoa na ccm, na sasa cuf ni ccm b kwahiyo hatutaki unafiki katika hili, huwezi ukawa rafiki yangu wakati wewe ni chizi wa akili hatutaelewana, kinachotafutwa hapo ni upinzani wa kweli na sio longo longo kama za ngeleja

   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nimemsikia WM kwenye PMQs inayoendelea sasa hivi Bungeni. Naye anajibu kama Makamba.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

  [​IMG]


  22.JPG

  525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

  Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

  Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

  Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

  Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

  Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

  Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

  Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

  Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

  Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

  (1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

  (2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

  (3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

  Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
   
Loading...