"ujisikitie na kujihurumia wewe kwa ubinafsi na njaa yako" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"ujisikitie na kujihurumia wewe kwa ubinafsi na njaa yako"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eistein, Oct 30, 2012.

 1. Eistein

  Eistein JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,107
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "UJISIKITIE NA KUJIHURUMIA WEWE KWA UBINAFSI NA NJAA YAKO"

  Baada ya uchaguzi wa kata 29 kuisha juzi (jumapili) yamesemwa mengi hunu, hasa wengi wakiiraumu CDM kwa kushindwa kuchukua kata nyingi toka mikononi mwa ccm( JESHI LA POLISI, USALAMA WA TAIFA, BARAZA LA MAWAZIRI,RUSHWA,WATENDAJI WA SERIKALI WENYE NYASIFA ZA KISIASA WILAYANI MPAKA KATIKA KATA, GREEN GUARD,) na kadhalika. Vyombo vyoote hivyo na watendaji woote wa serikali wa nafasi za kisiasa wapo hapokuhakikisha ccm inashinda, iwe kwa mauaji, kujeruhi, kuiba kutumia chuki,hira, vitisho na pesa chafu na rushwa ya wazi ya kununua kadi za kupigia kura.

  Lakini wachangiaji wengi tumejikita kuiraumu CDM, kwa kuongeza viti vitatu na siyo vyote 29, sababu zimetolewa nyingi na za msingi sana,(sitaki kuingia huko) leo nina swala moja tu

  NASEMA HIVI "UJISIKITIE NA KUJIHURUMIA WEWE KWA UBINAFSI NA NJAA YAKO" INAYOKUSABABISHA MPAKA LEO UONE HAKUNA HAJA YA KUPIGA KURA,

  1. Unataka viongozi wa CDM waje wakuchukue wewe toka kitandani wakupeleke katika kituo cha kupigia kura wakuonyeshe uchague Mgombea wa CDM?? nauliza hivyo kwa sababu hata katika chaguzi hizi matatizo ya watu kuwa na kadi na kutotaka kwenda kupiga kura yamejitokeza tena kama 2010 (uchaguzi mkuu), JE unataka CDM wafanye nini wakufunge kamba ili ukapige kura??? ndio maana nakwambia Ujisikitie wewe mwenyewe,

  2. Nafasi za kugombea zinatangazwa hutaki kujitokeza, unajificha matokeo yakitoka mabaya unalalamika, kama hutaki kuchukua hatua na kujitoa na kupiga kura unapiga kelele za nini, ni kipi usichokijua kuhusu hali mbaya ya maisha aliyonayo mtanzania wa kipato cha chini, lakini ndiyo huyohuyo unaona hakuna haja ya kupihga kura


  Nitoe mfano mdogo tu kata ya daraja mbili-Arusha mjini kabisa hapo sio kijijini inawatu waliojiandikisha katika daftari la kupiga kura mwaka 2009-2010 zaidi ya 10,000 lakini katika uchaguzi huu wa kata tumeona jumla ya kura zoote zilizo pigwa na kuharibika hazifiki 6000, sasa hapo unataka viongozi wajiuuru kwa lipi ikiwa kampeni zimepigwa na wewe umehudhuria na kadi unayo lakini hukwenda kupiga kura,viongozi wa CDM kwa lipi wao ndio waliokuzuia usiende kupiga kura?

  Mfano mwingine, hapo dar es salaam 2010 zaidi ya wakazi 800,000 walijiandikisha, lakini waliopiga kura 2010 hata laki 400,000 hawakufika na hao ndio wako mjini, wanapata access ya mambo mengi, kama ni magezui tulitegemea yaanzie hapo lakini hakuna kitu, watu wako bize na kujipaka pouda na kupenda starehe na kulalamika tu kama dk rushwa jk, sasa unataka NINI, DHAMANA YA MAISHA YAKO, NA AMANI IKO MIKONI MWAKO. USIMLALMIKIE MTU, JILALALMIKIE MWENYEWE KWA NJAA NA UBINAFSI WAKO.

  Nawaambia tena matatizo yoote haya yaliyopo na yanayozidi kwa kazi hapa Nchini (ukosefu wa ajira, uporaji wa rasilimali zetu waziwazi, mauaji ya raia ya makusudi kwa kutumia vyombo vya dora, ukosefu wa madawa hospitali... etc) yamesabishwa na sisi wenyewe watanzania, huitaji elimu ya darasa la kwanza kujua kama sisi ndio wenye matatizo, kwa sababu tunapopata nafasi ya kufanya maamuzi hatuko tayari kufanya maamuzi badala yake sisi ni wakulalamika tu kama serikali ya dk rushwa(jk)

  Ni wangapi humu mnakadi za kupigia kura na mmejiandikisha lakini hamkupiga kura 2010, hata katika uchaguzi huu wa kata 29, na hata ule wa serikali za mitaa 2014 hamtapiga kura??, sasa hapo nani ni tatizo viongozi wa CDM au wewe, ambaye huitaji mabadiliko... nasema hivi tukiendekeza hizi njaa na ubinafsi kamwe msitarajie mambo kubadilika.. yote tumeyataka wenyewe.. Kila kitu ki[po wazi hasa kwa sisis wa mjini kama ni nchi kuyumba kiuchumi, umaskini kuongezeka, serikali kutochukua hatua mahususi katika maswala muhimu, RUSHWA AMBAYO SASA NDIO SERA/ DIRA KUU YA YA TAIFA LETU KILA MLALA HOI INAMTAFUNA, LAKINI NDIYE HUYOHUYO AMBAYE LEO HAYUKO TAYARI KWENDA KUPIGA KURA, NDIYE HUYO HUYO AMBAYE YUKO TAYARI KUUZA KADI YAKE YA KURA KWA TSH 100,000, AU 150,000( ARUSHA -DARAJA MBILI YAMETOKEA SANA NA KWWINGINEKO) ILI TU APATE MKATE WA LEO, kwa hiyo tatizo si CDM wala CCM, TATIZO NI WEWE NA MIMI, Usilalamike kwa sababu hutaki kubadilika, unakubalina na yanayotokea.


  SASA KWA SABABU TUMEKATAA KUCHUKUA HATUA, KWA SABABU TUNAKUBALIANA NA LOLOTE( MAUAJI, WIZI, RUSHWA YA WAZI, UPORAJI WA RASILIMALI ZETU, UBAGUZI KATIKA ELIMU, MATABAKA YA WALIO NACHO NA WASIO NACHO) TUSILALAMIKE, UNATAKA UONGOZI WA CDM UFANYE NINI, WAKATI NI WEWE MWENYEWE HUYATAKI MABADILIKO, HUTAKI KUPIGA KURA, MAANA YAKE UMEKUBARI HALI ILIVYO.

  "SIKU ZOTE UNAKUWA NA MARAFIKI WA TYPE YAKO WANAONDENA NA TABIA NA HULKA YAKO", HATA VIONGOZI WA SERIKALI NDIO WA TYPE YA WATANZANIA (WAWIVU, HATUTAKI KAZI, HATUTAKI KUJITOA, HATUTAKI KUFIKIRIA, HATUTAKI KUHOJI, HATUNA UCHUNGU NA TAIFA WALA RASILIMALI ZETU, HATUNA UPENDO KWA WENZETU).

  HIVYO BASI TUSILALAMIKE, IKIWA SISI WENYEWE HATUATAKI KUCHUKUA HATUA., TULIYOPANDA 2010 NDIYO TUANAVUNA LEO, KWA SABABU YA UBINAFSI NA NJAA ZETU.

  "Ngumu kumeza".
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh, maneno mazito...
   
 3. m

  malaka JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  We mleta uzi mwenyewe kwanza unakadi ya CDM? Umejiandikisha?
   
 4. Eistein

  Eistein JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,107
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndiyo nimejiandikisha nina kadi ya CDM, na kadi ya kupigia kura ,mwaka 2010 nilipiga kura hapo mji kasoro bahari shule ya msingi mafiga B, kituo no 2.

  CDM No. 0065455 (niichukua SUA-MOROGORO 2007)
  kitambulisho cha kupigia kura *02119232* cha tarehe 17/11/2004


  NI VIZURI NAWEWE UKAFANYA KAMA MIMI!!
   
 5. Eistein

  Eistein JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,107
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  habari ndiyo hiyo mkuu, hakuna kuzunguka sisi wenyewe ndio chanzo cha haya yoote, ungozi tulionao unareflect watz tulivyo kwasababu nao ni part ya jamii yetu
  .
   
 6. Niambieni

  Niambieni JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kushinda kwa idadi ya kura chadema ina na imekuwa ikipata kwa asilimia kubwa sana.

  Lakini fumbuka na kujua ukweli mwingine ya kuwa kupata kura hata kama ni mia kwa mia sio ndio kushidwa na kupata madaraka.

  Kushinda chadema itashinda lakini matokeo yatatoka ya kupikwa na atakayeshinda ni mwingine ambaye ana uwezo mkubwa wa kushika madaraka na sio kushinda kura.

  Hata 2015 ndivyo itakavyo kuwa, hivyo penda usipende haki ni hakuna na usilazimishe kuwa ipo.

  Cha muhimu piga magoti na tumuombe mungu aingilie kati.

  Wanaoshinda wanapata uwezo wa kushinda toka kwa shetani wao, hivyo na sisi ni jukumu letu sio tu kukimbilia kupiga kura pia kumwomba mungu wetu atusaidie kushinda kwa haki.
   
 7. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hongera san nachukua fursa hii kukupongeza.
   
 8. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba mkombozi wa mtumwa ni mtumwa mwenyewe.
  Hakuna jamii iliyowahi kupiga hatua za kimaendeleo kwa kulalamika bila vitendo.Baadhi ya vitendo vina gharama kama komredi alivyokatwa na kitu chenye ncha kali wakati wa vuguvugu la Arumeru,lakini matokeo hata baba mkwe wa Sumari kijana anayaheshimu maana watu walisema kwa kupiga kura, wakazilinda ,na majambazi wa CHICHIEMU wakakimbiana Arumeru Magharibi.
   
Loading...