Ujirani mwema Uswahilini: Ni kweli kwamba hotpot (bakuli) ya jirani haipaswi kurudishwa ikiwa tupu?

Zamani ilikua hata ukienda kuomba moto kwa jirani hususan majiko ya mkaa lazima uendee na mkaa ambao bado haujawashwa ...hii ni early 2000 's
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Nipo ninaandaa makala moja kuhusiana na idara ya Ujasusi ya Israel (MOSSAD) ilivyoweza kutumia mbinu ya mawasiliano ambayo wakati wa vita baridi (COLD WAR) ilikuwa inajulikana sana kama "Numbers station" ili kusafirisha taarifa kutoka nchi za kiarabu (Misri, Lebanon, Syria, Jordan) kwenda Tel Aviv katika vita ile ya siku sita ya mwaka 1967.

Sasa kabla sijaiweka makala hii kule jukwaa la Intelligence, leo ninaomba kuwauliza wamama na wadada waliopo humu JF, hususan wale waliowahi kukaa uswahilini na kuishi yale maisha ya kupakuliana mboga siku kama umepika chakula kile adimu kama vile kuku au maini ya ng'ombe.

Eti ni kweli kwamba hotpot (bakuli) ya jirani haipaswi kurudishwa ikiwa tupu bila chochote kitu?

Huu usemi nilikutana nao jana Jumapili nilipoenda kumtembelea mama yangu mkubwa anayekaa kule Tandale kwa Mtogole huku Dar. Baada ya kunilalamikia sana kwanini siku hizi nimemsusa nikaona isiwe kesi, jana huyo nikapanda daladala kutoka Banana nikaungaunga huuuuuyoooo mpaka Tandale.

Sasa baada ya kupiga story kwa muda kama wa dakika 15 hivi, mtoto wa mama yangu huyo mkubwa akaingia na kumwambia mama yake kuwa mama Halima (huyu ni jirani yao) amesema bakuli la jirani huwa hairudishi ikuwa tupu. Inaonekana kuna kitu kizuri alipakuliwa na jirani yake sasa yeye akarudisha hotpot kama ilivyo.

Mama yangu huyu mkubwa yeye ni mwenyeje wa mkoa wa Mara na hizi taratibu za pwani inaonekana kama vile hajazizoea kwa namna fulani hivi, hivyo mara nyingi anajisahau sana. Baada ya kumuuliza ndio akanipa ufafanuzi kwamba;

"Kama jirani alipika mboga adimu (kuku au maini ya ng'ombe) akaamua kukupakulia katika bakuli au hotpot yake, basi na wewe baada ya siku 2 ukiwa unairudisha ile bakuli basi wekamo chochote kitu ulichopika siku hiyo na sio kuirudisha ikiwa tupu"

Je, huu msemo ni sahihi na una ukweli wowote enyi mama/dada zangu wa humu JF?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO
Hii ni kweli kabisa
 
Si lazima..ila ni utaratibu tu uliowekwa na majirani zetu hasa wa huku uswazi...masaki mbezibeach hakuna hayo
 
Huku Zanzibar mnamo mika ya 88 ilikua tukiteka maji ndoo tunaazima kwa jirani unapewa ndoo tupu ila ukirudisha iwe na maji vyenginevyo kesho unaambiwa ndoo zote zinamaji . nisawa na sasa mtu akuazime gari halafu ww usipite sheli (petrol station) kesho yake hatakosa sababu ya kukukatalia na hatokwambia kua tatizo hukutia hata mafuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom