Nimefanikiwa kutembelea Kigoma mjini, Ujiji na Kigoma Kaskazini kwa lengo la kutembea kama 'mtalii wa ndani'. Niliojinea tokea pale uwanja wa ndege hadi Kigoma mjini; ujiji na kule Kigoma pande za Kaskazini yanatia simanzi. Hali ya mwananchi wa Kigoma haifanani(reflect) kama nchi hii imepata uhuru miongo kadhaa. Reli haina mabadiliko yoyote tangu Jerumani alipoitandaza, Mji umejaa vumbi, umeme wa magilini magilini,. Kweli hawa ndugu zangu wa Kigoma ni kama kisiwa pale linapokuja suala la mgawanyo wa 'keki ya taifa'. Sasa kuna jambo moja ambalo limenitatiza na kunitia simanzi na sijui nimfikishie nani kwani siwezi kulimwaga hapa kwenye 'kuku wengi' [Ashakum! Nimetumia tamathali za semi] mpaka pale wakati muhafaka utakapokuwa umetimia na kupata the 'right person' who can handle this sensitive info.
Kwa mara nyingine tena poleni ndugu zanguni wanaKigoma.
Wasalaam,
Shadow.
Kwa mara nyingine tena poleni ndugu zanguni wanaKigoma.
Wasalaam,
Shadow.