Ujio wa Waziri wa Nishati Dk. Kalemani katika mradi wa umeme Rusumo, waulize NELSAP-CU ziko wapi bilioni 70 (US$ 32 Million) RAP, LADP na ESMP?

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
Mawaziri wa wanaohusika na Nishati wa Tanzania, Burundi Na Rwanda Ijumaa ya Tarehe 6 December 2019 wanatarajia kuzuru mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Mto Rusumo.

Mradi huu unatekelezwa na ubia wa Nchi hizi Tatu kwa Mkopo wa Takribani dola za Marekani Milioni 500 ili kuzalisha 80MW ambazo ni mkopo kutoka Taasisi mbali mbali za fedha zikiweno Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Mradi huu ni mojawapo ya miradi ghali sana Duniani ukilinganisha gharama na kiasi cha umeme utakaozalishwa.

Mradi huu unasimamiwa na Taasisi iitwayo Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program -Coordination Unit (NELSAP-CU).

Taasisi hi indo imekabidhiwa dhamana ya kusimamia masula yote katika mradi huu ikiwemo masuala ya Utaalamu na masula yahusuyo Jamii inayozunguka mradi huu.

Yaani Vijiji vya Rusumo upande wa Tanzania na Rwanda ingawa imekuwa ikilalamikiwa na wakazi maskini wa Eneo la mradi kwa matumizi mabaya ya Fedha za walala hoi wa nchi hizi tatu.

Kumekuwepo na malalamiko makubwa sana kutoka kwa wakazi wa eneo la mradi huu ambao wameathiriwa na uwepo wa mradi huu ambapo Taasisi za Fedha zilizokopesha mradi huu zilitenga takribani dola za Kimarekani milioni 32 (takribani bilioni 67 za Kitanzania) kwa ajili ya kuondoa makazi watu waliopo karibu mradi ambapo ulipuaji wa miamba utakuwa unafanyika (Resettlement Action Plan (RAP).

Na pia Kusaidia Kiuchumi Kaya za Waathirika wa Mradi huu Local Area Development Plan (LADP) pia Kusaidia huduma za Kijamii na Mazingira (Environmental and Social Management Plan (ESMP).

Hadi hivi sasa mabilioni hayo ya fedha yalitengwa kwa ajiri hio yameota mbawa, mana kuna nyumba zilitakiwa zilipwe ili wakazi wake wahame haijafanyika.

Hivyo badala yake baada ya nyumba hizo kupasuka na kudondoka kutokana na milipuko umefanyika ukarabati wa kienyenji wa nyumba hizo tofauti na thamani ya pesa iliyotengwa kwa ajili ya Resettlement Action Plan.

Maagizo ya Serikali ya Tanzania wakati wa Kuanza mradi kupitia kwa Kamishina wa Madini wa Tanzania na Afisa Mkazi wa Madini wa Mkoa wa Kagera yamepuuzwa na hawa NELSAP-CU.

Mojawapo ya nukuu za Barua kutoka maofisa hao wa Serikali zinasema hivi

“ALL BUILDING FALLING WITHIN A PROXIMITY OF 170M FROM THE CENTER OF TUNNEL MUST BE COMPANSATED AND REMOVED” Na

“ALL FAMILIES WITHIN 100 YARDS FROM THE CENTER LINE OF BLASTING TUNNEL SHOULD BE REMOVED SO AS TO ENSURE SAFETY FOR HUMAN SETTLEMENT”

NELSAP-CU, Yako wapi haya mabilioni ya Resettlement Action Plan? Waziri Kalemani tusaidie hilo uendapo Ijumaa hii huko Rusumo.

Kuhusu Uwezeshaji kiuchumi kwa Waathirika wa mradi mpaka hivi sasa waathirika wa mradi walichoambulia ni ufugaji wa Sungura ambapo ukifanya tathimini ya haraka mradi huu wa Sungura hauendani na gharama halisi zilizotengwa kwa ajili ya Local Area Development Plan (LADP).

Maana iliwezekana uwezeshaji mkubwa wa wa kiuchumi kufanyika kupitia Kilimo, Biashara, Uvuvi na Usindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo n.k

NELSAP-CU, Yako wapi haya mabilioni ya Local Area Development Plan (LADP)? Waziri Kalemani tusaidie hilo uendapo Ijumaa hii huko Rusumo.

Kwenye upande wa Huduma za Kijamii ambapo mradi huu ulitengewa fungu nono la kuimarisha huduma za Afya, Elimu, Maji, Barabara n.k, miradi hii yote kwa jamiii imekuwa kama ndoto za Mchana.

Hakuna Kituo cha Afya kilichojengwa, hakuna Shule iliyojengwa, hakuna Barabara iliyojengwa na mradi wa Maji umebaki Mdomoni kama Nchi ya Kusadikika. Wananchi wa Eneo hili wanaendelea kutaabika na huduma za Afya, Maji, Elimu na Barabara.

NELSAP-CU, Yako wapi haya mabilioni ya Environmental and Social Management Plan (ESMP)? Waziri Kalemani tusaidie hilo uendapo Ijumaa hii huko Rusumo.

Nakutakia ziara njema huko Mh. Waziri Kalemani naamini uadilifu wako na uzalendo wako utawaauliza hawa NELSAP-CU kwa niaba ya walala hoi wa nchi hizi 3,

YAKO WAPI HAYA MABILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA (Resettlement Action Plan (RAP) , Local Area Development Plan (LADP) na (Environmental and Social Management Plan (ESMP)?
 
Back
Top Bottom