CORONA: Bila mikakati mipya, Utalii Tanzania huenda ukashindwa kuinuka?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
9,995
34,607
Kuna mambo kadhaa ya kufahamu kwa kina kabla ya kujadili hili.

Kwanza tuukubali ukweli huu kuwa, kusambaa kwa Corona duniani ndio kuliko pelekea kusimama kwa shughuli za utalii hapa Tanzania. Sio mtu, watu au mamlaka fulani iliyoamuru kusitisha shughuli za utalii hapa Tanzania.
Watalii wenyewe na mazingira yanayozunguka utalii ndio yaliyopelekea kusimama kwa utalii hapa Tanzania. Hivyo tusijidanganye kuwa kuna mtu au mamlaka fulani inaweza kuamuru utalii urejee na watalii ghafla wakamiminika kuja nchini.

Pili, utalii ni jambo la ziada&gharama (anasa?) katika maisha ya mtu. Sio jambo la lazima, dharula au kufa na kupona kwa mtalii kuja kufanya utalii hapa Tanzania. Hivyo tusiwe na matumaini ya haraka haraka au kuwa na matumaini makubwa ya kutaka kuona utalii unarejea kama awali. Tujipe muda zaidi, tujipange upya na tuwe na subira.

Tatu, Corona imebadilisha kila kitu duniani kwa muda mfupi sana. Hivyo tukubali au tukatae, mambo hayataweza kurejea tena kama awali, lazima yatabadilika, na kwa vyovyote vile hayawezi kuwa chanya sana kwa upande wetu tulioathiriwa. Tunapaswa kujipanga upya, tena kwa namna tofauti.

Mwisho tunapaswa kufahamu kuwa, kuzorota ghafla kwa shughuli za utalii hapa Tanzania kumeleta hasara kubwa sana, hakuna namna ya kuweza kufidia kirahisi. Wapo ambao wameshafirisika, wengine wamepunguza mitaji yao kwa kuhamisha kwenye biashara zingine. Hivyo sekta nzima kwa sasa imechoka na imezungukwa na woga mwingi.

NINI SASA KIFANYIKE ILI KUREJESHA HALI YA MAMBO KATIKA SEKTA YA UTALII HAPA TANZANIA?

1. Tujikite zaidi kwenye uhalisia wa hali ngumu ya mambo ilivyo kuliko kujikita kwenye taswira tamu ya kisiasa yenye matumaini hewa.

2. Wadau wa utalii wasikilizwe, maoni yao yaheshimiwe na changamoto zao zitatuliwe kwa haraka na mamlaka husika.

3. Serikali ipunguze au kuziondoa kabisa baadhi ya kodi na tozo mbalimbali katika sekta nzima ya utalii. (Kumbuka utalii ndio sekta yenye mnyororo mrefu zaidi wa thamani (chain of value) huku ikiwa sekta mtambuka na yenye kutuingizia pesa nyingi za kigeni, hivyo utalii ni Economic catalyst hata kama serikali itakosa kodi katika sekta ya utalii)

4. Serikali ije na mpango mkakati mpya wa utalii katikati ya janga la Corona. Corona imebadilisha mambo mengi hivyo mipango na mikakati yetu ni vyema ikabadilika kulingana na hayo mabadiliko.

5. Tuimarishe Diplomasia ya kimataifa kwa kulinda ndimi zetu na twende sambamba na ulimwengu unavyotaka. (Vivutio vya utalii sio vitu pekee vinavyoweza kumvutia mtalii kuja Tanzania, mtalii ni mtu sensitive sana na anayependa kulindwa privacy yake na kuheshimiwa utaifa wake, tusije kumtumia mtalii kama ngao ya kuhalalisha siasa zetu, tuheshimu utaifa wake na nchi inayotokea. Zile lugha za kuwaita mabeberu, kuwanyoshea kidole kuwa wao wanatuletea Corona au nchi zao zimeshindwa kudhibiti Corona au wanakimbia Corona kwao, wamekuja kufuata nyungu kwetu nk. tuziepuke kabisa. Pia tusipende sana kuwapiga picha watalii wanapo wasili nchini au katika maeneo ya utalii ili kuziweka kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii. Kifupi kabisa tusimchanganye mtalii na mambo mengine ya kwao au ya kwetu)



Mimi ni mdau katika sekta ya utalii hapa Tanzania, ujio wa Corona duniani umeniathiri sana katika shughuli zangu. Hayo niliyoandika ni maoni yangu kulingana na upeo wangu katika sekta hiyo.
 
Tatizo Watanzania kwa kupiga porojo mtandaoni hawajambo

Rais ameongea, Waziri mwenye dhamana ameongea kumbuka hawa watu wanataarfa nyingi kuliko wewe

Sasa unakuja na utabiri usio na ukweli
 
"kuwanyoshea kidole kuwa wao wanatuletea Corona au nchi zao zimeshindwa kudhibiti Corona au wanakimbia Corona kwao, wamekuja kufuata nyungu kwetu nk. tuziepuke kabisa....

"Pia tusipende sana kuwapiga picha watalii wanapo wasili nchini au katika maeneo ya utalii ili kuziweka kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii. Kifupi kabisa tusimchanganye mtalii na mambo mengine ya kwao au ya kwetu)



Hizo ni point muhimu sana umeongea... Lakini hawatakuelwa...


Cc: mahondaw
 
Si mpaka tuwe na akili? Akili zetu zipo kwenye siasa uchwara na propoganda mfu.sisi tunaweza uongo na progroganda uchwara ili zitupe manufaa ya kisiasa tena ya muda mfupi sana
 
Ifute au iondoe kodi na tozo? Ili ikose mapato kabisa? Mdau wa utalii alafu unatoa wazo kama hili! Hujui mtalii mpaka anakuja Tanzania huwa amejipanga kipesa. Maana wanazunguka karibu Africa nzima.
 
Tatizo Watanzania kwa kupiga porojo mtandaoni hawajambo

Rais ameongea, Waziri mwenye dhamana ameongea kumbuka hawa watu wanataarfa nyingi kuliko wewe

Sasa unakuja na utabiri usio na ukweli


Wewe jamaa una kichwa cha kuku kifaranga😂😂😂😂😂😂
 
Ifute au iondoe kodi na tozo? Ili ikose mapato kabisa? Mdau wa utalii alafu unatoa wazo kama hili! Hujui mtalii mpaka anakuja Tanzania huwa amejipanga kipesa. Maana wanazunguka karibu Africa nzima.
Njoo huku kwenye hii sekta ndio utakuja kuelewa mzigo wa Kodi na hizo tozo unabebwa na nani.

Kwa mfano mtalii mmoja anaweza kutua Tz kwa malengo ya kutumia milioni saba kwa utalii wa siku 10 (Safari tour) akitaka kuzunguka Ngorongoro, Manyara, Serengeti na Zanzibar. Kwa sababu ya uwepo wa Kodi mbali na misururu ya tozo basi gharama inafika mpaka milioni 11. Hivyo anaona isiwe shida, unapunguza trips, anaamua kwenda Safari tour ya siku sita tu akitumia milioni saba, akipita Ngorongoro na Zanzibar na kisha anasepa zake.

Sasa washindani wetu wa utalii (Kenya) wanaweza kumdaka mtalii huyo huyo juu kwa juu kabla ya kutua Tz na kumwambia kwa Milioni Saba hizo hizo watampa Safari tour Kenya yenye package yenye kufanana sana na hiyo ya Tz aliyoshindwa. Wao Safari tour ya siku 10 watampeleka Nairobi, Masai Mara, Malindi, Mombasa nk.

Mambo sio rahisi ndugu.
Game iko tight kinyama.
 
Mbona huwa wanakuja Tanzania? Na utalii ni moja ya chanzo kikubwa cha mapato! Hauna nia nzuri na taifa la Tanzania.
 
Norway na Denmark kutoruhusu wa Swede kuiingia nchi zao. Kumbuka sweden haijatekeleza lockdown. Je nchi za magharibi zitaruhusu raia wao kutalii nchi ambazo hazijatekeleza lockdown hivyo kuwepo na mashaka ya maambukizi makubwa ya covid19 ?
(Norway and Denmark say they will open up tourism between their two countries from 15 June but will maintain restrictions for Swedes.

Sweden did not impose a lockdown, unlike its Nordic neighbours, and its Covid-19 death toll - above 4,000 - is by far the highest in Scandinavia.

Danish PM Mette Frederiksen said Denmark and Sweden were in different places regarding the pandemic.

Denmark is also opening up tourism with Germany and Iceland, within limits.)
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom