Ujio wa viongozi wa nchi za kigeni kuomboleza msiba wa mzee B.W. Mkapa ndio mtihani (challenge) wa kwanza kwa kaka yangu RC wa Dar Aboubakar Kunenge..

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

Ujio wa viongozi wa nchi za kigeni kuomboleza msiba wa baba yetu kipenzi na mzalendo aliyetukuka mzee B.W. Mkapa ndio mtihani (challenge) wa kwanza mkubwa kwa kaka yangu RC wa Dar Aboubakar Kunenge tangia ateuliwe katika nafasi hiyo kubwa kabisa ya uongozi ndani ya jiji hili kuu na mashuhuri kabisa la kibiashara hapa nchini.

Ninafahamu fika ya kuwa hili suala ni la kitaifa zaidi sidhani kama RC atakuwa na Maamuzi yake bali atapokea order kutoka juu japo atakuwa sehemu ya Decision maker kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi mkoa, ila mimi ninaongelea hili from a political angle na sio final decision making.

Nimeamua kusema hivi kwa maana kwamba, ujio wa viongozi wa kigeni ndani ya Tanzania yetu ninaweza kuulinganisha na ujio wa mgeni unayefanya naye kazi nyumbani kwako.

Mgeni anapokuja kuna logistics nyingi sana (hii logistics sijui kwa kiswahili wanasemaje) zinategemewa kuwa sawa ili zoezi zima la kumkarimu mgeni liende kwa usahihi kama ambavyo linatakiwa.

Kuna mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na suala zima la ulinzi na usalama, changamoto ya misafara ya viongozi na foleni, malazi, usafi wa jiji la Dar, ukizingatia msiba huu mzito umetufika katika kipindi ambacho bado kuna mvutano mkubwa sana unaendelea baina ya Tanzania na baadhi ya nchi zitakazotuma wawakilishi wao juu ya namna tatizo (changamoto) la ugonjwa wa COVID - 19 linavyoshughulikiwa.

Mh. Paul Makonda alipokuwa RC wa Dar alijitahidi sana kwa kiwango chake kuwakarimu wageni waliokuja katika mkutano mkuu wa SADC katika nyanja nzima ya ulinzi na usalama, usafi pamoja na mambo kadha wa kadha niliyoyaorodhesha hapo juu.

Kaka yangu Aboubakar Kunenge, huu ni mtihani wako mkubwa sana wa kwanza kama kiongozi wa jiji hili. Kama ambavyo wananchi wa Dar walivyokuwa wanampa ushirikiano ndugu Makonda ndivyo ambavyo ninategemea watakupa ushirikiano wa hali na mali na kwa kasi na nguvu ile ile katika kipindi hiki kigumu tunachopitia kama nchi, vile vile katika shughuli zako za kiuetendaji hata baada ya maombolezo haya kuisha.

Ninakuombea kwa Mungu akupe hekima, busara, ujasiri pamoja na afya njema pale utakapokuwa unajiandaa na zoezi hili kuu la kitaifa.

PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.

Mkapa.jpg


MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU WABARIKI WAKAZI WA DAR.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom