Ujio wa Tundu Lissu na shamrashamra za mapokezi makubwa zaashiria CCM kutupiwa virago na wapiga kura Oktoba hii

Duniani, umewahi kumuona amiri jeshi kilema!! Majeshi hawaajili vilema.

Atakaguaje gwalide!!
Kwa bahati nzuri, watu wakiamua kumchagua mtu awe kiongozi wao, hawaangalii duniani wanafanyaje.

Kuhusu 'vilema', kwanza futa hiyo kauli. Walemavu ni kama binadamu yeyote. Wana haki zote, ikiwa ni pamoja na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Sifa za rais ni umri, maadili, akili timamu na elimu.
 
Kwanza speech ya Lisu katoa lainiii sisi tumezoea KUFOKEWA BANA. Yaani kufoka tu mwanzo mwisho.
 
Hii ni ishara kwamba watu wanahitaji mabadiliko yaani sasa hivi Lisu ndiye talk of the town sio marehemu tena.
 
Mkapa hayupo wa kutangatanga na kutishia wakurugenzi wachakachue matokeo, Bashite yuko kwenye mawe baada ya wapiga kura kumtapika na sasa mpigania haki Tundu Lissu kawasili kwa mapokezi yenye ujumbe mzito: CCM BYE BYE

Hata kocha Maximo aliletwa kwa mbwembwe na shamrashamra lakini akatupiwa virago,Tundu kitu gani kama si mhemuko tu wa kisiasa
 
Paskali hua nakukubali ingawa kuna wakati nakukataa.
Kwa hili umeonesha maono ya hali ya juu.
Mi pia sikutegemea hadi alivyoteremka kwenye ndege jana.
Mungu ibariki tanzania
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

Paskali
 
Kwani jiwe si tulijua ni mwendawazimu, muulize hata jk alijua jiwe hawezi mbona jiwe yupo na mnamshangilia
Jibu niliyokuuliza.. leo amepokelewa mgonjwa aliyepona.. Mola mwema.. kuongoza nchi hata wewe unafahamu.. hawezi..
 
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

Paskali
Unakosea sana mkuu huwezi kumlinganisha Mandela na Lissu Lissu ni mwepesi mno kwa legendary Mandela muwe na adabu vijana
 
Back
Top Bottom