Ujio wa Tundu Lissu: Msaada tutani ndugu mawakili wasomi

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,151
2,000
Jana tarehe 27. 0. 2020 ndugu yetu Tundu Lissu alifanikiwa kurejea salama nyumbani Tanzania. So haba, alipata mapokezi mazuri. Ni hukue fursa hii pia kulipongeza jeshi la polisi kwa kuhakikisha amani itawale muda wote.

Aidha naomba tukumbuke kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Hali Halisi
Wakati ndugu Tundu Lissu anapatwa na kadhia ile ya kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya, tayari alikuwa na mashitaka kadha wa kadha mahakamani. Kwa namna yoyote, kukwama kwa kesi hizo pamoja na uchunguzi wa polisi kuhusu shambulio lake unachukua sura mpya baada ya yeye kurudi.

Swali
Endapo ndugu TAL atateuliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA, je, mashitaka/kesi hizi zitamsubiri amalize kampeni?

Pendekezo
Ikitokea kesi/mashitaka yakiendelea, wafuasi na wapenzi wake wanatakiwa wajiandae kisaikolojia ili kuacha kutafuta sababu za hapa na pale.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom