Ujio wa Rais Obama Kenya tuna cha kujifunza sisi kama Tanzania

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,813
1,823
Imekuwa ni kawaida ya waTanzania kukandia, kuponda na kupinga kila kitu. Nimejaribu kuchungulia media na comments za majirani zetu Kenya nimeona ni jinsi gani walivyoweka uzalendo mbele na kila mmoja anasifia na kujiona fahari kwa ujio wa ugeni huo mkubwa.

Cha kushangaza hapa kwetu walikuja viongozi wakubwa wa dunia hii kama rais Xi wa china na Obama wa marekani lakini kilichojiri ni wabongo kuponda mara anakuja kuiba rasilimali zetu na mambo mengine yasiyo ya kiustaarabu kama hayo.

Naamini kwa dhati kabisa: TUNA CHA KUJIFUNZA KUTOKA KWA MAJIRANI ZETU
 
Kiukweli wakenya wamefunguka hawaonyeshi itikadi ktk hili wote ni wamoja.
Cha kufurahisha zaidi wapinzani kwa maana ya wawakilishi wa vya upinzani wametengewa dakika 45 za kukutana na kuongea na Obama lkn hapa kwetu siasa ingekuwa kila kona, kuna vitu vya kujifunza kutoka kwa ndg na jirani zetu Kenya.
 
Ila maandalizi waliyoyafanya kwa kweli wameingia gharama kubwa sanna, na pia inadhihirisha wazi kwamba wakenya wanampokea OBAMA kwa vile ni Son of their Land. Hongereni sana majirani.
 
Pia wenzetu wanatumia bodi ya utalii ya kenya kutangaza fursa zao kwa wamarekan na uwekezaji.sisi tuliishia kumuandalia ngoma za asili na kudeki barabara
 
Chama kinachoongoza Kenya kimetawala muda gani? Unategemea uzalendo kwenye nchi ambayo maendeleo yanaopelekwa kwenye majimbo ya chama kilichopo madarakani wakati huohuo wapinzani wakibaniwa? Hapa kwetu angalia bunge letu ambalo ni taswira ya nchi uone itikadi ilivyotawala na spika anavyoendesha chombo cha wananchi kwa mitazamo ya chama chake. Huko kenya bunge lao hoja yenye mashiko ndio inayopita, je hapa ni hivyo?
 
Kiukweli wakenya wamefunguka hawaonyeshi itikadi ktk hili wote ni wamoja.
Cha kufurahisha zaidi wapinzani kwa maana ya wawakilishi wa vya upinzani wametengewa dakika 45 za kukutana na kuongea na Obama lkn hapa kwetu siasa ingekuwa kila kona, kuna vitu vya kujifunza kutoka kwa ndg na jirani zetu Kenya.
Obama kukutana na wapinzani ni jitihada za Rais Kenyatta kuonsha kwamba anajali na kuthamini uwepo wa wapinzani licha sio kweli kwani mara kadhaa Odinga amekuwa akishinda chaguzi zote lakini wanamfanyia uhuni.
 
Wakenya wapo vizuri sana, hapa ninapoandika hii comments nipo kwenye bodaboda wakenya wamekuja kunichukua toka huku ili niende kwao kumuona Obama.
Nimewauliza wanapata faida gani kuingia gharama za kunufuata na kunipeleka huko, jamaa akanijibu kuwa wanatangaza utalii.
 
Imekuwa ni kawaida ya waTanzania kukandia, kuponda na kupinga kila kitu. Nimejaribu kuchungulia media na comments za majirani zetu Kenya nimeona ni jinsi gani walivyoweka uzalendo mbele na kila mmoja anasifia na kujiona fahari kwa ujio wa ugeni huo mkubwa.

Cha kushangaza hapa kwetu walikuja viongozi wakubwa wa dunia hii kama rais Xi wa china na Obama wa marekani lakini kilichojiri ni wabongo kuponda mara anakuja kuiba rasilimali zetu na mambo mengine yasiyo ya kiustaarabu kama hayo.

Naamini kwa dhati kabisa: TUNA CHA KUJIFUNZA KUTOKA KWA MAJIRANI ZETU
Katika kujifunza tusiangalie tu comment zao ktk mitandao ya kijamii. Kimsingi, somo lakujifunza ni kwamba tusiwe wajinga kama wakenya na serikali yao ambayo imetumia pesa nyingi ktk ugeni wa mtu mmoja ambae hakai hata zaidi ya siku mbili, badala hizo pesa ziingeenda kwenye huduma za jamii ili wanaanch wengi na hasa masikini wapate hutuma nzuri.
 
nimeipenda comment yako. ni positive lakini in otherway round. Nakubaliana na wewe kwenye hilo.
 
ukiingia kwenye media zako,yaani kula kitu ni Obama Obama,yaani the guys are so excited.
pia wamechambua mambo mengi Sana ya Obama.
hata sisi hatukufikia huko alipokuja kwetu ,jamaa wameanfika article nyingi Sana..yaani hadi mbwa wa Obama wamemchambua,aliko zaliwa na nchi aliko zaliwa
 
Pia wenzetu wanatumia bodi ya utalii ya kenya kutangaza fursa zao kwa wamarekan na uwekezaji.sisi tuliishia kumuandalia ngoma za asili na kudeki barabara

Kwani wewe utalii maana yake ni nini ngoma sio utalii au wewe utalii kwako ni simba na pundamilia? Kweli tuna safari ndefu
 
Chama kinachoongoza Kenya kimetawala muda gani? Unategemea uzalendo kwenye nchi ambayo maendeleo yanaopelekwa kwenye majimbo ya chama kilichopo madarakani wakati huohuo wapinzani wakibaniwa? Hapa kwetu angalia bunge letu ambalo ni taswira ya nchi uone itikadi ilivyotawala na spika anavyoendesha chombo cha wananchi kwa mitazamo ya chama chake. Huko kenya bunge lao hoja yenye mashiko ndio inayopita, je hapa ni hivyo?

Wewe Ni Muongo mkubwa hakuna Bunge bure Dunia hii kama la Kenya kwanza bora Bunge la JMT mara 100 waulize Wakenya watakwambia, kazi nu kujiongezea Mishahara tu na hakuna kingine!
Mbunge wa Kenya ndiyo analipwa Mshahara mkubwa klk Wabunge wote Duniani, unafikiri ni kwanini waandamanaji walichinja nguruwe na kumwaga Damu mbele ya Bunge la Kenya? Ni kwa sababu ya ulafi wa Wabunge wa Kenya!
 
Je, sisi hapa bongo tulichinja hao nguruwe,,siku bunge letu lilipotumia mabilion ya pesa kwa katiba hewa??
 
Wewe Ni Muongo mkubwa hakuna Bunge bure Dunia hii kama la Kenya kwanza bora Bunge la JMT mara 100 waulize Wakenya watakwambia, kazi nu kujiongezea Mishahara tu na hakuna kingine!
Mbunge wa Kenya ndiyo analipwa Mshahara mkubwa klk Wabunge wote Duniani, unafikiri ni kwanini waandamanaji walichinja nguruwe na kumwaga Damu mbele ya Bunge la Kenya? Ni kwa sababu ya ulafi wa Wabunge wa Kenya!

Ukisoma vizuri hoja ya uliyemquote utaona ulivyochanganya mambo swala lakulipana mishahara mikubwa mie naona sio ishu kwa sababu watu wanaweza wakalipana mishahara midogo lakini wakawa mafisadi na wala rushwa na hasara yake ikawa kubwa ni bora wangepewa hiyo mishahara mikubwa.
 
obama angetoka madarakan bila kuja kenya kuna wakenya wangeugua! wanashabikia nchi nzima utadhani malaika katua mpaka wengne walipendekeza ijumaa itengwe siku ya mapumziko kisa obama! Tanzania hatuwezi kufanya huu wehu wa wakenya
 
ww vp obama si mkenya ndiyo maana mbona.kikwete akienda hawamfanyii uzalendo
 
Back
Top Bottom