Ujio wa pesa za kwenye simu uliambatana na habari ya "financial inclusion"

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,076
2,805
Falsafa haswa ya kodi ni kwamba mwenye pato achangie gharama za uendeshaji wa serikali.

Asiye na pato hatakiwi kuchangia.

Kwa hiyo kodi sahihi haswa ni ile inayotozwa kwenye kipato.

Mfano PAYE kwenye pato la mshahara.

Kodi ya mapato - kwenye pato la biashara.

VAT kwenye mauzo ya bidhaa na huduma. Mauzo maana yake kuna pato linatengenezwa hapo.

Pia kuna kodi za forodha mahususi kwa ajili ya kulinda uchumi wa ndani ya nchi kwa kufanya bidhaa za kutoka nje ziwe ghali zaidi kupitia kodi.

Sasa mtu anatuma hela au anatoa hela kwenye simu unamtoza kodi kwa falsafa gani?

Hiyo pesa anayotuma kama ni biashara analipia kitu, basi itaonekana kwenye biashara husika na itakatwa huko kupitia kodi ya mapato.

Lakini tunatumianaga pesa mara nyingi tu kwa mambo ambayo si ya kibiashara. Rambirambi, na pesa za matumizi kwa wategemezi.

Nashindwa kuielewa hii falsafa kwa sababu ukiweka pesa benki hautozwi kodi yoyote. Yaani ni kama serikali inataka turudi kwenye mabenki tu kulipana.

Ujio wa pesa za kwenye simu uliambatana na habari ya "financial inclusion". Yaani usogezwaji wa huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi, maana ni rahisi sana kufungua kibanda cha wakala wa simupesa kuliko matawi ya benki.

Sasa serikali, waziri wa fedha kwa uvivu wa kufikiria vyanzo vipya vya mapato ya kodi wanaongeza tozo kwenye miamala. Wanaiua sekta ya mobile money transfer, wanawapa mzigo wananchi na wanazidi kufifisha ndoto za kuwa na cashless economy.

Na kwa kutoza pesa ambazo hazihusiani na mapato au biashara imeonekana ndo inafaa imekuwa kama ni ile kodi ya kichwa imerudi kwa staili nyingine.
 
Back
Top Bottom