UJIO WA MILLYA CHADEMA: Hitaji la mifumo imara ya kitaasisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UJIO WA MILLYA CHADEMA: Hitaji la mifumo imara ya kitaasisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mmbwanga, Apr 18, 2012.

 1. M

  Mmbwanga Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari iliyotapakaa katika corridor za habari za siasa ni kujiuengua kwa Millya toka CCM na kuhamia CDM. Habari yenyewe inachokonoa mjadala kwa sababu zifuatazo
  1. Millya alikuwa difficult person from his party (Rejea kesi yake na Sendeka na ugomvi wake wa kudumu na makundi mengine ndani ya CCM/UVCCM)


  2. Ni chanda na pete wa EL (Ambaye ni adui wa kisiasa wa CDM kupitia list of shame ya Mwembe Yanga)

  Sasa Millya sio mwanachama wa kawaida ndani ya CCM, kuondoka kwake kumewatikisa wana CCM…Tumemsikia Nape na wenzake wakileta sizitaki mbichi hizi…kwamba ni sehemu ya mchakato wa kuvua gamba…
  Sasa kinacholazimisha udadisi zaidi ni mixed feelings ambazo wana CDM wanazo kwa sasa. .
  · Wengine wanamwoma kama pandikizi la EL
  · Wengine wanamwoma kama anatafuta pa kutokea baada ya kufungiwa milango ya kitaasisi kwenye chama chake
  · Wengine wanamwoma kama mroho wa madaraka anayekinyemelea kiti cha Arusha mjini ama Simanjiro
  · Wengine wanamwoma kama zao la awali la M4C
  My views:
  1. CDM kinatazamwa kama chama tawala in a wait hivyo kila mtu mwenye maslahi na siasa za vyama ni lazima akae karibu nacho. Na kwenye siasa timing ni jambo la msingi sana
  2. Karibu au zaidi ya 50% ya wanachama na wapiga kura wa CDM wa leo wamekwishawahi kuwa wana CCM ama kukipigia kura chama hicho. Hivyo Millya sio ajabu kuhamia CDM leo
  3. Millya amekuwa kwenye confrontational politics hivyo kuonekana kirahisi zaidi…yawezekana kuna wana CDM wengi wa aina ya Millya ila hawana umaarufu kiasi wakajulikana kama Millya
  CDM ifanye nini?
  Iboreshe Recruitment and Retention Sytems kwa wanachama wapya ili kuepuka hofu inayojitokeza sasa. Mfano wa karibu ni kadhia ya kiutawala ndani ya CDM iliyosababishwa na Shibuda…na ni lazima kujua, tuendako kutakuwa na kina Shibuda wengi sana. CDM inakaribia kuwa dodoki, hivyo kufyonza vichafu na visafi. Ni wajibu kwa CDM kuwa na mkakati rasmi wa kudeal na ujio wa wanachama wapya hata wakiwa wachafu kiasi gani. Who knows, tunaweza kusikia EL na RA wanataka kuingia CDM, dawa haiwezi kuwa kuwazuia kuingia ila kuwacontain.
  Bila CHADEMA imara, mustakabali wa nchi uko mashakani
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Umenena vyema, waboreshe hata screening process.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,642
  Trophy Points: 280
  Very constructive idea mkuu wangu,Chadema wanachangamoto kubwa mno kuelekea kushika dola
   
 4. Mozila

  Mozila Senior Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Millya sio wa kwanza kuondoka ccm,kuondoka kwake ni kuimarisha ccm.why always 1985-20? Is ccm?
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa siasa ilivyo ni mchezo mchafu sitosita kuamini jamaa kaja kumsafishia el njia kwakujifanya kujiunga na CDM usipoamini mpaka ifikapo 2015 utaamini
   
 6. M

  Mmbwanga Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mozila...CCM ina sura ua dubwana kubwa kitasisi...imejisimika katika siasa za nchi kwa muda mrefu na kwa rasilimali nyingi za halali na haramu...iko madarakani kwa sababu halali na haramu...
  Kuliondoa dubwana CCM sio kazi rahisi....nikubaliane haraka yeye sio wa kwanza kuondoka...waliondoka kina Seif Sharrif Hamad, Mrema, Mpendazoe na wengine wengi sana...
  Je unaweza kufananisha uimara wa kitaasisi wa CCM kabla ya kuanza kuikmbiwa kipindi hicho na CCM tunayoiona leo??
  Na jambo la ziada ni hili, hoja kwa CCM isiwe Millya ila sababu zilizomfanya aondoke...bila kufanyia kazi sababu hizo ni dhahiri kutakuwa na wengi watakaokimbia (kama ambavyo wengi wasio maarufu wamekwisha fanya)
  Mfano mwingine wa CCM kukimbiwa (tena bila kuita waandishi wa habari au kurudisha kadi ya uanachama) ni wakazi wa jimbo la KAWE kuchagua CDM kwenye ubunge 2010.
  Je unajua Oysterbay, Masaki, Msasani, Mikocheni, Mbezi Beach, Kunduchi Beach, Makongo Juu yote ni jimbo la Kawe? Umewahi kujiuliza ni kina nani wanaishi maeneo hayo??????? Huku ndiko CHAMA na SERIKALI huwa inalala, inafanya send off, harusi na misiba.
   
 7. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 180
  ivi Millya asingekuwa wa kaskazini wangempokea kiraisi ivyo!?
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,642
  Trophy Points: 280
  Anayependa kuongelea ukabila na udini yeye ndio mkabila na mdini!
   
Loading...