Ujio wa kodi mpya ni nini? Serikali inalenga nini kwa umma kuongeza tozo mpya kwa mlipa kodi kupitia miamala ya mitandao?

ImanHB

Member
Mar 14, 2019
10
17
KODI (ushuru) ni malipo ambayo kila mtu mwenye shughuli za kuingiza kipato anatozwa na serikali kulingana na kipato chake. Hivyo kodi ni chanzo cha mapato ya serikali ambayo hutumika kugharamia huduma za jamii zinazotolewa na serikali kama ujenzi wa miundombinu, ujenzi wa mahospitali, shule, viwanda, masoko na kughalamia malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma.

  • Chanzo cha uvumbuzi wa kodi mpya
Shughuli nyingi za serikali hutegemea kodi ya mwananchi, hivyo kila serikali mpya inapoingia madarakani hujaribu kutafuta nyenzo mpya za kuenndeleza na kukuza uchumi wa nchi zaidi ya pale ulipofikishwa na serikali iliyopita. Kwa kuwa kila utawala una sera zake, ni jambo halisi kabisa kwa kiongozi ili awe kiongozi bora ni lazima aonyeshe mabadiliko kwa umma wake na kuipigisha jamii hatua za kimaendeleo zaidi ya yale aliyowakuta nayo, na kuwatatulia matatizo yao yaliyoshindikana kutatuliwa na kiongozi aliyepita. Yaani aonyeshe mapya asifanye yaliyokwisha kufanywa na viongozi waliopita.
  • Tozo mpya kwa makato ya fedha kupitia miamala ya mitandao
Tozo za makato ya fedha kwa miamala limekuwa wimbi zito na kuleta sitofahamu kwa umma tangu itambulishwe, hasa sisi walio na kipato cha chini. Ukweli usiopingika sio wote ila wengi wao wanaumia, kitendo ambacho kinatufanya kutafuta njia zingine mbadala kufanya malipo na miamala ya kutuma na kutoa pesa kwa njia ya mitandao.
Lakini kwa tathmini niliyonayo naweza kuushauri umma kuwa japo inaumiza kwa kiasi, ila tujaribu kulipokea hili jambo maana ya kuwa serikali haipendi kumuumiza mwananchi wake ila imefanya hivi katika harakati za kupambana na umaskini wa taifa la kesho.

Tunaweza kuona utawala wa aliyekuwa Rais wetu wa awamu ya tano hayati Mh. John P. Magufuli , kipindi anaingia madarakani kuna baadhi ya mambo mengi yalibadilika na mabadiliko makubwa yalikuwa kwenye upande wa kodi. Ukusanyaji na usimamizi wake wa kodi ulikuwa wa kipekee tofauti na ilivyokuwa kwa tawala za nyuma. Kila muda uliposogea katika utawala wake alibuni njia mpya za kukusanya kodi mpaka mjasiliamali mdogo kama machinga alianza kuchangia taifa kupitia vitambulisho vya ujasiliamali.

Hakuishia hapo pia alifufua kodi za majengo na ardhi ambazo hazikutekelezwa na viongozi waliopita. Kuna baadhi waliumia, kuna baadhi walilaumu na wengine kujutia utawala wake. Lakini mwisho wa yote hizo kodi zetu zimetangaza taifa letu kwa kujenga miradi mikubwa kama Rail Way ya standard gauge, kufufua shirika la ndege, ujenzi wa vivuko na madaraja pia kupitia kodi hizo alifufua mitambo ya kufua umeme ambayo ilitoa ajira kwa watanzania wengi kitendo ambacho kiliishawishi Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuwa taifa lenye uchumi wa kati.

Hivyo nilikuwa najaribu kukumbushia juu ya kodi zilizojitokeza hapo nyuma na jinsi gani zimeweza kulisogeza taifa katika maendeleo. Nikirudi kwenye mjadala, kwa mtazamo wangu japo inaumiza wengi lakini naona ni vyema umma tulipokee hili swala la tozo za makato maana naamini serikali imebuni hii injia ya kukusanya kodi si kwakuwa taifa limeishiwa fedha bali ni juhudi tu za kutaka taifa lisonge mbele zaidi ya hatua aliyotufikisha hayat Mh. John Magufuli.

ASANTENI KWA KUUNGANA NAMI
 
Back
Top Bottom