Ujio wa Kiwanda Cha Mount Meru Millers na hatima ya viwanda vidogo vya kukamua alizeti Singida

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Wakuu kwa Wiki Mbili sasa nashuhudia magari kwa magari ya kisomba mitambo ya kiwanda kipya kinacho tarajiwakujengwa Mjini singida na Mount Meru Millers Co Ltd,

Mitambo hiyo imekuwa ikisombwa kutokea Bandari ya Mombasa kwa kupitia Namanga hadi Singida, na kwa mujibu wa Waziri nilimsikia kiwanda hiki kitakuwa ni kikubwa kabisa East and centre Africa katika viwanda vya kukamua mafuta ya alzeti,

Hii ni habari njema kwa Wakulima wa Alzeti katka Mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, make huku ndo alzeti inapo limwa kwa wingi sana,

Na inaweza kuwa si habari njema kwa wamiliki w viwanda vidogo kwa miji ya Singida, Babati, Hanang na hata Dodoma, hii ni kwa sababu kiwanda kipya kitakuwa na uwezo mkubwa sana na kuweza kukamua mafuta mengi kwa wakati mmoja, na kitahitaji Alzeti ya kutosha,

Kwa Viwanda vidogo vidogo ambavyo ni vingi sana mjini Sinida na Babati vitakuwa na wakati mgumu kushindana na huyu jamaa,na ikumbukwe kabla ya hapo MOUNT MERU MILLERS CO LTD ndo alikuwa na mitambo ya kuweza kukamua mashudu ya alzeti na kupata mafuta tena, hii ni kwa sababu viwanda karibia vyote kwa miji ya Babati na Singida hukamua mafuta kwa 80% yaani mashine hazina nguvu ya kukamua kwa 100%

Ni wakati sasa kwa wamiliki wa Viwanda vidogo katika miji hiyo wachague moja, Kuungana pamoja na kuwza kushindana na Mount Meru Millers au wafunge viwanda, na kwa Watanzaia tulivyo watu wako radhi kufunga biashara kuliko kuungana pamoja, na hakuna njia nyingine zaidi ya kuungana pamoja, make kwa mtu mmoja mmoja kupata mtaji wa kushusha kiwnda kama cha Mount Meru si ishu ya kitoto,

Huyu Mount Meru Miller amekuwa ndo mtu pekee anaye uza nje ya nchi CRUDE SUNFLOWER OIL, na huwa anapeleka nchi za Kiarabu,

NA HII NI IWE KWA WAFANYA BIASHARA WENGINE KWA KWELI BILA KUUNGANA NI VIGUMU SANA KUWEZA KUSHINDANA NA WATU WENYE MITAJI MIKUBWA KABISA
 
Mkuu Chasha sidhani kama hicho kiwanda kitatosheleza mahitaji yote yaani soko la ndani na nje, so bado hao wadogo wadogo nao wataendelea kupiga kazi. Wawekezaji wakubwa nao wana challenges zao ikiwemo operating costs kuwa kubwa na hivyo kushindwa kukamata soko lote. Ulaya kuna masupa maketi ya kufa mtu lakini bado wahindi wanapiga kazi na vimini super market vyao
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mmoja wa watakaoendelea kununua mafuta yanayozalishwa na wakamuaji wadogo?hayo mafuta ya mount meru siyataki hata kidogo!!mafuta yao ya pili yanakamuliwa kwa kuchanganya na petrol!nimewahi kufanya kazi kwenye kiwanda chao cha arusha na baadaye nilihamishiwa singida mara tu waliponunua kiwanda hicho kilichopo eneo la mangua-njuki karibu na kambi ya FFU,ambapo mwanzo kilimilikiwa na Bunda oil mills,hapo ndipo nilipogundua njia hii ya ukamuaji iliyonitia mashaka kuhusu afya ya mlaji,mafuta yanayopelekwa nje(uarabuni nk)ni ile first product isiyohusisha njia hiyo,huku mafuta yanayotokana na makapi+petrol yakiuzwa humu nchini,mafuta ya kienyeji ni bora kwangu kuliko hayo ya viwanda vikubwa.
 
Na Mgama, iringa kinajengwa miller kubwa sana ya sembe, mwekezaji huyo anategemewa kununua sehemu kubwa ya mahindi ya nyanda za juu kusini kwa bei ya soko

Maana yake? Kwa mkulima? Mahindi na alizeti zitakua cash crops as opposed to food crops ilivyo sasa.

Hivyo mjitahidi kurudi kwenye kilimo kinalipa
M
 
Mimi ni mmoja wa watakaoendelea kununua mafuta yanayozalishwa na wakamuaji wadogo?hayo mafuta ya mount meru siyataki hata kidogo!!mafuta yao ya pili yanakamuliwa kwa kuchanganya na petrol!nimewahi kufanya kazi kwenye kiwanda chao cha arusha na baadaye nilihamishiwa singida mara tu waliponunua kiwanda hicho kilichopo eneo la mangua-njuki karibu na kambi ya FFU,ambapo mwanzo kilimilikiwa na Bunda oil mills,hapo ndipo nilipogundua njia hii ya ukamuaji iliyonitia mashaka kuhusu afya ya mlaji,mafuta yanayopelekwa nje(uarabuni nk)ni ile first product isiyohusisha njia hiyo,huku mafuta yanayotokana na makapi+petrol yakiuzwa humu nchini,mafuta ya kienyeji ni bora kwangu kuliko hayo ya viwanda vikubwa.

sio mtaalamu katika chakula ila ninachofahamu kidogo ni kuwa hii refining ya pili inaweza ikainvolve normal hexane solvent na hii n-hexane ni one of the products from petroleum refining so labda umechanganya kuwa ni petrol ilhali ni solvent.
ki kawaida hii solvent inatakiwa iondolewe to the extent inakuwa kidogo sana na isilete madhara kwa mtumiaji, na hapo ndipo changamoto zainapokuja , ila vile vile mafuta kama hayajafanyiwa double refining yanakuwa na kaharufu flani hv na pia stability yake ni ya muda mfupi sana
 
Hivi acre 1 ya alizeti inatoa mafuta lita ngapi?

hili hutegemea mambo mengi kama aina ya mbegu , mvua, na fertility of the soil na matunzo ya shamba kwa ujumla katika dhana nzima ya kilimo cha kisasa. wapo wanaopata magunia 20 kwa ekari na wapo wanaopata gunia moja kwa ekari, hata hivyo jambo la kueleweka ni kuwa gunia moja la debe sita litakupatia mafuta kati ya lita 16-18-20, pamoja na mashudu ambayo still ni bidhaa inayouzika vizuri
 
Mimi ni mmoja wa watakaoendelea kununua mafuta yanayozalishwa na wakamuaji wadogo?hayo mafuta ya mount meru siyataki hata kidogo!!mafuta yao ya pili yanakamuliwa kwa kuchanganya na petrol!nimewahi kufanya kazi kwenye kiwanda chao cha arusha na baadaye nilihamishiwa singida mara tu waliponunua kiwanda hicho kilichopo eneo la mangua-njuki karibu na kambi ya FFU,ambapo mwanzo kilimilikiwa na Bunda oil mills,hapo ndipo nilipogundua njia hii ya ukamuaji iliyonitia mashaka kuhusu afya ya mlaji,mafuta yanayopelekwa nje(uarabuni nk)ni ile first product isiyohusisha njia hiyo,huku mafuta yanayotokana na makapi+petrol yakiuzwa humu nchini,mafuta ya kienyeji ni bora kwangu kuliko hayo ya viwanda vikubwa.

Mkuu Petrol inachanganywa kwenye mafuta ya kula? Unajua petrol kweli? mkuu utauwa na chuki binafisi na hawa jamaa, na kingine Mount Meru hauzi mafuta taliyo safishwa nje, anauza Crude Sunflower oil,
 
Mkuu,

Kiukweli kuungana kwa wasindikaji wadogo wa alizeti kuna umuhimu mkubwa lakini jinsi nionavyo kuna kazi kubwa sana ya kufanya hadi waelewe point yako. Kikubwa kinachowasumbua ni umimi, kila mtu anataka kuonekana ana kiwanda....wakati wangeweza kuungana wakawa na kiwanda kimoja kikubwa, chenye teknolojia bora na hata mtaji mkubwa wa kiushindani.

Ujio wa Mt. Meru Singida utakuwa na mengi sana. Kwa wakulima, wenyewe kwao neema. Bei za mbegu za alizeti zitakua za kiushindani hivyo watapata malipo bora kwa mazao yao. Kwa upande wa wasindikaji wadogo hapa kidogo majanga. Mtaji mkubwa wa Mt. Meru pamoja na mahitaji makubwa ya kiwanda yatawasumbua sana. Huenda hata uzalishaji wao wa mafuta ukayumba kutokana na nguvu kidogo watakayokuwa nayo kwenye kugombania malighafi.

Kwa upande wa sera za usindikaji alizeti nchini, hili ni pigo jingine kwa wasindikaji wadogo (huenda Mt. Meru wameliona hili). Mafuta yatakayoruhusiwa kuuza kwa ajili ya final consumption ni yale yaliyo fanyiwa chemical refining na kuongezwa vitamin A. Hii itawashinda wengi na hivyo watalazimika kuuza mafuta yao kama crude oil. Matokeo yake ni kushuka kwa kiwango cha faida walichokua wakipata kwa miaka chungu nzima iliyopita.
 
NI jambo la amaana hao wadogo watajua namna ya kujiadjust mbele ya safari
 
Wakuu kwa Wiki Mbili sasa nashuhudia magari kwa magari ya kisomba mitambo ya kiwanda kipya kinacho tarajiwakujengwa Mjini singida na Mount Meru Millers Co Ltd,

Mitambo hiyo imekuwa ikisombwa kutokea Bandari ya Mombasa kwa kupitia Namanga hadi Singida, na kwa mujibu wa Waziri nilimsikia kiwanda hiki kitakuwa ni kikubwa kabisa East and centre Africa katika viwanda vya kukamua mafuta ya alzeti,

Hii ni habari njema kwa Wakulima wa Alzeti katka Mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, make huku ndo alzeti inapo limwa kwa wingi sana,

Na inaweza kuwa si habari njema kwa wamiliki w viwanda vidogo kwa miji ya Singida, Babati, Hanang na hata Dodoma, hii ni kwa sababu kiwanda kipya kitakuwa na uwezo mkubwa sana na kuweza kukamua mafuta mengi kwa wakati mmoja, na kitahitaji Alzeti ya kutosha,

Kwa Viwanda vidogo vidogo ambavyo ni vingi sana mjini Sinida na Babati vitakuwa na wakati mgumu kushindana na huyu jamaa,na ikumbukwe kabla ya hapo MOUNT MERU MILLERS CO LTD ndo alikuwa na mitambo ya kuweza kukamua mashudu ya alzeti na kupata mafuta tena, hii ni kwa sababu viwanda karibia vyote kwa miji ya Babati na Singida hukamua mafuta kwa 80% yaani mashine hazina nguvu ya kukamua kwa 100%

Ni wakati sasa kwa wamiliki wa Viwanda vidogo katika miji hiyo wachague moja, Kuungana pamoja na kuwza kushindana na Mount Meru Millers au wafunge viwanda, na kwa Watanzaia tulivyo watu wako radhi kufunga biashara kuliko kuungana pamoja, na hakuna njia nyingine zaidi ya kuungana pamoja, make kwa mtu mmoja mmoja kupata mtaji wa kushusha kiwnda kama cha Mount Meru si ishu ya kitoto,

Huyu Mount Meru Miller amekuwa ndo mtu pekee anaye uza nje ya nchi CRUDE SUNFLOWER OIL, na huwa anapeleka nchi za Kiarabu,

NA HII NI IWE KWA WAFANYA BIASHARA WENGINE KWA KWELI BILA KUUNGANA NI VIGUMU SANA KUWEZA KUSHINDANA NA WATU WENYE MITAJI MIKUBWA KABISA

CC: jingalao

Mambo ya aibu haya. Nilikuambia kwamba awamu hii inafanya maigizo na ndio maana hata wewe unakwepa kuweka rekodi ya viwanda kila mkoa. Halafu kwa mwendo huu unategemea tuamini hiyo viwanda 3000+ tunavyoambiwa viko hapo mkoa wa Pwani?
 
ni kweli kiwanda kilikuwepo muda mrefu lakini hakikufunguliwa kwa sherehe, ni shughuli tu za uzalishaji ndio zilifunguliwa.
huu ni wakati muhafaka kufunguliwa sababu kama taifa tupo zama za tanzania ya viwanda sio ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
 
Eti kilifungwa na Lugola Rais ndo kakifungua
 
ni kweli kiwanda kilikuwepo muda mrefu lakini hakikufunguliwa kwa sherehe, ni shughuli tu za uzalishaji ndio zilifunguliwa.
huu ni wakati muhafaka kufunguliwa sababu kama taifa tupo zama za tanzania ya viwanda sio ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
iko miradi mingi sana iliyoanza utekelezwaji lakini haijawahi kufunguliwa
 
Hayo ndiyo huwa na kataa ,sikila shughuli itaitwa kiwanda,hivi vingine ni factory sio viwanda
 
Back
Top Bottom