Ujio wa kitabu cha mhariri msalabani cha Ben Mtobwa

nameless girl

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
4,195
2,663
Kwanza tupeane pole na hili janga lililovamia dunia yetu. Lakini hatuna budi kupambana nalo litoweke hapa duniani kwa kufuata yale ambayo wataalamu wametuambia.
Mbali na hapo, ninapenda kuwatangazia vitabu vya nguli marehemu Ben Mtobwa.
Sasa kitabu cha Mhariri Msalabani kinapatikana kwa bei ya shilingi elfu sita za Kitanzania.
Pamoja na vingine kama
  1. Mtambo wa mauti (10,000)
Hii ni riwaya ya kipelelezi inayomuhusisha msichana anayeitwa Monalisa. Msichana huyu mpole, mzuri mwenye haya, anamtafuta Joram Kiango kwa nia ya kusaidiwa muswada wake.
Ghafla msichana huyu mpole, mzuri, anafia kwenye kitanda cha Joram Kiango.
Joram anafanikiwa kutoroka toka eneo la tukio lakini kila anapokimbila, msichana huyu aliyefariki, anaonekana tena akiwa hai, lakini safari hii akiwa msichana katili ambaye yu tayari kufa au kuua.
Imekuwaje akawa hai? Mimi sijui? Mtambo wa mauti ina majibu yote hayo.

2) Najisikia kuu tena (10,000)
"Inspekta najisikia kuua tena..." Imagine wewe ni polisi kisha unapokea simu hiyo ambapo unafikiri ni mwendawazimu fulani aliyejisikia kuchezea jeshi la polisi kwa kupiga simu kujifurahisha.
Lakini pale ambapo simu hiyo inakuwa inaleta madhara ya vifo kadhaa, mambo yanakuwa si mambo katika kituo cha polisi mpaka pale Joram Kiango anapoingilia kati.

3) Mikononi mwa Nunda (10,000)
Hapa tunakutana na msichana mpole, mzuri mwenye maumivu makubwa huko nyuma. Anajikuta akichukia wanaume wote hivyo anaua kila anayeonyesha kumtamani.
Lakini hakuishia hapo tu, kila alipofanikiwa kuua, akajipatia wazo la kukusanya pesa kwa njia ya mauaji.
Mwisho wake ulikuwa ni nini? Yote hayo unayapata katika kitabu cha Mikononi mwa Nunda.

4) Malaika wa shetani (10,000)
Ni usiku wa manane. Mjumbe kutoka nchi ya mbali akiwa taabani kwa uchovu na maradhi anafanya hili na lile hadi anamfikia Joram Kiango. Lakini baada ya kumwona Joram Kiango, pasipo kuongea lolote lililompeleka hapo, anaanguka na kufa mkononi akiwa na ujumbe...

5) Salamu toka kuzimu (10,000)
Wakiwa wanataka kufanya jambo baya kwa nchi yetu, kikwazo kinakuwa ni Joram Kiango. Hivyo ni lazima auawe kwanza ili mipango mingine iendelee.
Aliyepewa jukumu hilo anafanikiwa kupiga bomu mahala ambapo Joram Kiango yupo....
Alifika vipi kuzimu na kurudi duniani? Mimi na wewe hatujui. Ila kitabu hiki ndicho chenye majibu haya.

6) Dimbwi la damu (10,000)
Hapa Joram anakwenda kwao Kigoma ambapo badala ya kupumzika, mambo anakutana na uovu mkubwa ambao unafanywa na baadhi ya watu ambao hawaoni tabu kupoteza maisha ya mtu ili kufanikisha lengo lao.

7) Mikataba ya kishetani (10,000)
"Atakuwa amevaa suruali ya kitambaa, yenye rangi nyeusi na koti lake lenye rangi ileile juu ya shati lenye rangi ya bdnedera ya taifa. atatoka nje ya mlango wa hotel saa nne na robo akiwa katikati ya Rais wa nchi kulia kwake na bilionea wa machimbo ya madini upande wa pili.
Baada ya muuaji huyu kufanya kazi yake, anashangazwa sana na taarifa ambazo alipewa kufanikisha kazi yake. Nani anayeweza kujua nguo ya mtu ambaye anapaswa kuuawa kuwa atavaa nini na atatoka muda gani hotel na atasimama wapi!
Muuaji anapogeuka kuwa mpelelezi wa mauaji yake mwenyewe.

8) Kiguu na njia (15,000)
Hii ni riwaya ya kihistoria inayomuhusu Kionambali Mtukwao ambaye kutokana na mila potofu, wanakijiji wanataka kumuua. Babu yake anamshawishi kukimbilia kwenda sehemu nyingine ikiwa kama njia itakayomwezesha yeye kupata elimu iliyokuwa inatolewa na wakoloni.
Lakini babu anamuachia 'ulinzi' hirizi ambayo imerithiwa toka kwa mababu wa babu yake katika ukoo wao. Hirizi hiyo inapoonekana na padri, hapo ndoto ya Mtukwao kufanikisha ndoto yake ya kupata elimu inakufa lakini mwanzo wa utembezi wake unazaliwa na kutufikisha sehemu mbalimbali ambazo zinatufundisha na kutuburudisha.

9) Pesa zako zinanuka (10,000)
Hapa tutakutana na Kandili ambaye alikuwa masikini wa kutupa. Lakini ghafla anakuwa mtu mwenye wadhifa mkubwa sana na mali nyingi. Pesa zake zinasababisha vifo vya baadhi ya watu na hata mtoto wake wa kumzaa pasipo yeye mwenyewe kufahamu.
Mwanamke aliyempenda kwa dhati anamtaka Kandili arudishe pesa hizo alipoziiba kisha warudi kuanza maisha upya.

10) Zawadi ya ushindi (10,000)
Rusia msichana mzuri, mzalendo ambaye anamshawishi mchumba wake kwenda kupigana vita dhidi ya Idd Amini.
Sikamona anakubali kwenda huku akijua kwamba, akirudi toka vitani, Rusia atampatia zawadi ya ushindi.
Huko Sikamona anapigwa na bomu...

11) Dar es salaam usiku (10,000)
Hapa tutaona maisha ya wasichana wengi wanaotegemea miili yao ili kujipatia chochote.
Tutakuwa na Rukia ambaye atatuonyesha athari nyingi za kuishi maisha ya kutegemea miili na changamoto nyingi zinazotokea katika kazi zao.
Sambamba na Rukia, pia tutakuwa na Hasira pamoja na Hasara ambao ni watoto wa mtaani wanaohangaika mradi kukuche.

12) Mhariri Msalabani (6,000)
Hii si riwaya ya kutunga kama ambavyo Mtobwa alivyozoeleka. Hapa anaongelea changamoto ambayo iliwahi kumkuta akiwa katika harakati za kufanikisha ndoto zake. Pamoja na hayo, tutapata kuifahamu historia ya marehemu Mtobwa katika kitabu hiki.

13) Roho ya paka (10,000)
Hapa ni mpambano kati ya Joram Kiango na Kakakuona. Jambazi ambaye anatumwa kwenda kumuua Joram Kiango. Hajali juu ya maisha ya mtu mwingine. Mradi mauaji yake anatumia kufikisha ujumbe kwa Joram Kiango, haoni tabu. Pale anapomfikia Nuru, msichana wa Joram Kiango, mambo yanakuwa si mambo.....

14) Tutarudi na roho zetu? (10,000)
Wakati Afrika ikiwa imekumbwa na hujuma nzito za kiuchumi zinazoambatana na kuhatarisha maisha ya watu, mashujaa wanatumwa kwenda South Africa lakini hakuna anayerudi akiwa hai.
Dunia inamlilia Joram Kiango lakini Joram huyu si kama yule wa zamani. Joram huyu ni mlevi anayependa starehe. Mbaya zaidi anaiba pesa na kukimbilia South Africa kufanya starehe.
Huko hana uhakika kama atarudi na roho yake ama la.

VINAPATIKANA WAPI?
DAR ES SALAAM,
- POSTA MPYA KWA KAKA GEORGE 0713454152
- KINONDONI KONA YA RIWAYA DADA ZAMIRA 0655428085
MBEYA KWA DADA EDNA 0754091481
ARUSHA KWA KAKA ALLY 0656744390
KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANE KWA NAMBA 0712504985
Image may contain: 1 person, indoor
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom