Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Tayari kuna mchakato umeanza wa kuanzisha taasisi rasmi ya gay, lesbian, transgender Tanzanians ili kutetea maslahi yao na kutoka katika maficho yao. Mchakato umefikia mbali na wakati wowote watajitokeza ili kujiweka wazi kuwa nao wapo na taasisi yao itambuliwe rasmi. Swali - Je Tanzania nchi yenye kudai kila mtu anastahili haki "ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake".. iko tayari? Tunajua wapo na wengine ni marafiki na jamaa zetu - je tufute sheria ambazo zimepitwa na wakati kama nchi nyingi duniani zimefanya au tuendelee kudai kuwa si "uafrika na ni dhambi" wakati tunajua kuwa wapo? Mjadala is officially OPEN.