Ujio wa Chama Kipya -Patriotic Front Alliance-(PFA) na 'Kujitenga' Kwake..

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Naona wanasiasa wetu nchini wanazidi kujitayarisha na 2010...

Vyama vitano vyaanzisha umoja


Na Muhibu Said

VYAMA vya Democratic Party (DP), Demokrasia Makini, National League for Democracy (NLD), PPT-Maendeleo na Sauti ya Umma (Sau), vimejitenga rasmi na wenzao wa upinzani na kutanga umoja mwingine.


Kuanzishwa kwa umoja huo ni kujitoa rasmi na ule wa vyama vya Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Labour Party (TLP) na NCCR-Mageuzi.


Ushirikiano utajulikana kama Patriotic Front Alliance (PFA), ulizinduliwa na viongozi wake wakuu kwenye sherehe zilizofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam jana, ukiwa ni mwaka mmoja tangu vyama vya CUF, Chadema, TLP na NCCR-Mageuzi, kuanzisha ushirikiano Oktoba, mwaka jana.


Mkataba wa maelewano kati ya vyama hivyo, ulitiwa saini jana na Katibu Mkuu wa DP, Georgina Mtikila, Mwenyekiti wa Demokrasia Makini, Profesa Leonard Shayo, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi, Kaimu Katibu Mkuu wa PPT-Maendeleo, Hamisi Saidi Hamadi na Mwenyekiti wa Sau, Paul Kyara.


Akizindua ushirikiano huo, Mwenyekiti wa muda, Dk Makaidi alisema, sababu zilizofanya waanzishe ushirikiano huo, zinatokana na sera za vyama vyao alivyoviita vya kizalendo, kuendana na mrengo wa kushoto tofauti na vyama vya wenzao ambavyo ni vya mrengo wa kulia.


"Sera za vyama vya wenzetu, imelenga zaidi nguvu ya soko na ubwanyenye, lakini sisi ni sera za jamii," alisema Dk Makaidi.


Sababu nyingine, inatokana na kuwepo viashiria na utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unakaribia tamati, na kwa hiyo, wameona wajipange upya kuunganisha nguvu za kisiasa kuinusuru nchi na watu wake kuangukia mikononi mwa watawala mbadala wabovu kama wanaotarajia kuwafukuza sasa.


Hata hivyo, Dk Makaidi alisema ushirikiano wa vyama vyao, utakuwa tayari kufanya kazi na umoja wowote wa wapinzani uliopo hivi sasa au utakaoundwa baadaye kwa manufaa ya taifa.


Vipengele walivyokubaliana kushirikiana, ni masuala muhimu kitaifa, kusimamia maslahi ya taifa, kuhakikisha mgawanyo bora wa rasilimali za taifa, kusimamia kuwepo utawala unaoheshimu Katiba na sheria, kusimamia utawala bora wa demokrasia, haki za binadamu na haki za raia, kudai na kupigania kuwepo Katiba mpya na muafaka wa kisiasa nchini.

Source link: Mwananchi.


SteveD.
 
haya sio matarisho ila ni kubomoa nguzo za ujenzi wa muungano mkubwa uliokuwa ukitegemewa. Nina hakika k za Zitto na Dr. Slaa zimetumika kama ni mbolea ya uchochezi wa utengano huo.
kwa hiyo kuundwa kwa chama hiki kipya kunatanguliwa na KUJITENGA kwa vyama hivi ktk muungano wao wa mawasiliano. Pengine yawezekana kucheleweshwa kwa muungano halisi na kuwepo kwa kitu kimoja wakati muda wa kujitangaza unazidi kuyoyoma hawa jamaa wameona kuwa hawawezi kushiriki ktk upuuzi wa siasa za kuvikana vilemba..
Jamani hivi lini hawa jamaa wa CUF, Chadema TLP na NCCR- Mageuzi tupate kuwafahamu viongozi mapema.
 
Hata mashuleni kwa wale waliosoma kwa kutumia makundi baada ya Lecture huwa yapo.

Mkiwa mnafanya discussion wakati mchango wako ni mdogo huwa linatokea kundi jingine lenye uwezo unaoshabiliana ndani ya kundi lenye uelewa unaolingana hili kuokoa jahazi kwa masilahi ya wahusika.
 
Back
Top Bottom