Ujio wa Brazil - Tuiuze Tanzania vizuri tena 'Bure'

icon1.gif
ina maana tutaikosa hii chenga!!!!!


2yk0qoh.gif


Kweli mkuu wangu tutakosa mengi.
 
Nadhani kuja kwao bado hatihati. Katika nadharia za uongozi/biashara huwezi kupata matokeo ya kudumu kwa mechi moja ya Brazil. Tutakachopata ni kuandika historia tu kwamba tulicheza na Brazil, if at all they will show up !
 
hata taifa stars ni kivutio tosha cha utalii bongo ndo maana wanahitaji kucheza na stars ili wafurahi maana wanaambiwaga kuna kivutio cha hatari bongo hawataki kuamini sasa wameamua wakajionee wenyeeeee!!! mgosi upooooz?
 
three billions ni too much aisee, haiji kichwani kabisa. hii nchi tunatumia pesa kama vile tunajua kuzitafuta vile....badaye tunakinga bakuli kuomba misaada kwa hao hao brazil pengine..
 
Hii wizara ya utalii apewe Dr. Magufuli......lakini hadi inakera hivi miwaziri mingine ikoje?? haina akili kweli?? eti mwangunga......so what???

I won't be suprised kusikia Waziri wa Utalii hana taarifa kwamba Brazil wanakuja. Na mbaya zaidi ni pale ambapo awe ana taarifa kwamba wanakuja ila asijue kwamba ni fursa muafaka ya kutangaza utalii wa nchi nchi yetu, kwa kuwa tu hajui tofauti ya Brazil na Tanzania kwenye ubora wa soka. Tuna safari ndefu kuliko mnavyofikiria.
 
Wehu mtupu, kwa tsh 3bil?

TFF wamelipa USD 1.5m sawa na Tshs 2.25b. Kwa pesa za kiingilio na wadhamini wa matangazo ya biashara, nina uhakika wata ''break-even''. Kwa hiyo faida kubwa tunayoipata hapo (na tumeshaanza kuipata) ni kuitangaza nchi yetu kwa kuwa media toka dunia nzima inafuatilia ujio huo.

Pia si vibaya kama tukagawana hiyo ''nantional cake'' kwa njiaa hii badala ya kuwaachia kina Liyumba peke yao. Its a once in a lifetime exeprience.
 
daah gharama yakutangaza utalii huo ni Tsh 3 Bn kwa habari zilizoko baranarani.
 
Matangazo hayo ya utalii yataharibiwa na tangazo la matokeo ya mechi yenyewe;

6 - nil!

inabidi Brazil wajihadhari maana wavuta bangi wetu wanaweza kuondoka na viuno vya watu.
 
hilo soko la utalii tukiwa wazembe tunaweza tusilitangaze kabisa. nia yetu kubwa nchi zitakazo angalia pambano hili kama walivyotabiri idadi ya watu itakuwa (mil 160 watatazama) kuweza kuitambua tanzania kwenye mambo ya utalii.

je tumetayarisha matangazo ya vivutio vyetu na kulipia kwenye hizi channel zitakazo rusha hii mechi moja kwa moja hili watangaze vivutio vyetu kabla ya mechi,wakati wa halftime na baada mpira kuisha? au tunategemea tu kwamba hizi nchi wakiona brazil wanacheza na tanzania watapata hamu ya kuja nchini kwetu?


au tutaendelea kuwaachia wakenya kutangaza mlima kilimanjaro kitu ambacho wamefanya vizuri sana kushinda sisi.
 
Mimi sioni big deal ujio wa hawa Brazil kwa sababu kwanza wameisha tinga South wanacheza huko, watacheza Zimbabwe kisha ndio Bongo..Utaweza vipi kuitangaza nchi yetu hali sisi wenyewe wavivu wa kujitangaza toka mwanzo..Hii ni kampeni ya ndani kuwafurahisha Wadanganyika tu hakuna mpya. Kama wangetinga Brazil na kuweka kambi, hapo tungezungumza makubwa zaidi lakini maadam hadi sasa hatuna timu hata moja inadhihirisha uchovu wetu ktk kuitangaza nchi yetu.
 
Back
Top Bottom