Waziri wa Kaskazini
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 6,980
- 14,741
UJIO WA BILL GATE TANZANIA.
Nakumbuka Mwaka 2008 Rais wa Marekani GEORGE
BUSH alipotembelea Tanzania na kumwaga Pesa kiasi
cha Billion Tsh.700. Siku hiyo nilifuatilia mjadala mkali
TBC uliowahusisha Mtangazaji Tido Mhando, Prof.
Azaveli Rwaitama, Dr. Sengondo Mvungi na Prof. Mwesiga Balegu. Niliwasikiliza wasomi wachambuzi
vizuri hoja zao zilikuwa hivi;
1. Dr. Mvungi "As a nation We need to think Globally
but act Locally" "Ujio wa George Bush tusiuchekelee
kwakuwa wazungu huwa wanatega mitego ya miaka
50 hadi 100 mbele wakati sisi waafrika uwezo wetu wa kufikiri ni MACHWEO na MAWIO."
2. Tido Mhando. "Kwahiyo mnataka viongozi
wachukue hatua gani ili tusije tumbukia Shimoni?"
3. Prof. Mwesiga "Sera ya nje ya Marekani
wanasema,We neither have permanent friend nor
permanent enemy but permanent interest, tafsiri yake "Hatuna rafiki wakudumu wala adui wakudumu
bali Maslahi ya kudumu". Kwahiyo tuwe waangalifu
sana hii pesa ya Bush inawezekana ni chambo na sisi
ni samaki.
4. Prof. Rwaitama. "Ngoja niwaambie viongozi wetu
tena wanielewe wasipaniki kama kawaida yao. Mambo yaliyomleta George Bush sio kutuleta pesa bali
ni mambo manne makubwa"
i) Bush ni mwanahisa wa BARRICK GOLD MINE hivyo
amekuja kuangalia maendeleo ya migodi na
kutupumbaza ili watunyonye vizuri.
ii) Baada ya "September 11 terrorist incident in USA" Marekani alisambaza walaka Dunia nzima nchi zote
zitunge sheria ya ugaidi, Kenya ambao pia ni marafiki
wa Marekani waligoma na kusema wao wana
matatizo yao hilo ni la Marekani lakini Bunge la
Tanzania lilitunga sheria harakaharaka hivyo kitendo
hiki kiliwafurahisha Marekani kwahiyo ziara ya George Bush Tanzania ni kujenga urafiki wa muda na
sisi ili baadae wavunje rasmi urafiki na kenya na
kuhamisha Kambi yao ya kijeshi iliyopo Kenya "USA
MILITARY BASE" na kuiweka Tanzania.
iii) Baada ya China kupenyeza bidhaa zake nyingi kwa
nchi Masikini na Tajiri sasa USA inajaribu "ku- descourage" speed ya China kufanya biashara na nchi
hizi masikini ili awekeze viwanda vyake kwa nchi
kama Tanzania kumkabili mchina.
iv) Marekani wameshtuka kuona uchumi wa mataifa
makubwa ya Ulaya unaimarika kwa kufanya biashara
na yaliyokuwa makoloni yao"PROTECTORATES" sasa USA kwakuwa hakuwa na Makoloni "PROTECTORATES"
ziara ya George Bush ataelekea Rwanda ktk
kukamilisha mpango wa kuvuruga mahusiano kati ya
Ufaransa na yaliyokuwa Makoloni yake (Rwanda)
kwakuwa Ufaransa wamejisahau kusimamia
makoloni yake hivyo Kum Ufaransa ni kufungua milango mipya ya kibiashara.
MATUNDA YA ZIARA YA BUSH 2008.
A. Tanzania imetoa mji wa kigamboni kwaajili ya
ujenzi wa mji wa kisasa "USA INVESTMENT"
B. Kuanzishwa kwa Kiwanda cha Net/vyandarua
Arusha cha Wamarekani ambacho sasa kimedhibiti uingizaji wa vyandarua toka China.
C. Mpango wa Rais Kikwete kupitia mikataba ya
madini na kurekebisha baada ya kuunda kamati ya
ku-review mikataba iliyomhusisha Mbunge
Machachali wakati huo "Zitto Kabwe" ulikufa kifo cha
mende na kuruhusu upo Raji mkubwa wa rasilimali za nchi.
D. Ufaransa na Makoloni yake hawapatani tena tayari
makampuni ya Marekani yameweka kambi katika
"PROTECTORATES" za Ufaransa. Mfano Rwanda.
E. Baada ya China kupora tenda kwa Wamarekani ya
Mradi wa Gesi asilia Mtwara Juzi Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi kuzindua mradi mkubwa wa
Marekani ambapo ameridhia Bomba la Mafuta ghafi
kupitishwa tanzania kwa hesabu (Arithmetics) lengo
ni kumjibu China na kumpoteza East Africa.
RAI YANGU.
1. Ujio wa Bill Gate isiwe cheleko kwa Tanzania hasa Baada ya mgogoro kati ya Tanzania na Makampuni ya
madini ya USA "The Giants"
2. Bill Gate ni Taasisi sio "An individual" na kama
mlisikiliza maneno yake alisema "Taasisi ya Bill Gate
imetenga Tsh. 777 Billion"
3. Kwa wanaofuatilia siasa za Marekani Mtakumbuka mara baada ya Donald Trump kuapishwa Rais wa USA
kikao chake kikubwa cha kwanza alikaa na matajiri
wakubwa wa Marekani "The Bill Gates" tunadhani
walipe ana mkakati gani? Tunahitaji uangalifu.
4. Ni wakati wa Rais Magufuli kusikiliza ushauri wetu
wasomi na wataalamu kuliko kukanyaga moto wakati mwili una ganzi kutahamaki ganzi itakapoisha
tunaimba wimbo mmoja.
P