Ujio wa Asha-Rose Migiro----Tafakari kisha weka maneno kwenye hii katuni

Senior member inaelekea huyu mama Migiro unachuki nae, pengine amekukosea, lakini huko mimi siingilii kwani mtu kama humpendi ndio humpendi, mimi si mwana siasa, sisupport chama chochote, na wala sipigi kura, huu ndio msimamo wangu, lakini misemo yako kuhusu huyu mama inaonyesha CHUKI KUBWA, Sijui mwenzetu ulijuaje kuwa muda wake haukwisha ila alichemsha, na kama ulisikia (Kama msikilizaji na muelewaji) nini Ban Ki Moon alisema wakati alipokutana na vyombo mbali mbali vya habari duniani kuhusu utendaji wa kazi wa Migiro,(Je Ban Ki Moon Muongo? wewe unajua zaidi?) na kwamba anabadili team nzima, je hiyo team nzima ilichemsha? au Migiro peke yake? na kama team nzima ilichemsha basi kuna walakini hata kwa mwenyewe Ban Ki Moon, itakuwaje team yote iliyochini yako ichemshe, ndugu yangu fanya kwanza uchunguzi kabla hujasema, naamini jamii hii ni ya kusema kweli na yenye uwazi na pia ni jamii ya kuelimishana sasa tukiwa tunakurupuka kusema mambo tutafika? ni kweli lazima kuheshimu fikara za kila mtu lakini je hata kama hazina ukweli na zinasemwa kwa misingi ya chuki?
:shock:
 
Mama atawanyima sana usingizi nyinyi wanamakundi- Ndio hivyo imekula kwenu na nusura yenu ni kuvunja makundi hayo kama kweli mnania ya U-urais na rahisi kuupata.
 
Senior expert member mbona una hasira? ni kweli ng'ombe akivunjika guu hurudi zizini, lakini Migiro hajavunjika guu (Fatilia kwa Kina) pili hachaguliki je kwa nani? na wapi? mbona majina ya wagombea uraisi hayajotoka? sasa hii kutajwa tajwa inakupa taabu? pengine hata mawazo hayo hana, japo kuwa inawezekana pia akawa nayo, kuchumbia sio kuoa, basi kutajwa sio ndio kuwa, na hata hivo ndio maana kuna KURA muhimu ni kutumia kura yako vizuri, japo mimi si mpiga kura, na hiyo kashifa kwa kweli hata mimi ningependa kuisikia, kuisikia tu, maana kashfa tu haimfanyi mtu kutokuchagulika, mfano uko hapa hapa kwetu viongozi wangapi wana kashfa nzito nzito na wanapeta? tena kwa ngazi zoooooooooote:eyebrows:
 
Huyo ni mwizi tu, Ebu nipeni picha ni kipi katufanyia kama kibaraka wa UN. Atatuuza tuwe waangalifu kwani kisha andaliwa tiyari ulimusikia kin moon. kuhusu ushoga? Tutakua mashoga si muda tujiroge mtaniambia kama tukiwa hai.
 
Nasikia JK alishaapa kuwa kamwe hatomwachia kiti mkristo!

Sasa mbona sijaona muislam yeyote aliye mstari wa mbele kugombea hata sasa??

Mimi pia ni mkristo lakini embu punguzeni kuupa nafasi huu udini namna hii..hatutafika namna hii..tizameni yanayotokea nigeria huko mjifunze.
 
Heri tumpe yeye kuliko hawa wana Magamba wa kiume waliochoka kifikra. Huyu tumelishwa sumu, huyu tujitolee, huyu tunaheshimiana nk. Badala ya kujadili namna ya kutatua matatizo ya watz wao wanawaza urais tu. Membe, Sitta, Lowasa wote mabazazi tu hawana jipya
 
Ndiyo, huyu ni chaguo la ccm kwenye uraisi mwaka 2015. Kumbuka tuna spika mwanamke hivo ni zamu kwa ccm kumteua mwanamke kuwa raisi 2015.
 
ACHA WANANCHI SAFARI HII TUKAJICHAGULIE WENYEWE RAIS WETU KWANI HAWA MARAIS WA KULETEWA KAMA CHUMVI JIKONI TAYARI TUNAVUNA HASARA ZAKE NCHINI

Kwa msingi huo 2015 kutakua na kura za kuchagua kati ya UADILIFU NA UTENDAJI ULIOTUKUKA kwa upande mmoja versus uchaguzi kwa kutegemea kwamba MTU KAUMBWA NA JINSIA GANI katikati ya miguu.

Uchaguzi kwa kuzingatia msingi huo wa pili tayari WaTanzania tunaendelea kuvuna stahili zetu za DOUBLE STANDARDS kila uchao toka kwa Anna Makinda bungeni tuliemchagua kwa kuegemea jinsia yake na UTENDAJI ULIOTUKUKA tukaumwaga nje kwa jina la Samuel Sitta mzee wa STANDARDS AND SPEED iliothibitika.


Ndiyo, huyu ni chaguo la ccm kwenye uraisi mwaka 2015. Kumbuka tuna spika mwanamke hivo ni zamu kwa ccm kumteua mwanamke kuwa raisi 2015.
 
yapi aliyoyafanya mazuri mpaka mpendekeze, yeye si ndiye aliamasisha JK Mbayuwayu kuruka kila siku Majuu akiwa waziri wa mambo ya nje.
 
huyu KUKU HANUNI vp? mbona anataja status za members badala ya majina yao?

NDUGU YANGU ZUMBEMKUU ASANTE KWA SWALI LAKO, NIMEKUELEWA NITAKUA NATAJA MAJINA, KUKU MIMI NILIKUWA NATAJA STATUS KWA KUELEWA KUWA UKISEMA RAIS ANAJULIKANA NI NANI - UKISEMA SPIKA ANAJULIKANA NI NANI, BASI ZUMBEMKUU USIPATE TAABU HILO JAMBO DOGO TU NITATAJA MAJINA SISI WOTE WANA JF NA LENGO LETU MOJA. MUHIMU HOJA KUELEWEKA, BASI ONDOA MKONO SHAVUNI NA:smile-big::smile-big:
 
Back
Top Bottom