Ujio wa AMAPIANO umenikosha sana

Memtata

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
552
1,800
Habari wakuu,

Niwaambie ukweli leo mi huwa sijui kucheza kabisa niwapo club, sasa wakati ule wale ma broman na masister du wanaoujuaga kucheza kwaito walivyokuwa wakijishaua kila ikipigwa kwaito nilikuwa nakwazika sana.

Yani mi nipo club kama mlevi nacheza zangu hovyohovyo a'fu ikipigwa kwaito unaona watu wanaanza kujipanga wanacheza kwa utaratibu "maza saka!" Nani kawaambia ushenzini tunachezaga kwa utaratibu? Kwani tunatoa show hapa!!?

Sasaivi imekuja 'amapiano' mtindo huu umenifurahisha sana, kwanza hakuna code ya uchezaji just kucheza hovyohovyo ilimradi kuendana na tone alafu imefunika kabisa ujinga wa kwaito.

 
Back
Top Bottom