Ujinga wetu ndio umasikini wetu

i-77

JF-Expert Member
May 23, 2015
724
806
Tunajifunza kiingereza ili tuwasiliane na wanyonyaji VIZURIi;na tukinyonywa vizuri tunalalamika VIBAYA.

Hakuna nchi maskini duniani kama MAREKANI,na hakuna nchi tajiri duniani kama nchi zinazoitwa "developing countries"

Shida ni moja tu;tumekubali kupimwa kwa vigezo vya pato la taifa(nation income[kodi,mishahara,ushuru,mauzo n.k!]),badala ya utajiri wa taifa (national wealth[madini,uoto wa asili,wanyama,nk]).

Tukiichukua Marekani na rasilimali zake zote (national wealth)tukagawanya kwa idadi ya watu wake(zaid ya ml 300) .haitokua sawa na tukiichukua Tanzania na rasilimali zake zoote (national wealth)tukagawanywa kwa watu wake (zaidi ya ml 45)

Chanzo kikuu cha kweli na cha asili cha national income ni national wealth(hapa ndipo tulipodanganywa ili tuibiwe)

Ujinga wetu umetuletea Paradox ya ajabu mno,wasiokua na utajiri(national wealth) ndo wenye pato kubwa la taifa (national income),na kinyume chake .

Wachumi waliomezwa na elimu ya mabepari wanakuja na hoja ya "resources utilization" ndo sababu ya Paradox hii.Hawataki kusema WIZI na Unyonyaji ndo umetuleta hapa.

Marekani na wenzake ni vibaka tu kama walivyo vibaka wa Tandale kwa Mtogole,Chamwino Morogoro,Ngamiani Tanga,Darajani Zanzibar,Soko la nyanya Makambako nk.

Siku marekani na ulaya zitakapoacha kuiba,kupora,kunyonya nk ndo siku watakayokua maskini.

Napata shida kutabiri siku ya mwisho wa wizi huu utakua lini ,kama soko la vipodozi vya kujichubua,ma-wigi nk linazidi kunawiri Afrika.Wametuibia mpka utamaduni na tunaununua wa kwao kwa gharama kubwa.

Dini,(hasa ukristo),lugha,uwekezaji nk ni orbits zinazotufanya Afrika tubaki kwenye wizi huu!!.

Kwa hisani ya:-

...NGUZO NOEL .R.
 
UZI WAKO HUU AKIUFANYIA EDITING PASCAL MAYALLA AU MSHANA AU YERIKO UNAWEZA UKAPATA COMMENTS NYINGI,PUNGUZA UKOROROO WA ARUSHA UNAPOTAKA KUZUNGUMZIA VITU SENSITIVE KAMA HIVI.
 
Back
Top Bottom