Ujinga wetu ndio uliotuponza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujinga wetu ndio uliotuponza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rubabi, Nov 7, 2007.

 1. R

  Rubabi Senior Member

  #1
  Nov 7, 2007
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wameongoza nchi kwa miaka 50 sasa na nchi inazidi kuwa masikini.Tulipata chance ya kuwaodoa hawa lakini tukawachagua tena!Chama chochote kikikaa zaidi ya miaka hata kumi na kuchaguliwa tena ofcourse lazima wajione invincible! CCM wanajua kuwa hata wakiboronga vipi(kuuza nchi,BOT kuwa personal bank)watanzania hawana ushujaa wa kuchagua chama kingine zaidi ya CCM.

  Tujilaumu wenyewe, tumekosa ushujaa, sasa tunakula ujinga wetu!
   
 2. C

  Choveki JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pokea tano Rubabi,
  Ila siyo kwamba ujinga wetu "ulituponza", bali "UNATUPONZA". Ni hivi, huo ujinga uliotuponza miaka ya nyuma bado unaendelea kutuponza sasa na utaendelea kutuponza miaka ijayo, kwani sote huo ujinga umetujaa sana, na kwa kiasi fulani ni kama tunaambukizana virusi vya ujinga!

  Watanzania sisi tunachoangalia ni kuwa majina ya dini ipi yemezidi nyingine sisiemu na kwingineko, wakata watu wanakufa mahospitalini bila kujali dini au madhehebu yao, umasikini umepiga kambi ya matofali ya zege na siyo maturubali, lakini hilo watu haliwabughudhi....Mtu anakubali kupewa rushwa kidogo tu halafu anauza kura yake, je huo ni ujinga ulioje? ...Miaka nenda rudi watu wanalia lia kutokana na umasikini na kuingizwa mjini na viongozi waliowachagua, cha ajabu ni kuwa baada ya miaka mitano tunadanganywa tena halafu tunawachagua watu haohao je tunategemea nini?

  Sasa hivi wengi wanamlalamikia ati muungwana anauza nchi au haijali nchi bila kufikiria au kuona kuwa kuuza nchi ni tatizo sugu nchini, limekuepo miaka nenda rudi na litaendelea kuwepo hadi tutakapoamka.

  Chukua mfano wa Radar, aloipigia debe ikanunuliwa ni huyo P****, pia akanunua Ndege ya Raisi (Chinga),tetesi ni kuwa ndo ameleta wale wakaguzi (ma editor) toka marekani ambao wanalamba mamilioni kwa wiki za madini, nk....Mtu huyo huyo tutampa kura zetu tena!, Na nakumbuka bajeti ya juzi juzi alipendekeza ati ile ndege ya Raisi iliyonunuliwa haifai hivyo itanunuliwa nyingine kwa mamilioni mengine ya Watz, nasi tukakaa kimya tena.

  Mfano wa mikataba ya Madini ni mazingaombwe na viini macho tu, ambavyo unatakiwa uwe huna akili kabisa ndiyo usielewe kwamba tumeingizwa mjini na jamaa wote bado wanatesa na bado tunawapa kura, na 2010 tutawapa kura zetu tena!

  Imetokea hii ya Richmond, ati sasa weshapewa na tenda za kusambaza/kuuza umeme nchini na bado tumekaa kimya kama makondoo yaliyonyeshewa!

  Na hao wawakilishi wetu(viongozi) hata macho wamegoma kupimiwa Tz, achilia mbali kuugulia muhimbili, KCMC au Bugando, wakipata vikohozi tu wanapanda ndege kwenda ulaya kupimwa na kutibiwa.....sisi bado tumekaa kimya tu na nduguzetu wanaishia kupasuliwa vichwa bila sababu

  Juzi hapa amechaguliwa makamu wa m/kiti wa sisiemu hata hapa kwenye JF watu wakawa wanaunga mkono ati huyu jamaa ni mzoefu na ameenda shule na kupewa sifa nyingi tu, mtu huyo alochaguliwa ameanza kutesa tangia uhuru, na ana zaidi ya mika 70 hilo hatuoni kuwa ni dosari, je tutaendelea kweli?....

  Naishia hapa, kwani mifano ni mingi kupita kiasi. Na umasikini unaendelea kutuua.Na hasira zinanizidia
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  inazidi kuwa mbaya zaidi ya kipindi kile cha UKOLONI kabla ya ccm kushika madaraka ?(yaani una maana tuna hali mbaya zaidi ya ile ya ukoloni??) ?? hapa sijaelewa !
   
 4. A

  Atanaye Senior Member

  #4
  Nov 8, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa maoni yangu-
  Ushujaa ulikuwepo kwa vishinikizo vya westi kantre. Opposition ilianza kama 'vigenge'(hapa na maanisha watu wachache bila sauti ya wananchi wengi) vya wasomi, na wale ambao walikuwa hawana sehemu ya kwenda kuwakosoa waliowakosea na waliokosa! Haya magenge kwa vishinikizo yalitaka Uongozi wa juu, Urais mmoja wapo badala ya kuwafumbua wananchi macho kwa yale waliyoyaona wakiwa Serikalini au ndani ya chama, hapa CCM. Si mpaka kampeni za Urais ndio wananchi vijijini(kwenye roots)walipojuwa kuwa kuna Vyama vya upinzani!
  CCM inajiporomosha yenyewe! we are yet to see the next elections!!
   
 5. A

  Atanaye Senior Member

  #5
  Nov 8, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uerevu wa watu ndio utakaondoa ujinga na ndio utaoupatia ufumbuzi tayari for next elections! CCM ilifanya hivyo kutukomboa kutoka kwa wakoloni na ndio maana mzizi wake umekuwa kwa miaka hamsini! Kichuguu hiko....
   
 6. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kichuguu tena si kidogo ! ccm went through a lot, lakini watu wanaona nje nje tu !

  (Mod: inakuwaje nikitaka kusign out inakataa ??)
   
 7. K

  Koba JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...Kada najua this sound so bad lakini its just a fact,nina uhakika mkoloni angekuwepo leo hii tungekuwa mbali zaidi kuliko hao CCM wanaotutia umaskini everyday
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hii inanikumbusha...
  ...maana kubadili serikali
  si kama kubadili nguo
  , ...'wengi' walilalama 1995 kunyimwa KIKWETE na kupewa MKAPA, leo hii ndio kwanza miaka miwili ya 'utawala' wa KIKWETE, CCM inaonekana haifai, bora 'Upinzani'!,

  SWALI ni je, chama gani basi angalau kinamwelekeo/chafaa kututawala? CHADEMA? CUF? NCCR? TADEA? TLP?... ushindi wa 80% aloupata KIKWETE 1995 ni ishara tosha 'wananchi' wengi bado wapo tayari kumpa kura nyingi za ndio Rais toka CCM hata kama kura za ubunge/mwakilishi atapewa 'mpinzani', kwanini?

  ...kwa mtizamo wangu, mpaka pale Opposition parties zitapoamua kufanya coalition na kumsimamisha mgombea mmoja 'mahiri' kwa kiti cha urais ndipo hapo CCM itapoweza 'kutikiswa' kiduchu, la sivyo hadithi itaendelea hivi hivi "tukistahmiliana na joto la bakery madhali twautaka mkate!"


   
 9. A

  Atanaye Senior Member

  #9
  Nov 8, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Urais sio suluhisho la opposition... Wananchi waliosimama kichuguu wanataka kulainishwa (kuelewa vyama vyao na sio viongozi) hata kama ni kweli kwamba viongozi ndio 'chama' basi wale waliotoka ccm (walikuwa viongozi wazuri tu) wangechaguliwa!
  ;)
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Nov 8, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  kwa sababu umejiandikisha kwa jina jingine baada ya kufungiwa kwa wiki moja...
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hakuna improvement kwa hali ya maisha ya mtanzaniak wa miaka hamsini.

  labda kulikuwepo na afuweni miaka kumi ya mwanzo ya nyerere, lakini baada ya hapo kumekuwa na wingi wa ubadhirifu na manufaa machache kwa mtanzania wa kawaida
   
 12. A

  Atanaye Senior Member

  #12
  Dec 30, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Je ni ujinga uliowaponza kina Kibaki. Je huu ujinga utawaponza CCM elfu mbili na kumi?
   
 13. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2007
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Wakati mwingine mabadiliko ni wakati na nafasi. Ukishindwa kuutumia nafasi yako vizuri inaweza kukuchukua miaka mingine 50 kuitafuta bahati hiyo au usiipate kabisa mpaka unakufa.

  Watanzania walikuwa na nafasi ya kubadilisha serikali mwaka 1995, tukaboronga na CCM ikajifunza kutawala kwa umoja wa wale waliomo ndani ya system.

  Hutakiwi kuboronga unapopata nafasi kwa sababu hiyo nafasi inaweza kuwa ya mwisho.
   
 14. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  nilivyoona aliyeuliza hili swali nikashangaa!!lakini nilipogundua ni wewe ndugu yangu kada mpinzani nikakumbuka kuwa ni kawaida yako sasa swali lililofuata ni kuwa ndugu yangu kada..kwa kipindi hichoo choote cha miaka 50 labda hujawahi ishi Tanzania ama?au labda nikuulize nicely..when was the last time kuishi Tanzania??as kwa mtu mwenye akili timamu na aliyeishi Tz kwa hivi karibuni angeona aibu ku ask such qns though we all use our right ya freedom of speech
   
Loading...