Ujinga wetu ndio uliotufikisha hapa

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,143
1,291
Baada ya raia wa Kenya kuhutubia kwenye mkutano wa kimataifa kwa bonde la olduvai liko Kenya ,hivi sasa kila kona na katika mitandao ya jamii watu wanapiga kelele kuwa mlima kilimanjaro upo Tanzania ,bonde la Ulduvai liko Tanzania .Kelele zimekuwa nyingi sana kana kwamba hivi vituvimegunduliwa jana .Suala la msingi jirana zetu wa Kenya kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia jina la mlima kilimanjaro katika kutangaza biashara zao,wamediriki hata kuipa jina mojawapo ya ndege zao na kuiita kilimanjaro.
Kwanini miaka yote iliyopita tumeshindwa kutangaza vivutio nyetu vya asili mpaka Kenya wakatupiku , ujinga wetu ndio uliotufikisha hapa,
Katika nchi za Ulaya mara kwa mara utaona kwenye magazeti Kenya ikijitangaza hususa hoteli zake zilizoko kwenye beach na mbuga za wanyama. Lakini kwa Tanzania hii issue ni tofauti hata katika zile cab nyeusi maarufu za London huoni matangazo ya Tanzania , Utaona kenya na Afrika kusini zinaongoza kujitangaza. Ukipandandege zinazotoka Ulaya abiria wengi huteremka Nairobi na wachache wao huteremka Dar .Serikali inabidi ifanye mkakati wa kutangaza vivutio nya nchi sio watu binafsi kutangaza kuwa bonde la olduvai liko Tanzania kwenye Facebook
 
Back
Top Bottom