Ujinga wa baadhi ya watanzania ndio mtaji wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujinga wa baadhi ya watanzania ndio mtaji wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anyisile Obheli, Jun 24, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Elimu duni na kutojitawala kifikra kumetufanya watanzania kuwa ngazi ya mafisadi, kila chaguzi zikaribiapo, tazama mtu amekuwa kiogozi tangu mimi nazaliwa na sasa nina umri wa miaka 31 jimbo lake hakuna alichokifanya hivi tuna msubiri nani atwambie mtu huyo hatufai?

  Kweli hapo panahitajia elimu ya chuo kikuu kutambua? ama ni yale yale ya tumerogwa?

  Wana JF tunalionaje hili....tusaidiane maana hapa ni uwanja mpana
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo siyo elimu tu ni mind set za watanzania walio wengi pamoja na njaa. Fikiria wanafunzi (wajinga) wa vyuo vikuu kufikia hatua ya kumchangia mtu kama Kikwete pesa eti za kuchukulia fomu wakati huyu jamaa amekwiba hela kibao na anajenga kasiri lake pale chalinze.

  Pia usifikiri kila majimbo CCM wanashinda suala ni wizi wa kura hasa vijijini. Lakini kwangu mimi tatizo kubwa la kuwaweka CCM madarakani miaka yote hii ni kutumia njaa na ujinga wa wananachi walio wengi na wizi wa kura.
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni kweli Magenzi,
  hapoa ndipo utakapo gundua kuwa ujinga ni sehemu ya maisha ya mtanzania bila kujari elimu aliyonayo mtu, mimi binafisi nimegundua kuwa ujinga hauondolewi kwa mtu kuelimika, maana kama
  si hivyo basi wasomi wengi wangekuwa wanaongoza kwa kuwaelimisha wale non-wasomi juu ya nini kinatakiwa kufanya ili kuwakwepa watu waliofahamika hawana msaada kwa maendeleo ta nchi
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ...mtaji wa ccm ni ujinga wetu wenyewee heee.!!!
  ...kwa kuwa msituni jamani hatuwezi...!!
  ...wala bunduki hatujawahi tumiaaa....!!!

  ...akili tunazo Mola katujaria...!!!
  ...sasa ni wakati wa kuzitumia vizuri hiii..!!

  ...hao ccm hawatushiki mikonoooo...!!!
  ...kupiga kura eee!! ni jukumu lako mwenyewe..!!

  ....akili ni zetu tuzitumie vizurieeeeeee....!!!! fade out
   
 5. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #5
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wizi vile vile ni sehemu ya mtaji wao....
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Binafsi huwa nafikiri mtaji mkubwa wa CCM ni umaskini wa watanzania. Hizi habari za bunduki inaweza kuwa ni mbali sana huko. Marekani wanafanya mabadiliko makubwa ya uongozi bila kutumia bunduki wala kuhofia suala la bunduki. Hapa kwetu umaskini mkubwa walio nao wananchi unawafanya wapumbazwe na bahasha za khaki zinazotolewa na CCM kununua kura. Mmeona wenyewe huko Dar es salaam ambapo wapiga kura wamekuwa wakiwashambulia TAKUKURU eti wanawazibia ulaji. Ndiyo maana CCM kila wakati imejitahidi sana kuwafanya watanzania kuwa masikini zaidi na zaidi, tena wa kifedha na kimawazo (kuwajengea shule zisizokuwa na walimu ili wanaokwenda huko watoke wajinga kama walivyoingia). Na hapo ndipo ninaposema wengi wa wanaojipendekeza kwa CCM hivi sasa wanasumbuliwa na njaa, si kwamba wameona CCM imefanya lolote bali wanatafuta kupona njaa zao. Umaskini!!!!!
   
 7. m

  muafaka Senior Member

  #7
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Si kila mtu ni mjinga au wapumbavu nadhani usichanganye fikira zako za kisiasa kwa minds za watanzania wote in general. I think you are wrong !!, This is a democratic world na mtu asipoendana na mawazo yako doesn't mean kwamba ni mjinga, it is his/her own choice. And if many choices falls on more on the side you unfortunately dislike, then we just have to accept that, neither should think the other ni mjinga. Let the freedom of expression, freedom of choice prevail not your dictated views. Nadhani jamiiforums haiko owned na chama cha siasa, that is my understanding it is owned by people who wants to promote freedom of expression to create a platform where even our leaders can ultimately depend for different views from diverse Tanzanian population. THE BEST WAY NI KUJENGA HOJA watu wata support kama hoja ina maana, let us learn to respect one another that way tutajenga Tanzania inayoendeshwa na fikra za Watanzania. Remember you create your own credibility and natural forces create an envelope of dependable population around you, YOU CAN'T BE CREDIBLE BY FORCE.

   
 8. a

  alibaba Senior Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani wakulaumiwa hasani Wanasiasa wa Vyama vya upinzani waliojiweka katika vikundi vidogovidogo kwa Maslahi yao binafsi, ikiwa ni pamoja na kujipendekeza kwa CCM na Serekali yake na kupokea kitu kidogo wakati unapojiri. Huhitaji shahda kujua kuwa kwa mtaji huo wa wapinzani kamwe, narudia kamwe hawawezi kuitikisa CCM. mimi nawalaumu wao na wao ndio Wajinga wetu.
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  safi sana mkuu, Muafaka.
  nafikiri umeonesha kuwa na uwezo mkubwa kusikia maumivu juu ya hii kitu, lakini miye nadhani,
  umefika wakati wa kutumia zaidi hata elimu ya kuzaliwa ikiwa ile ya kukariri vitabu vya mashuleni,
  itaonekana kutokukusaidia sana, sijui labda ulikuwa unajibu hii topiki baada ya kuwa na hanng over
  ama basi tu umeamua kuonesha kuwa wewe ni kiongo mkuu wa watu wanao kurupuka sana,

  kwani hiyo topiki imekukwaza wapi? pengine uvue hiyo kofia uliyoivaa then utaweza kuona ulichokisoma na ulichokijibu viko sawa? ama, na kama haviko sawa umekaa wapi katika hilo
  naona umejikanyaga sana, lakini ukweli uko pale pale mtazamo wako na wangu hauwezi kuenda sawa
  kwanza hilo ujue, unapocheka miye hununa, unapokula kinyesi miye hula sambusa, hivyo hatuwezi
  kuwa sawa, unapolala mimi huamka, sasa kama ni kweli kuwa watanzania wote siyo wajinga, basi ni kweli kuwa welevu wote siyo watanzania, utajijuaje wewe kama si mjinga? si mpaka uambiwe?

  hivyo hupaswi kupinga uambiwapo wewe ni mjinga, nadhani ungetumia nafasi hii kuuliza ama
  kutaka kujua kwa nini,,,ujinga uwe mtaji wa ccm? na siyo kuleta blah blah nyingi,
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JK ajivunia mafanikio sekta ya elimu
  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete
  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesifia mafanikio ya serikali yake katika sekta ya elimu kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
  Akiwa katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kampeni, aliwaeleza wananchi kuwa ingawa kuna watu wanapita wakiibeza serikali kuwa haijaafanya kitu, dunia imetambua mchango wa serikali katika kuandikisha wanafunzi wengi wa shule za msingi na wameamua kuipatia tuzo.
  Rais Kikwete alisema hatua ya serikali kufanikiwa kuandikisha wanafunzi kwa asilimia 99 ndiko kumeifanya dunia kutambua mchango huo mkubwa na hatimaye kuamua kuipa serikali tuzo.
  “Watu wanatubeza, lakini dunia imetutambua kuwa sisi ni kiboko, tukiahidi tunatimiza, sisi ni waaminifu, tuliahidi kuandikisha shule za msingi kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule na tumefanya hivyo, huwezi
  kutulinganisha na vyama vingine,” alisema. Kikwete alisema kuwa wakoloni hawakujenga shule na kwamba serikali mara baada ya Uhuru ndiyo ilianza harakati za kujenga shule na yaliyoonekana hayawezekani kwa miaka yote yamewezekana.
  Alisema safari ya kila mtoto kuwa na kitabu chake imekaribia na kwamba baada ya muda mfupi, wanafunzi hawatakuwa wakichangia vitabu.
  Alisema serikali ya Marekani imeshasaidia vitabu 800,000 na mwakani itatoa vitabu vingine milioni 2.4 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Rais wa Marekani, George W. Bush.
  Alisema serikali imejitahidi kukarabati hospitali ya Wilaya ya Kongwa na itaendelea kuiboresha pamoja na kununua magari zaidi ya kubebea wagonjwa ili kurahisisha ubebaji wa wagonjwa wakati wa dharura.
  Wakati huo huo, Kikwete leo anatarajia kuanza kunguruma katika visiwa vya Unguja na Pemba katika harakati zake za kusaka kura kwa ajili ya kuingia Ikulu kwa awamu ya pili.
  CHANZO: NIPASHE
  MY TAKE
  Naona JK hausiki na ubora wa Elimu kama tafiti mbalimbali zinavyosema.
  Lengo naona ni kujenga kizazi cha mbumbu ili iwe rahisi kuwarubuni kwa khanga,kofia,shati,fulana
   
 11. P

  Pax JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hii kauli imekuwa ikitamkwa sana lakini sikuwahi kuona katika khali halisi nini maana yake. Pamoja na wizi, ghiliba na matumizi ya vyombo vya dola na watumishi wa idara za serikali kufanikisha CCM kubaki madarakani, hali imekuwa tofauti maeneo yenye wasomi na kiasi kikubwa yenye maendeleo. Angalia sehemu CHADEMA waliposhinda ni maeneo ambayo kuna maendeleo na uelewa mkubwa. Mfano Wakati wachagga wa ROMBO wakimlaani Basil Mramba kwa kuwadhalilisha kwa wizina kuwakejeli watu wale nyasi lakini ndege ya Raisi inunuliwe, Monduli kwa Lowassa wameona wizi wake ni ufahari. Hii ni tofauti ya jamii mbili tofauti zenye maendeleo tofauti. Warombo wana maji, umeme, tena barabara ndio inawekwa lami, sidhani Monduli kama wana maendeleo haya. Mramba alijaribu kujitetea oooh barabara hii nimeileta mimi na msiponichagua lami haitawekwa yote lakini wachagga wamesema HAPANA, HUTUFAI wewe.

  Mikoa ya kusini, Morogoro, Dodoma na kwingine wametia aibu kubwa. Wamesaliti nafsi zao na maisha yao. Mtu analala kwenye nyumba ya tembe, hajui godoro, bati wala saruji achilia mbali maji safi ya kunywa lakini kwa kuwa shida imemaliza uwezo wake wa kufikiri, hawajaweza kuiga wenzao wa mikoa yenye wasomi na maendeleo. Niliamini mikoa mingi ya kusini wangeiadabisha CCM maana kuna shida na tabu za ajabu lakini hawakufanya hivyo. Nawapa pole sana.

  Mtaji waCCM ni ujinga wa wananchi, imedhihirika wazi sasa kuliko wakati mwingine wowote.

  Struggling is nature's way of strengthening, wapenda mabadiliko tutakumbukwa daima kwa naman tunavyoendelea kuikomboa nchi yetu. Tuendelee kupigana na kuangalia mbele maana ukombozi umekaribia. Tukilala tutamuona Ridhiwani na Januari Makamba wakigombea uraisi hivi hivi, tuliosoma nao hawa tunawaelewa fika hawana lolote zaidi ya pesa haramu za wavuja jasho wa hii nchi.

  Nawasihi wenzangu wote tusife moyo, Dr Slaa, Zitto, Mdee, Wenje, Godbles Lema, Mrema A, Marando, Lissu, Mnyika, Wenje, Mbowe na wengine wote kazi ndio imeanza, liko vuguvugu msiloweza hata kuelewa ukubwa wa nguvu yake lipo nyuma yenu, msifadhaike mioyoni mwenu, kuweni imara maana Mungu yupo pamoja nasi. Vita hii sio yenu peke yenu, ni yetu sote wapenda maendeleo. Dr Slaa endelea kukataa matokeo kwa kutoa vielelezo vya uhuni wa NEC, kamwe usiisaliti nafsi yako na sisi wapenda mabadiliko ya AMANI
   
 12. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu ni kweli kabisa ujinga ndio mtaji wa ccm, unapokuwa huna maendeleo na wala huyatafuti hata nani akuhubirie umuhimu wake hutauona,utaona kama anayekueleza hayo mambo ni mwendawazimu au ndoto.Yaani kuna watu wanaishi maporini huko wanalala sehemu ambazo hata huwezi kuelewa na ukiwaeleza maendeleo hawataki,wao wanjiona maisha waliyonayo ndio mazuri.Wanahitaji msaada mkubwa,shaka wataupataje wakati wasanii ndio hao wanarudi huku chama chao ndio hicho hata dira hakina tena.
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aliyetamka hayo maneno ni "PROFESSOR"

  sasa wewe ni nani usiyetaka kuamini?
   
 14. P

  Pax JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hatuamini bila kugusa, wewe vipi, nimekuwa mwana CCM mimi niamini ahadi hewa bila kuona maendeleo miaka yote CCM imekaa madarakani? ebo, wewe vipi tena, wamekuchakachua tayari mafisadi eee. Hebu tuache tuko vitani hapa, kama unataka uingie kazini ka hutaki endelea kuamini ahadi hewa tu.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Apo lazima umuacknoledge professor Baregu aliona Mbali.
  No wonder shule za kata zaongezeka uku idadi ya walimu inasikitisha
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Umasikini na CCM vina uhusiano wa damu. Sehemu zote wanazoshabikia CCM ni masikini na mara nyingi hata wabunge wa maeneo hayo ni wanyonyaji wakubwa wanaonufaika na umbumbumbu wa wananchi wao. Hivi mkoa masikini kama Mtwara una raha gani kuwa chini ya ccm kwa miaka karibu 50 na ni mkoa mojawapo ya masikini hohehae?
  :A S angry:
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ukita uamini hayo maneno angalia Tshirt na Kofia za CCM zinavaliwa zaidi na watu wa namna gani,
   
 18. m

  mzeewadriver Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwenye kampeni tulivyojitokeza mlitusifia kwamba sasa watanzania tumeamka na kwa ushaidi wa picha mkaweka lakini sasa hivi mnaanza tena kututusi kwamba hatuna akili, duh jamani mbona hueleweki? Lazima penye ushindani mmojka ashinde, na kwani ndo hakutakuwa na uchaguzi tena? nadhani huu ni wakati muafaka wa kuangalia wapi mtu aliteleza na ajipange vipi, lakini wewe kama hii miaka mitano utaendelea kusema watanzania hatuna akili ukisubiriwakati wa kampeni uje useme tumeamka na tuko tayari kwa mabadiliko, hadithi itabaki ni ile ile.
   
 19. m

  mzeewadriver Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Uko vitani na nani? hakuna vita hapa. Kama upepo umeenda vibaya angalia wapi pakuweza kurekebisha kwa awamu ijayo siyo kuendelea kutisha watu vita vita unaijua vita wewe, au ndo nyie mnaotaka kuneemeka pindi machafuko yatakapotokea?
   
 20. m

  mzeewadriver Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nini maana ya maisha?
   
Loading...