Ujinga Ni Nini?

Gigo

JF-Expert Member
Aug 6, 2006
456
46
Rushwa...wizi...!?
Japo elimu sio wingi wa vitabu ulivyosoma !!bali hata Ufahamu Ni Roho (spirit) uliyozaliwa nayo ...sasa Inapokuaja kwenye tuwe Ujinga!? wajinga?..Nataka kujua zaidi! Hivi Ujinga ni nini?
 
hili ni swali muhimu na kuna haja ya kulitafutia jibu. waweza kusshangaa wasomi wetu wa chuo kikuu wanajiona waelevu na intellectuals lakini ndo hao wanasaini mikataba ya buzwagi nk, sasa hawa wameelimika? mimi naamini sana kwamba kuna watu ambao hawajasoma lakini ni waelevu na sio wajinga na kuna wasomi kibao ambao hamnazo.
 
Mjinga ni yule asiyejua kuwa WOGA ni sumaku!

Ukitishwa na mbwa Usipoogopa na mwenzio akaogopa...mbwa anamfuata na anapata kitoweo kwa yule aliyeogopa. Mbwa anamfuata yule mwoga.

Ujinga ni kutokujua kuwa WOGA ni sumaku. Ujinga ni kumpa mbwa WOGA bila kujua kuwa umempa pia kitoweo cha mnofu wa mwili wako.

Ujinga ni kutaka kumua mbwa kwa kuwa amekudhuru badala ya kuua WOGA.

Hakuna ujinga zaidi ya kutokujua kuwa hisia za mwanadamu kama woga , wasiwasi, chuki na hisia hasi zote ni sumaku ya kuvuta kile unachokielekezea hisia hizo.

Ujinga sio utu wala sio ubinaadamu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom